Featured

    Featured Posts

SHANGWE, NDEREMO VYATAWALA MAPOKEZI YA MNEC MLAO MISENYI

 


Na Lydia Lugakila  Misenyi.


Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa  Cde Ramadhani Mwishehe Mlao (MNEC) ametikisa kwa kishindo kikubwa kuelekea maadhimisho ya miaka 46 ya CCM katika wilaya ya Misenyi mkoani Kagera.


Katika ziara hiyo ya kuelekea maadhimisho ya miaka 46 ya CCM MNEC Mlao ameungana na viongozi wa Uvccm Mkoa wa Kagera na wanachama wa chama cha mapinduzi ambapo amepokelewa kwa kishindo kikubwa  alipowasili katika ofisi ya CCM Mkoa.


Aidha MNEC Mlao ametembelea mradi wa ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa, inayojengwa Ihungo Manispaa ya Bukoba na kusitisha mara moja ujenzi wa nyumba ya Mtumishi kujengwa maeneo hayo, hii ni kutokana na sababu za msingi kuwa ni mbali na Ofisi kwani zaidi ya km.7 kutoka Ofisini, Miundombinu kutokuwa rafiki na Nyumba iko pekee yake mbali na eneo yalipo makazi ya watu.


Aidha MNEC Mlao ameuagiza uongozi wa Uvccm mkoa kutafuta kiwanja haraka kilicho karibu na makazi ya watu, na Ofisi pia na katika kusisitiza hilo MNEC Mlao amechangia mchango wa ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Mkoa Tsh. 3,750,000/= kwaajili ya kununua tofali zote za nyumba hiyo.


Pia amelakiwa kwa kishindo wilayani Missenyi, na kutembelea jengo la mradi wa ujenzi wa miradi ya Chama na Jumuiya Ambapo ameweza kuchangia Bati 100 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa mradi huo na kusisitiza kuendelea kuwa nao pamoja.


MNEC Mlao pia ameweza kutembelea Mashina ya mabalozi, na kupandisha bendera na kuzindua Madarasa ya MAKADA Mkoa wa Kagera, kwa kuzungumza na Maelfu ya Vijana waliofurika katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi na kusisitiza wanachama wa chama cha mapinduzi kuendelea kuwa kinara kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan maana kazi anayoifanya ya kuhakikisha watanzania wote wanapata maendeleo kwenye kila maeneo ni kubwa sana.


Sambamba na hivyo Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kagera ukiongozwa nza mwenyekiti  Cde Falis Athuman Buruhani umempongeza sana MNEC  Mlao kwa kuwaunga mkono kwenye ujenzi wa nyumba ya katibu wa vijana wa Mkoa na mradi wa Jumuiya ya vijana wilaya ya Misenyi.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana