RAIS SAMIA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI USHIRIKIANO KATI YA CHEMBA YA BIASHARA TANZANIA ZANZIBAR NA YA QATAR MJINI MJINI DOHA NCHINI HUMO, LEO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia utiaji saini wa makubaliano ya Ushirikiano kati ya Chemba ya Biashara ya Tanzania (iliowakilishwa na Rais wake Paul Koyi), Zanzibar (iliyowakilishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) Ali Suleiman Amour pamoja na Chemba ya Biashara ya Qatar iliyowakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Qatar Muhammed bin Ahmed Al Kuwarit. Hafla ya utiaji saini wa Mkataba huo umefanyika Doha nchini Qatar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Qatar Muhammed bin Ahmed Al Kuwari pamoja na ujumbe wake, Doha nchini humo tarehe 06 Oktoba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Qatar Muhammed bin Ahmed Al Kuwari mara baada ya mazungumzo, Doha nchini Qatar tarehe 06 Oktoba, 2022. Kushoto ni Rais wa Chemba ya Biashara ya Tanzania (TCCIA) Paul Koyi na kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC) Ali Suleiman Amour. (Picha na Ikulu).
Post a Comment