Gazeti la Uhuru linalochapishwa na Kampuni ya Uhuru Publicatins Ltd ambayo ni miongoni mwa Vyombo vya Habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), limeibuka mshindi wa kwanza katika uandishi wa makala kwenye maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani, Oktoba 9, 2022.
Julai mwaka huu, Shirika la Posta Tanzania lilitangaza mashindano mbalimbali katika kuadhimisha siku hiyo, likiwemo Shindano la uandishi wa makala yenye mada; "uhuru wa vyombo vya habari uliopo katika serikali ya awamu ya sita na ujenzi wa Tanzania ya kidijitali".
Mwandishi nguli wa habari Jacqueline Liana wa gazeti hilo lenye historia iliyotukuka nchini, ndiye aliyewezesha ushindi huo baada ya makala yake aliyoiandika kushika nafasi ya kwanza.
Wakati Jaqueline Liana akishinda na kuwa wa kwanza katika Uandishi wa Makala, Mgasa Robert kutoka COSTECH naye aliibuka mshindi wa kwanza Ubunifu wa TEHAMA.
Josephine Mlewa kutoka Shule ya Sekondary Msalato akawa mshindi wa kwanza Uandishi wa Barua, huku Astarick Mcharo kutoka Dodoma akiwa mshindi wa kwanza Ubunifu wa Graphics.
Mshindi mwingine ni Oscar Senya kutoka Shule ya Sekondari Mawenzi ambaye aliibuka wa kwanza Uandishi wa Insha.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia, Nape Nnauye, akimkabidhi Jacqueline Liana, mfano wa hundi ya zawadi ya Sh. Milioni 1.5 na cheti cha ushindi, wakati wa hafla hiyo Oktoba 9, 2022, jijini Dar es Salaam.
Post a Comment