Featured

    Featured Posts

TUNA RAIS NA MWENYEKITI WA CCM MUUMINI WA USAWA WA KIJINSIA; UWT TUNAJIVUNIA!!!

 

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI. 

Awali ya yote nichukue baraza hii kumpongeza Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuchaguliwa tena kwa ushindi mnono wa kura 1,914 katika ya 1,915 kuwa Mwenyekiti wa Chama chetu kwa kipindi cha mwaka 2022/2027.

Aidha pia nimpongeze Dkt Hussein Ali Mwinyi kushinda Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar, Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara ndugu Abdulrahman Omary Kinana pamoja na Wajumbe wote 20 Bara na 20 Zanzibar wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa waliochaguliwa Jana Desemba 07, 2022. Hongereni sana. 

Hakika Uchaguzi huu, Chama chetu Cha Mapinduzi kimeonesha ukomavu mkubwa wa Demokrasia duniani kwani ulikuwa Uchaguzi wa Haki, Huru na uwazi unaofaa kuigwa na Vyama vingine vyote vya siasa ndani na nje ya mipaka ya Nchi yetu. 

Kipekee katika Uchaguzi huu, UWT tumekoshwa sana na uamuzi wa Chama chetu chini ya Uongozi wa Mwenyekiti Dkt Samia, kwa mara ya kwanza kutenga 30% ya nafasi za Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kuwa nafasi za wanawake. Haya ni Mapinduzi makubwa mno katika agenda ya usawa wa kijinsia katika Uongozi kama inavyosisitizwa na Ilani yetu ya Chama 2020/2025, Katiba yetu ya Chama na Katiba ya Nchi, Haki za Binadamu, pamoja na Maridhiano mbalimbali ya Kikanda na Kimataifa ya usawa wa kijinsia ambayo Nchi yetu tumeingia. 

Mheshimiwa Rais Dkt Samia amekuwa mdau mkubwa wa usawa wa kijinsia katika uongozi wake na siasa tangu mwaka 1995 aliposhiriki mkutano wa siasa. Tunampongeza sana na tunajivunia kuwa na Rais mwanamke wa kwanza tangu tupate Uhuru mwaka 1961 ambaye hamumunyi maneno lipokuja suala la usawa wa kijinsia. Vitendo vyake vinazungumza kwa sauti kubwa. Hongera sana Mwenyekiti wetu Dkt Samia. 

UWT inapenda kuwapongeza wanawake wote 12 walioshinda katika nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kati ya Wanawake 80 walioteuliwa kugombea nafasi hiyo katika Uchaguzi huu wa mwaka 2022. Wanawake wote ambao kura hazikutosha, tunawaomba wasife moyo, kuna kushinda siku nyingine, Uchaguzi umeisha sote tuwe wamoja, tuvunje makundi, tujenge Chama chetu na tuimarishe UWT yetu.


Katika kuzingatia suala hili la usawa wa kijinsia, tunaamini huu ni mwanzo mzuri wa Chama chetu cha Mapinduzi CCM katika kupanua Demokrasia na hivyo tunaamini kuwa kuanzia sasa chaguzi zote ndani na nje ya chama kwa ngazi zote zitazingatia kutenga % ya nafasi kwa ajili ya wanawake ikiwemo chaguzi zijazo za Serikali za Mitaa 2024,  Uchaguzi Mkuu 2025, Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi wa mwaka 2027 na chaguzi zinginezo. 

UWT tunamhakikishia Mwenyekiti na Rais wetu Dkt Samia kwamba UWT imeichukua agenda ya Usawa wa Kijinsia katika Siasa na Uongozi kama agenda mahususi katika agenda za Jumuiya ya UWT ili kuhakikisha wanawake wote katika nyanja zote; siasa, uchumi, kijamii na kitamaduni wanashirikishwa vilivyo na kupewa fursa kuingia katika vyombo vya maamuzi. 

KAZI IENDELEE!! #JeshiLaMama

Mary Pius Chatanda, 
Mwenyekiti wa UWT Taifa, 
Desemba 08, 2022.


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana