Benki ya NMB imewataka Wananchi kujisajili katika Mbio za NMB Marathoni Ili kwenda kuwasaidia wakina mama wenye matatizo ya fistula.
Akizungumza Afisa Mkuu wa Rasilimali watu Benki ya NMB Emmanuel Akonaay amesema lengo la kukimbia Leo ni kufanya ukaguzi wa njia kwa Mbio za Kilomita 5,10 mpaka 21 Ili kuangalia kama zimekamilika.
Akonay amesema Mbio za mwaka huu ni mwendelezo wa zile walizofanya mwaka jana kwani walipata kiasi cha Mill 400 hivyo Kwa Mwaka huu malengo Yao ni kapata kiasai Cha Tsh Mill 600 zitakazosaidia wakina mama wenye fistula.
“Leo tumekimbia zaidi ya watu miamoja wameshiriki hivyo tunaendelea kuwahimiza wakimbiaji kujitokeza Kwa wingi Katika NMB Marathon kwani licha ya kujenga Afya pia wanawasaidia watanzania”amesema Akonay
Kwa Upande wake Abraham Mlay Kutoka Kampuni ya Bima Sanlam amesema wameamua Kuungana na NMB Katika Marathoni hiyo kwani wanakwenda kusambaza upendo kwa watu Wenye uhitaji Kwenye marathon inayokuja kufanyika September 24 Mwaka huu.
Naye Maulidi Kitenge ameipongeza NMB Kwa kufanya Maandalizi ya marathan hiyo ya kujaribu njia hivyo imeonyesha ishara nzuri ya marathon itakayokwenda kufanyika tar 24 kutokana na namna walivyojipanga.
Amesema Mbio hizo zinamsisimko kwa zinarudisha fadhila kwa Jamii kwa kuwasaidia wakina mama wenye matatizo ya fistula na kwa pesa zitakazopatikana kutoka kwa washiriki zitakwenda kuwasaidia wakina mama hao.
Post a Comment