Featured

    Featured Posts

NDEJEMBI AZINDUA MAJENGO YA MASJALA, AIAGIZA MKURABITA KUTOA MAFUNZO YA MIKOPO NACHINGWEA+video

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deo Ndejembi amezindua majengo ya masjala ya kuhifadhia hakimiliki za ardhi katika vijiji vya Mbondo na Nakalonji wilayani Nachingwea, Lindi, zilizojengwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali ba Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA).Akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa majengo hayo Oktoba 12, 2022, , Naibu Waziri Ndejembi ameuagiza uongozi wa MKURABITA uliongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, Mujungu Masyenene kuendesha mafunzo ya jinsi ya kutumia hakimiliki hizo kama dhamana kupata mikopo katika taasisi za fedha.

Ndejembi akizungumza na Mwenyeikiti wa Kijiji cha Mbondo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Hashim Komba.
Jengo la Masjala lililozinduliwa katika Kijiji cha Mbondo.
Ndejembi akikata utepe wakati wa uzinduzi wa jengo hilo.
Ndejembi na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Kasyenene  wakifunua pazia ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa jengo hilo/
Ndejembi  akiteta jambo na  Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Kasyenene 
 Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa MKURABITA, Kasyenene  akisoma taarifa ya taasisi hiyo ya ujenzi wa jengo hilo la masjala.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika kutano huo
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Hashim Komba akihutubia pamoja na kutoa shukrani kwa serikali pamoja na MKURABITA kwa kujenga jengo hilo la Masjala.

Baadhi ya wananchi waliopata hakimiliki ardhi katika Kijiji cha Mbondo.
Wananchi walioshiriki katika mkutano huo.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Naibu Waziri Ndejembi akitoa maagizo hayo...

 IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
 MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
 0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana