Na Christopher Lissa, Songwe
Mkuu wa Mkoa w Songwe Waziri Kindamba amesisitiza matumizi ya mbolea sahihi kwa wakulima ili kuongeza tija katika sekta ya kilimo.
Ameyasema hayo wakati akifungua Maonyesho ya Siku ya Mbolea Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika katika Viwanja vya Kimondo, Mlowo, mkoani hapa.
Akiwa katika Banda la Kampuni ya Mbolea Tanzania TFC, Kindamba alisema mbolea ya organic ni muhimu kwa wakulima kutokana na kutokuwa na madhara katika aridhi hasa wakati huu ambao dunià inakabiliwa na mabadiliko ya tabia nchini.
Amesema dhamira ya serikali ni wakulima kulima kulimo chenye tija kwa kutumia mbole sahihi isiyo na isiyo na madhara katika aridhi.
"Hii ndiyo mbolea tunayo hitaji kwa kipindi kirefu. Mbolea ya organic isiyo na madhara katika aridhi yetu,"alisema RC Kindamba.
Awali Kaimu Meneja wa Kampuni ya Mbolea Tanzania TFC, Kanjel Mlona alisema pamoja na aina nyingi za mbolea zinazo sambazwa na TFC wamepoke mboleo ya SBL ya Kenya kutokana na kuonyesha mafanikio makubwa nchini humo na kwamba ni organic na rafiki wa mazingira.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya SBL kutoka Kenya Joe Kariuki allmesa, mbolea hiyo ina uwezo wa hali ya juu na inasambazwa kupitia TFC hapa nchini.
Joe amesema kwa kutambua umuhimu wa wakula SBL kwa kushirikiana na TFC itatoa 'ofa' ya mfuko mmoja bure kwa kila Mkulima atakayenunua zaidi ya mifuko mitatu ya mbolea ya Kampuni ya SBL.
"Mkulima atakayekuja katika Viwanja vya Kiimomdo na kutembele katika banda la TFC akinumua zaidil ya mifuko mitatu ya mbolea ya SBL atapata mfuko mmoja wa kilo 25 bure"amesema Joe.
Amesema ofa hiyo haitaishia Songwe, bali kwa wakulima nchini kote ambao watanunua mbolea ya SBL.
Maonyesho hayo yameandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania, yatafungwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kesho Oktoba 13 mwaka huu.
Post a Comment