Featured

    Featured Posts

UGENI MZITO KUTOKA NJOMBE ULIVYONOGESHA IBADA YA KANISA HALISI, JIJINI DAR ES SALAAM, JUMAPILI YA NOV. 20, 2022

Baba Halisi akiendesha Ibada iliyofanyika Jumapili iliyopita ya Novemba 20, 2022 kwenye Kao Kuu la Kanisa Halisi la Mungu Baba, Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, ibada hiyo ambayo ujumbe wake mkuu kutoka kwa Baba Halisi ulikuwa 'Tumbo la kupokea utajiri' ilihudhuriwa na Watekeleza Sauti kutoka vituo vyote vya Kanisa Halisi vya ndani na nje ya Tanzania pamoja na viongozi na Wazee zaidi ya 20 kutoka mkoani Njombe.
"Ukitaka mambo yako ya kazini, biashara au uzalishaji wako wowote uende vizuri, hakikisha kila siku unaamka mapema saa 11 alfajiri, halafu unaenda utajirishoni (Kanisani) kumuomba Chanzo Halisi (Mungu Baba), na ukishatoka utajirishoni usiende kulala, toka uende kufanya uzalishaji, ukienda kulala utaibiwa", akasema Baba Halisi, halafu alipoongeza neno 'utaibiwa' akacheka kidogo.
Baadhi ya Viongozi wastaafu na ambao bado wanahudumu, wakiwa na Wezao kutoka mkoani Njombe kwenye Ibada hiyo huku wakionekana kumsikiliza kwa makini Baba Halisi. Walioketi mbele ni Daktari Martin Mkalawa na Watekeleza Sauti na Uzao na wageni wakimsikiliza kwa utulivu Baba Halisi.
Baba Halisi akimnywesha Damu safi nyeupe (Maji) Mtekeleza Sauti Faida Ujenzi Halisi, wakati akiendelea wakati akiendelea kutoa somo hilo la 'Tumbo la kupokea Utajiri', Baba Halisi alimfanyia tukio hilo kwa sababu agano lake (ndoa) ilifanyika siku ya Ibada ya Shamba la Utajiri ni Alfajiri na sasa ana watoto wawili.
Kisha akam-mwangia kichwani kumbariki katika kupokea uponyaji.
Kisha Baba Halisi akaendelea na somo, akasema "Nakuhakikishia ukifanya hivi (kuamka mapema na kwenda Kanisani) kila siku utaona mambo yako yanayooka tu, lakini ukichelewa kuamka ukapiga usingizi tuuu hadi kunakucha, kila utakakoenda unakuta mavumbi tu! Kisha akasema, Sasa simameni halafu upigwe wimbo mmoja wa kupokea sauti. Kikundi cha muziki wa kumuinua Chanzo Halisi wakipiga wimbo maalum wa kupokea sauti kama walivyoelekezwa na Baba Halisi. Mwanamuziki wa Bendi hiyo akiliungumsha gita kukoleza wimbo huo. Mwamuziki nguli King Maluu, akikoleza wimbo huo kwa 'domo la bata'. Ikawa siyo kuimba tu bali na kusakata wimbo huo.
Watekeleza Sauti na Uzao wakiwa wamesimama wakati wimbo wa kupokea sauti ukiimbwa
Watekeleza Sauti na Uzao wakiwa wamesimama wakati wimbo wa kupokea sauti ukiimbwa.
Uzao wakiwa wamesimama wakati wimbo wa kupokea sauti ukiimbwa
Wageni kutoka mkoani Njombe wakiwa wamesimama wakati wimbo wa kupokea sauti ukiimbwa

Watekeleza Sauti na Uzao wakiwa wamesimama wakati wimbo wa kupokea sauti ukiimbwa.

Kisha Baba Halisi akaongoza shukrani ya kupokea 'Tumbo la kupokea utajiri'.

Mama Halisi akipokea Shukurani hiyo. 

Kisha Baba Halisi akamuita mbele 'kumpaka mafuta' Dk. Ndosa ili kwenda kuwa Mtekeleza Sauti wa Kituo cha Kanisa Halisi nchini Rwanda. kabla ya hapo alikuwa Zambia. 👇


============ 

Kisha Baba Halisi akaketi kifamilia kuwapokea rasmi Wazee, viongozi wastaafu na ambao bado wanahudumu pamoja na ujumbe wote wa ugeni kutoka mkoani Njombe ambao walihudhuria Ibada hiyo.👇

"Sasa nimekaa kifamilia kuwakaribisha hawa ndugu zetu kutoka Njombe, haya, Mtekeleza Sauti kutoka Njombe njoo hapa utueleze japo kwa ufupi hawa ndugu zetu waliwezaje kuwapata hadi wakasafiri na wewe kutoka mbali kuja hapa", akasema Baba Halisi.
Mtekeleza Sauti kutoka Njombe akieleza alivyoweza kuwapata wageni hao.
Mtendaji wa mtaa wa Mjimwema Njombe Mjini Issack Mwakyusa na Mwenyekiti wa Mtaa huo Lenard Mkupi (kulia) wakifuatilia kwa makini wakati Baba Halisi akiendesha Ibada hiyo.
Mtendaji wa Mjimwema Lenard Mkupi akizungumza kidogo kisha akamkaribisha Mwenyekiti wa mtaa huo Issack Mwakyusa kusalimia.
Mtendaji wa Mjimwema Njombe Mjini Issack Mwakyusa akaizungumza kwenye Ibada hiyo, baada ya kutambulishwa na Mwenyekiti wa Mtaa huo wa Mjimwema Lenard Mkupi (kushoto).
Mzee mwingine kutoka Njombe naye pia akapata nafasi ya kusalimia, akasema, "Baba Halisi unaona leo tumekuja basi moja, siku nyingine tutakuja mabasi matano", usemi huo ukaamsha shangwe kwenye ibada hiyo.
Watekeleza sauti na Uzao wakasimama kumishangilia.
Dk. Martin Mkalawa kutoka Njombe akizungumza kwenye Ibada hiyo.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Tawi la Mjimwema Njombe  akizungumza katika Ibada hiyo.
Mkazi wa Mjimwema Njombe mjini Erica Anna Mkilasi akizungumza katika Ibada hiyo.
"Baba Halisi, kwa hakika unafanya jambo kubwa sana nakuombe kila la heri, ila pia naomba nipige magoti kumuomba Mama Halisi azidi kukutunza zaidi ili tuweze kuwa tunapata mafundisho yako haya ambayo kwa kweli ni na wenzangu tuliokuja kutoka Njombe tumeyakubali", akasema Mama huyu huku akipiga magoti.
Baba na Mama Halisi wakaipokea heshima ile na kwenda kumuinua huyu mama.
Mama huyu akiendelea kumshukuru Mama Halisi.
Kisha akamaliza kwa kumkumbatia.
Kisha akamkumbatia pia Msaidizi wa Mama Halisi.
Kisha wajumbe ambao hawakupata fursa ya kwenda kuzungumza wakasimamishwa na kupunga mikono.
"Mimi nina umri wa miaka 70 lakini chini ya Kanisa Halisi la Mungu Baba najisikia kijana, nina nguvu za kutosha kabisa" akasema mzee huyu baada ya kupewa nafasi.
Kisha Baba Halisi akazungumza kuwashukuru wageni hao, halafu akawaita mbele kuwafanyia shukurani (maombi), ili kila jambo lao liende vema na kufika pia salama wakati wakirejea Njombe.
Baba Halisi akifanya Shukurani kwa ajili ya wageni hao, ili wakapate baraka tele na kurejea salama, Njombe.
Kaka Huduma akicharaza kinanda wakati ukipigwa wimbo wa kuwasindikiza wageni hao kutoka Njombe, wakati wanatoka Kanisani baada ya Ibada hiyo.
Wageni hao kutoka Njombe wakipanda basi kurejea kwao baada ya Ibada hiyo.
Wageni hao wakiwa katika basi kurejea kwao Njombe.
Baadhi ya wageni hao wakiagana na Watekeleza Sauti kutoka Kao Kuu la Kanisa Halisi waliowasindikiza hadi Mbezi. Mlangoni ni Mtekekeleza Sauti wa Njombe.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana