Na Scolastica Msewa, Kibaha
Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amewapongeza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni Nchini (BRELA) kwa huduma wanayoendelea kuitoa ya usajili kwenye Maonesho ya tatu ya Uwekezaji na Bashara yanayoendela kweye viwanja vya Stendi ya Zamani Mailimoja Kibaha Mkoani Pwani.
Amesema hayo wakati alipofika kutembelea kwenye banda la BRELA katika mkoa Pwani katika Maonyesho ya tatu ya Uwekezaji na Biashara yanayoendelea katika viwanja vya standi ya mailmoja na kufanikiwa kumkabidhi kijana Idriss Njeru cheti chake cha usajili baada ya kukamilisha hatua za usajili.
"Lazima vijana mjifunze kufanya kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za serikali kama jinsi wewe ulivyojisajili nakupongeza sana" amesema Waziri Kikwete.
Ameongeza kusema "vijana lazima mjisajili hasa kwa Kampuni za Teknolojia kwani ukijisajili unakuwa vizuri na unakuwa na ulinzi katika utendaji wa kazi zako.
Endeleeni kufanya kazi kwa njia halali na kuingia katika mfumo rasmi wa serikali, hongera sana kwa kupata usajili kwani hii ni sehemu ya kuchangia pato la taifa
Nenda ukawe balozi mzuri kwa vijana wenzako kua mjanja ni pamoja na kujisajili BRELA huku ukifanya kazi nzuri zenye kuzingatia maadili ya Mtanzania kwani kuna mambo mengi ya kuisadia jamii yanayopaswa kufanywa huku ukiwa ndani ya mfumo uliosajiliwa rasmi".
Post a Comment