Na Mwandishi Maalum, Lindi
Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Hamis Livembe, ameagiza matawi ya Jumuiya hiyo nchini kufungua akaunti zao katika benki ya NMB.
Livembe alitoa maelekezo hayo, juzi, mkoani Lindi, wakati wakiingia makubaliano ya kuimarisha uhusino na benki hiyo, kuelekea mkutano mkuu wa jumuiya hiyo.
Alisema wamekubaliana na benki hiyo baada ya kukubali kugharamia mkutano huo, unaotarajiwa kufanyika mkoani Dar es Salaam, Novemba 17 na 16, mwaka huu.
"Tumeingia makubaliano ya kuimarisha uhusiano na benki ya NMB, hivyo niagize matawi yetu yote, kuanzia Wilaya, Mikoa na maeneo yetu maalumu ya biasahara waanze kufungua akaunti zao katika benki hiyo", alisema.
Pia Livembe alisema hali ya biashara inaendelea vizuri licha kuwepo baadhi ya changamoto ikiwemo kuwa na wakusanyaji kodi wengi.
Alisema tangu serikali ya awamu ya sita ingie madarakani, kuna unafuu umeanza kurejea kwa wafanyabiashara.
Livembe alisema kuna baadhi ya kodi wanalipa lakini hazina maelezo, kwa mfano kodi ya huduma wanalipa hali kuwa huduma zote wanalipa.
"Tunaomba serikali kuliangalia suala hili kwani kodi zote tunalipa pamoja na ushuru, lakini bado kuna hii kodi ya huduma bado hatuajaelewa ni huduma ipi tunalipa, wakati hizo huduma tunazilipia", alisema
Post a Comment