Featured

    Featured Posts

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAUGUZI SACCOS (LTD) AFUNGUA MKUTANO MKUU WA 8 WA MWAKA 2022 JIJINI DAR ES SALAAM.

 

  Mwenyekiti Bodi ya Wauguzi Saccos LTD. Christine Hhayuma akifungua Mkutano Mkuu wa 8 wa Mwaka 2022 ulio fanyika Ukumbi wa Ngome Saccos Jijini Dar es Salaam leo 26, 2022. Ambapo alianza kwa kumshukuru Mungu na kuwashukuru wajumbe na Viongozi wote kwa kuwakaribisha wanachama na viongozi kwa kuendelea kujitokeza kwa wangi na aliweza kuwapongeza kwa kujuhudi ya viongozi kufika katika baadhi ya vituo mbalimba na kuvuna wanachama wapya 90.


Hayo aliysema, wakati alipokuwa akifungua Mkutano huo na alisema, Huduma za chama kama mnavyofaham Biashara kubwa katika chama chetu ni Biashara ya huduma za kifedha inayoendana na ukusanyaji wa hakiba, hisa, utoaji mikopo kwa madhumuni ya kuwajengea uwezo kiuchumi katika kukabilana na changamoto mbalimbali za kimaisha ya kila siku 

 
Tumeendelea kutoa mikopo ya maendeleo,  dharura, kopa leo na jiunge leo kwa maendeo ya wanachama wetu ili kuendana na kutatua mahitaji yao ya kifedha na tumeendelea kutoa riba ndogo kwa mikopo ya dharura, maendeo kuendana na Sheria, Masharti na kanuni bora za utoaji mikopo.


Tumewafikia wanachama wengi zaidi kwani uongozi umewezakufikisha  Elimu ya Uuguzi Saccos LTD kwa kutembelea baadhi ya vituo vya Afya mbalimbali kupitia Mkutano Mkuu ulio fanyika Mkoani Dododoma ambapo tumefanikiwa kuvuna wanachama 90 na utekelezaji wa malengo ya mafanikio yaliopatikana mwaka 2022.


Chama kimekuwa kikichukua hatua mbalimbali za kukuwa kiuchumi kwa kuongeza mtaji kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufikisha Elimu kwa wauguzi wengi ili waweze kujiunga kwa wingi na  Saccos ikiwemo kushiriki semina mbalimbali zinazo husu wauguzi na kuendesha chama kidemokrasia, kufata Sheria kanuni na misingi ya chama na kanuni zilizowekwa ili kulinda pesa za wanachama wanazo weka kwenye mfuko wa chama kama akiba.


Katika kutimiza madhumuni ya uanzishwaji wa chama cha akiba na mikopo kama ilivyo ainishwa katika mashrti ya chama kwa kipindi kuanzia Octoba 21 hadi Octoba 22 chama kimetoa mikopo milioni mia Tisa themanini na nane lakisita na themanini na tano ongezeko la shilingi milioni  mia tatu arubaini mia tisa lakimoja sabini na tano sawa na asilimia hamsini na nne.


kimeendelea kuchukuwa hatua mbalimbali ya kutoa katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha ya kila siku na tumeendelea kutowa mikopo ya Maendeleo kwa wenye kutimiza vigezo pesa zipo za kutosha karibuni sana na mwisho nawaomba mjitokeze kwa wingi kupata mikopo.

 Afisa Ushirika Kinondoni Zahara Mohamed akiwapongeza wanacha hasa aliomba kujitokeza kununua tisheti ili tupendeze kwa pamoja naomba nishauri Mkutano ujao tufanene pia niwapongeze kwa kukamilisha akidi nakulingana na muda naomba tumchague mwenyekiti wa muda atuendeshee mkutano wetu  kati ya watu wawili alifanikiwa kupita kwa ushindi wa kimbunga ni ndugu Oswin Mbungu.

  Mkuu wa Idara ya Uuguzi, Mazingira na Ubora Saccos LTD ya Wauguzi, Mwenyekiti wa Kamati ya Mikopo na MC wa Mkutano huo. Clauda Stephano akizungumza jambo wakati wa mkutano huo.
Muuguzi Msajiliwa Hospitali ya Huberty Kairuki. Anna Mukaya (aliye simama) akizungumzia safari yake aliyoianza katika upatikanaji wa mkopo na njia aliyopitia huku akisema kwa hisia kali lihali ni mjane.
WanaChama wakijisajili
WanaChama wakijisajili na kuendelea kununua flana.
Meneja Wauguzi Saccos LTD. Michael Tarimo akiwagawia makablasha Wanachama wakati wa Mkutano Mkuu wa 8 wa Mwaka 2022 ulio fanyika Ukumbi wa Ngome Saccos Jijini Dar es Salaam leo 26, 2022.
Wanachama wakionekana wakinyoosha mikono wakati wa zoezi la kumchagua Mwenyekiti wa muda wakuongoza Mkutano huo uliofanyikaWauguzi Saccos LTD 


Afisa Muuguzi Msaidizi Mwandamizi Seif Nyamungumi (katikati) akiwa na baadhi ya wajumbe wakifuatilia Mkutano Mkuu wa 8 wa Mwaka 2022 wa Wauguzi Saccos LTD wakati Mwenyekiti wa Chama hicho alipokuwa akifungua mkutano huo.



Mwenyekiti wa Muda. Oswin Mbungu akiwashukuru Wanachama kwa kumchagua kwa kura za kimbunga 

Picha ya pamoja Viongozi na Wanacha
Picha ya pamoja Viongozi na Wanacha
Picha ya pamoja ya Viongozi
  Makamu Mwenyekiti Wauguzi Saccos. Robert Mallya akisoma muhtasari wa chama hicho wakati wa Mkutano Mkuu wa 8 wa Mwaka 2022, uliofanyika Ukumbi wa Ngome Saccos Jijini Dar es Salaam leo 26, 2022. 

Pia na kuwasomea wanachama Mkutano uliopita ambao ulifanyika mwezi wa kumi Mkoani Dodoma ulio funguliwa na mgeni rasmi kiongozi wetu. Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya Bi. Ziada Sellah
Wanacha wakifuatilia kwa utulivu kumsikia Mwenyekiti wao alipokuwa akufungua Mkutano Mkuu wa 8 wa Mwaka 2022 wa Wauguzi Saccos LTD. 




Meneja Wauguzi Saccos LTD. Michael Tarimo akisoma ripoti ya Chama wakati wa Mkutano Mkuu wa 8 wa Mwaka 2022 ulio fanyika Ukumbi wa Ngome Saccos Jijini Dar es Salaam leo 26, 2022.
Afisa Msaidizi Mwandamizi Mkuu. Anthony Malulu akishauri wakati wa Mkutano Mkuu wa 8 wa Mwaka 2022 ulio fanyika Ukumbi wa Ngome Saccos Jijini Dar es Salaam leo 26, 2022 jinsi viongozi wa Wauguzi Saccos LTD wanavyo weza kuendelea kuwasiliana na watu wa Benki.  
Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Dar es Salaam. Abdillahi Mutabazi (wa pili kushoto),  
Mkutano Mkuu wa 8 wa Mwaka 2022 wa Wauguzi Saccos ulifungwa kwa maombi na Afisa Muuguzi Msaidizi Singida RRH Grace Mpilimi. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).
 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana