Na mwandishi Maalum, Geita
Waziri wa madini amewataka wananchi na wakazi wa Geita kujenga tabia ya kujitolea kuchangia Damu ili kusaidia Majerui wa ajali mbali mbali.
Waziri aliyasema hayo wakati akikagua maonyesho ya madini na kutembelea katika banda la kampuni ya GF Trucks & Equipment’s ndani ya Maonyesho hayo na kukuta zoezi la uchangiaji Damu wa hiari lilkiendelea chini ya Kitengo cha Damu salama kwa kushirikiana na kampuni ya GF Trucks & Equipments Ltd
Kampuni hiyo iliweza kuhamasisha wadau mabali mbali wakiwemo madereva Boda boda na Bajaji katika mkoa wa Geita na kuweza kushiriki uchangiaji Damu kwa hiari na jumla ya chupa 25 za damu ziliweza kupatikana katika zoezi hili.
Nae Dereva Bajaji, Martini Malima alisema alikua anaogopa kutoa damu kwa kuhofia usalama wake lakini baada ya watu wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s kumhamasisha ameweza kuchangia damu ambayo itawasaidia watu waopata ajali lakini wakikosa ndugu wa kuwasaidia basi damu hii itatumiaka kuokoa maisha yao
Kwa upande wake Meneja Masoko na mawasilioano wa kampuni ya GF , Smart Deusi alisema kampuni hiyo imeweza kuratibu zoezi hilo kutokana na wao kuwa wauzaji wa magari na mitambo na kwa kuziongatia ajali nyingi zinazotokea barabarani tukaamua kuwashawiwhi watu wa bodabooda na bajaji kushiriki zoezi hili.
GF Tumeamua kufanya hivi ikiwa ni sehemu ya kurejesha kwa jamii faida tunayoipata ikiwamo kuisaidia serikali katika kunusuru wahanga wa ajali kwa kuchangisha Damu na tunashukuru tumefanikiwa kupata chupa 25
Hii ni mara ya tatu tunaratibu zoezi la uchangiaji damu na pia kwa kanda ya ziwa tumekuwa wadhamini wa mpira kwa timu ya Mbao hapo awali na sasa ni sahemu ya wadhamini wa Timu ya Geita inayoshiriki Ligi kuu.
Pia kampuni hiyo imeshiriki maonyesho ya madini ikiwa na lengo la kuwasogezea bidhaa wadau wa sekta ya madini ikiwamo Tipper aina ya FAW pamoja na mitambo ya kichimbia madini ya XCMG ambavyo vinapatikana katika banda la kampuni hiyo Pia kuna offa kwa wateja wa mwazo wazawa ambao watanunua mashine pamoja na magari katika kindi hiki cha maonyesho
Waziri wa Madini, Dotto Biteko akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd wakati wa maonyesho ya Madini yanayoendelea mkoani Geita.
Waziri wa Madin, Dotto Biteko akipata maelekezo kutoka kwa Afisa mauzo wa Kampuni ya GF Trucks &Equipments Ltd, Poul Msuku wakati alipotembelea banda lao kwenye Maonyesho ya Madini mkoani Geita. Kijana akichangia damu Maofisa wa Dam salama wakihifadhi chupa za damu. (Picha zote na Said Khamis)



Post a Comment