Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Lumumba Hamis Kawambwa, Ziada Majipwani (Mwenyekiti wa CCM tawi la Kidimu), Katibu Mwenezi wa CCM Tawi la Lumumba (Sanai Daud Harrison), na Fred Atirio Mbwilo (Katibu wa CCM Tawi la Lumumba).
WENYEVITI wa Chama cha Mapinduzi katika matawi ya Lumumba, Mkombozi na Kidimu wamefanya kikao chao kufuatualia taarifa ya nyumba zaidi ya 2140 katika mitaa hiyo kutakiwa kuvunjwa.
Kulingana na mwenyekiti wa kikao hicho, Ziada Majipwani wananchi katika mitaa ya Kidimu na Lumumba kwenye kitalu namba 34 chenye zaidi ya nyumba 2140 wameandikiwa notisi ya kutakiwa kuvunja nyumba zao.
"Notisi imeandikwa tarehe 22 Novemba ya kuwataka watu wote kuvunja nyumba zao ndani ya siku saba" anasisitiza Hamisi Kawambwa, katibu wa kikao hicho.
Kawambwa ambaye ni mwenyekiti wa CCM Tawi la Lumumba, anasema wenyeviti kwa ujumla wanaiangukia Serikali kuangalia namna ya kulimaliza tatizo hilo vizuri kwani hadi sasa limeleta taharuki.
Licha ya kupewa notisi lakini hakuna maelezo ya wapi wananchi hawa wanatakiwa kuhamia baada ya nyumba zao kubomoa.
Post a Comment