Neema Peter Majule
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, anayemaliza muda wake, Neema Peter Majule ametaja sababu zilizomfanya ahamasike kugombea tena wadhifa huo kuwa ni mafanikio makubwa waliyoyapata katika kipindi cha uongozi wake. "Wanawake Viongozi UWT Dodoma ninatoa shukrani nyingi jinsi mlivyoniamini kwa miaka 5 kuwaongoza nikuwa Mwenyekiti wenu wa Mkoa. mmeniwezesha kujenga shule ya UWT Nursery school. Block 2 za maduka 11 na phamarcy 1 na Nyumba ya Katibu UWT Mkoa na kununua Gari la UWT Mkoa Ninawaombea kwa Mungu mnipe kibali tena tushirikiane tujenge kila Wilaya nyumba ya Katibu na mradi kila Wilaya kwa miaka 5 mingine tujenge mradi kila Kata. Wanawake wa Dodoma mjikwamue kiuchumi na kisiasa. Mimi Mwenyekiti wako wa mkoa Neema Majule." Nipe nafasi.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Majule akielezea mafanikio waliyoyapata kipindi cha uongozi wake na kuomba achaguliwe tena wazidi kupeleka miradi ngazi ya wilaya na kata...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 0754264203
Post a Comment