Na Scola Msewa, Kibaha, Pwani
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete ametoa wito kwa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) kutengeneza bidhaa zenye viwango vya ushindani nchini na nje ya nchi.
Dk. Kikwete amesema haya jana alipokuwa mgeni rasmi katika maonesho ya tatu ya Maonesho ya Uwekezaji ya Biashara ambayo yameanza leo Oktoba 6 na ameyafungua rasmi mchana na yanayoendelea kwenye viwanja vya stendi ya zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.
Aidha Rais Mstaafu Kikwete amesema hayo huku akitolea mfano wa bidhaa za mashine zilizotengenezwa na SIDO ambazo ni za kubangulia korosho kuwa hakuridhishwa na ubora wake wa utengenezwaji pamoja na umaliziaji wake kuwa haziwezi kuhimili ushindani sokoni.
Amesema kuwa hivi sasa ushindani wa mauzo ya bidhaa sokoni ni mkubwa hasa ikizingatiwa nchi ni mwanachama wa nchi za Afika Mashariki ambapo katika nchi jirani wametuzidi
"Nachukua fursa hii kuwaasa SIDO kupambana na ushindani wa bidhaa mnazozitengeneza na kuzisimamia kwa kujali ubora wake kabla ya kupeleka sokoni na kuzingatia kumudu ubora wa bidhaa ili kukabiliana na ushindani wa soko la biashara kwani hivi sasa soko ni huru katika nchi za Afrika na dunia nzima."
Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete
Post a Comment