Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano, Anna Nkinda, imesema kuwa wataalamu wa JKCI watashirikiana na wataalamu wa hospitali ya hiyo kuhudumia wananchi.
Amesema upimaji huo utafanyika kwa watoto na watu wazima kuanzia leo Oktoba 13 hadi Novemba 4, 2022 kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa 10 jioni katika viwanja vya hospitali hiyo.
“Tutakuwa na wataalamu wa lishe, ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na kufuata mtindo bora wa maisha, utakaowasaidia kuepuka magonjwa ya moyo,”ameeleza Nkinda.
Amebainisha kuwa watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kwenda kutibiwa JKCI.
Amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao, kujua kama wana matatizo ya moyo, ili kuanza matibabu mapema kwa watakaobainika kuwa na tatizo.
“Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa namba 0655345566 na Dk Gerald Muniko na kwa namba 0765939068 Fadhila Mwambene,”amesisitiza Nkinda.
Post a Comment