Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP), Slyvester Mwakitalu akielezea mbele ya vyombo vya habari jinsi walivyopunguza kwa kiasi kikubwa ucheleweshwaji wa kesi mahakamani, alipotembelea Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria kwenye viunga vya Nyerere Square jijini Dodoma Januari 25, 2023.
Afisa Usajili wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Gabiriel Girangay akitoa maelezo kuhusu kazi za wakala hiyo.
Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali, Slyvester Mwakitalu akimkabidhi hati ya usajili wa kampuni mmoja wa wakazi wa Dodoma katika Banda la Brela.
DPP akiwa banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). anayetoa maelezo ni Rose Chilongozi Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Sheria wa Tume.
DPP Mwakitalu akiwa Banda la Jeshi la Polisi akipata maelezo kuhusu utendaji wa jeshi hilo kutoka kwa ASP Michael Mtebene. Kutoka kulia ni Mkaguzi wa jeshi hilo, Christer Kayombo na Dkt Amina Mtika.
Kayombo wa jeshi hilo akifafanua jambo mbele ya DPP Mwakitalu.
DPP Mwakitalu akitembelea maonesho hayo.
DPP Mwakitalu kipatiwa zawadi katika Banda la Ofisi ya Taifa ya Mashitaka baada ya kumaliza kutembelea maonesho hayo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, DPP Mwakitalu pamoja na mambo mengine akielezea wanavyojitahidi kupunguza ucheleweshwaji wa mashauri mbalimbali...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDAMHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
Post a Comment