Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kesho kinaanza Vikao vyake vya Uongozi ngazi ya Taifa ambavyo pamoja na mambo mengine vitafanyakazi ya kupokea mapendekezo, kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho wa wanachama walioomba uongozi ngazi ya mikoa na Taifa kwa upande wa Chama na Jumuiya.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka amesema leo katika taarifa kwamba vikao hivyo ambavyo vyote vitafanyika Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma, ni Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (CC) ya CCM, amacho kitafanyika kesho Oktoba 28, 2022.
Shaka amesema baada ya kikao cha Kamati Kuu, keshokutwa Oktoba 29, 2022 kitafanyika Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, na kuongeza kuwa vikao hivyo vimetanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kilichofanyika kwa siku mbili, kuanzia Oktoba 24, 2022 Jijini Dodoma.
Hatua hiyo ni mchakato unaoendelea wa Uchaguzi ndani ya Chama ambapo Uchaguzi umeshafanyika kuanzia ngazi za matawi, Kata hadi ngazi za Wilaya na viongozi wa ngazi hizo wa Chama na Jumuiya wameshapatikana.
Post a Comment