Featured

    Featured Posts

KIGAMBONI WANAWAKE SACCOS (KIWASA) YAZINDULIWA KWA KISHINDO, MBUNGE KISANGI AWAFUNDA WANACHAMA WA SACCOS HIYO

Na Bashir Nkoromo, Kigamboni
Wanawake wanachama wa Kigamboni/Wanawake Saccos (KIWASA), wameaswa kuhakikisha hawakopeshani fedha kwa vigezo vya ushoga (urafiki), badala yake wakopeshane kwa kufuata sheria na kanuni za fedha na kuonywa kuwa wasipofanya hivyo Saccos yao itaingia kuzimu.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalum kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mariamu Kisangi wakati wa uzinduzi wa Saccos hiyo uliofanyika sanjari na Mkutano Mkuu wa kwanza wa Sacoos hiyo,  jana, Katika Ukumbi wa Nevy, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

"Katika Jitihada tulizowahi kufanya ili kuwakomboa wanawake kiuchumi zilianzishwa Saccos katika Wilaya mbalimbali hapa Dar es Salaam, lakini wanachama wakafanya makosa ikiwemo kukopeshana fedha kwa kushoga badala ya kuzingatia sheria na kanuni za fedha, sasa kama pale Temeke imekufa na wanachama wamebaki kuhangaika wakidai fedha zao", akasema Mbunge Kisangi.

Alisema, yeye kwa nafasi yake anatoa ushirikiano wa karibu na Saccos hiyo, lakini akaiomba Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kuwa karibu zaidi na Saccos hiyo, kwa kuhakikisha pale fedha za mikopo ya Kina mama zinapotoka nayo haiachi nyuma.

Mapema Katibu wa Saccos hiyo Emerician Kimario, alisema katika risala kwamba Saccos yao ilianzishwa mwaka 2019 kwa hamasa ya Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake na kwamba hadi sasa wapo wanachama 34 na wana akiba ya zaidi ya sh. milioni moja ambazo zipo Benki.

Alisema, pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo ikiwemo ukosefu wa ofisi, lakini changamoto hizo watakabiliana nazo, na kuhakikisha kuwa zinakwisha au kupungua, huku wakilenga kuongeza wanachama wapya kwa kuingiza asilimia 80 ya Wanawake wa Kigamboni.

Afisa Ushirika Manispaa wa Kigamboni Valentin Shija (kulia) akimkabidhi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mariam Kisangi Cheti cha Usajili na Leseni ya Biashara ya Kigamboni Wanawake Saccos (KIWASA) katika hafla ya uzinduzi wa Saccos iliyofanyika sanjari na Mkutano Mkuu wa kwanza wa Saccos hiyo, katika Ukumbi wa Navy, Kigamboni jijini Dar es Salaam, jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Saccos hiyo Pili Mwigamno. 

Mtiririko wa matukio kuanzia mwanzo wa hafla hiyo haya hapa👇

Bango lililokuwa likitangaza uwepo wa shughuli ya Saccos hiyo ukumbini.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mstaafu Angelina Akilimali na baadhi ya Viongozi na wanachama wa Saccos hiyo wakiandaa mambo muhimu kabla ya mgeni rasmi kuwasili ukumbini.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mstaafu Angelina Akilimali, akihamasisha wanachama na waalikwa kuingia ukumbini mgeni rasmi alipokaribia kuwasili.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mariam Kisangi akilakiwa na wanachama wa Saccos hiyo wakati akiingia ukumbini. Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mstaafu Angelina Akilimali, akimlaki Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mariam Kisangi alipowasili ukumbini.Kisha Akilimali na Viongozi na Wanachama wa Saccos hiyo wakamuongoza mgeni rasmi kwenda mahala pa kuketi..
"Pita hapa", Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mstaafu Angelina Akilimali akimwaambia Mgeni Rasmi. Kushoto ni Afisa Tarafa ya Kigamboni Selemani Mshimo ambaye alifika kwenye hafla hiyo kwa niaba ya DAS wa Manispaa ya Kigamboni.Mbunge Kisangi akiwa amewasili meza kuu pamoja na viongozi mbalimbali. Kushoto ni Afisa Ushirika Kigamboni Valentin Shija na Mratibu wa Uwezeshaji Manispaa ya Kigamboni Masesa Luanda na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Saccos hiyo Pili Mwingamno na Afisa Tarafa ya Kigamboni Selemani Mshimo ambaye alifika kwenye hafla hiyo kwa niaba ya DAS Manispaa ya Kigamboni.MNEC Mstaafu akihamasisha nderemo baada ya mgeni rasmi kuingia ukumbini.

Wanachama wa Saccos hiyo wakiwa katika chereko-chereko ya kumpokea mgeni ukumbini.

Shangwe ya kumpokea mgeni ikiwendelea, huku wapigapicha/waandishi wa habari wakiendelea kurekodi.
Kisha Makamu Mwenyekiti wa Saccos hiyo Pili Mwingamno akasimama kukaribisha mgeni rasmi.
Mjumbe wa Bodi ya Saccos hiyo Neema Nditi akitambulisha viongozi na wanachama wa Saccos hiyo kwa mgeni rasmi.
Viongozi wa Saccos hiyo wakawasili na kujipanga mbele ya meza kuu.
Halafu wanachama wote nao wakajinga na viongozi katika kujipanga mbele ya meza kuu.
Kisha Mgeni Rasmi Mbunge Mariam Kisangi na viongozi wengine wakapigwa nao picha ya kumbukumbu.
Kisha Mbunge Kisangi na Viongozi wa Kigamboni wakapigwa picha ya kumbukumbu na Viongozi waandamizi wa Saccos hiyo.
Kisaha Katibu wa Saccos hiyo Emiriciana Kimario akasoma risala.
Halafu akamkabidhi mgeni rasmi risala hiyo.
Baada ya Risala Mgeni Rasmi akasimama na kuanza kusalimia kabla ya kuzngumza, akasema, "Saccos hoyeee, Kinamama hoyeeee, Rais Dk. Samia Hoyeeeee!".
Wanachama wakaitika "Hoyeeeee"
Mbunge Kisangi akaendelea kuzungumza na viongozi na wanachama wa Saccos hiyo.

Baadhi ya viongozi na wanachama wa Saccos hiyo wakimsikiliza Mgeni Rasmi.
Baadhi ya Wanachama na Viongozi wa Saccos hiyo wakimsikiliza mgeni rasmi.
Afisa Tarafa ya Kigamboni  Selemani Mshimo akasimama kuzungumza. Mshimo alifika kwenye hafla hiyo kwa niaba ya DAS Kigamboni.
Baada ya kuzungumza Mshimo akaalikwa kupokea Wanachama wapya wa Sacoos hiyo.
Mjumbe wa NEC ya CCM Mstaafu Angelina Akilimali akawa wa kwanza kuitwa na kumsalimia Mshimo akiwa miongoni mwa wanachama wapya wa Saccos hiyo.

Baada ya wanachama wapya kufika mbele ya jukwaa, Mshimo akapigwa nao picha ya kumbukumbu.
Halafu Afisa Ushirika Manispaa wa Kigamboni Valentin Shija (kulia) akamkabidhi mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mariam Kisangi Cheti cha Usajili na Leseni ya Biashara ya Kigamboni Wanawake Saccos (KIWASA)

"Ohhh, safi Sana", Mgeni rasmi akajisemea moyoni wakati akizitazama vyeti hivyo.
Kisha akaonyesha vyeti hivyo vionwe na kila mtu aliyekuwa katika hafla hiyo.
Halafu ikawa heka heka kufuarahia tukio hilo.
Mgeni rasmi akashuka kutoka jukwaani na kuzungumza maneno ya nyongeza na viongozi na wanachama wa Saccos hiyo.
Shamrashamra zikaendelea.

Kisha Mgeni rasmi Mbunge Mariam Kisangi akawa tayari kupanda gari lake ili kuongoka eneo la tukio mwishoni wa hafla hiyo. Kushoto ni baadhi ya Viongozi na Wanachama wa Saccos hiyo wakiagana naye.

©Dec. 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana