Na Odace Rwimo. Igunga
MBUNGE wa jimbo la Igunga Mkoani Tabora Nicholaus Ngassa amezindua awamu ya kwanza ujenzi wa Ofisi za kata ikiwa ni sehemu mojawapo ya kutekeleza ahadi zake alizotoa wakati wa uchaguzi mkuu 2020.
Akizungumza wakati wa hafla ya kusherekea miaka 46 yachama cha mapinduzi CCM pamoja na uzinduzi wa ujenzi Ofisi 16 za kata za jimbo la Igunga ambapo anatarajiia kutumia zaidi milioni 480 katika ujenzi huo.
Alisema kujenga ofisi za kata ni moja ya ahadi zake alixotoa wakati wa uchaguzi mkuu hukuakisema ni muhimu kutimiza kile ulicho kiahidi kufanya katika uongozi wake hivyo nitafanya kazi hii kwa asilimia kubwa kuhakikisha natimiza jukumu hili kubwa.
“ Wanachama wa CCM jimbo la Igunga lina Imani na mimi kwa asilimia kubwa ndio sababu katika kutimiza miaka 46 ya chama cha mapindizi nimeitumia katika kuzinduwa kazi hii kubwa ya ujenzi wa ofisi za kata”alisema Ngassa
Alisema na hili litaenda sababu na kuwepo na vibanda vitatu kwa kila ofisi hii ikiwa ni kwa ajili ya jumuiya zote yaani jumuiya ya Wazazi,Vijana na Umoja wa wanawake UWT ikiwa ni hatua ya kuimarisha uchumi wa jumuiya hizo.
Alisema jukumu kubwa alilonalo sasa ni kuhikikisha uchumi wa chama cha mapinduzi inamirika kwa matokeo chanya ya maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu mwaka 2025 pamoja na kujenga imani kwa wanachama waliokiamini chama cha mapinduzi.
Ngassa alifafanua kuwa Rais amefanya kazi kubwa kwa wananchi hivyo sasa ni jukumu la wabunge kuhakikisha kazi aliyoifanya mama kila mtanzania anaitambua kupitia kwa wawakilischi waho hao na kutambua mchango wa serikali katika uimarishaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu CCM Hassan Mwakasuvi akimlisha keki mbunge wa jimbo la Igunga Nicholaus Ngassa kama ishara ya kuzaliwa kwa CCM.Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na mjumbe wa kamati kuu ya Halmashauri kuu ya CCM Hassani Mwakasuvi alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteuwa katika nafasi hiyo kubwa hivyo atafanya kazi kw uzalendo mkubwa.
Alisema chama cha mapinduzi kina misingi imara ya kiuongozi ndio maana kimekaa madarakani kwa miaka minggi bila ya kuteteleka na atahakikisha anatimiza majukumu ya kuinadi ilani ya CCM katika kulinda na kutetea haki za watanzania.
Wanachama wa CCM Mkoa wa Tabora wakifurahia maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCm na kutimiza miaka 46 tangu kuanzishwa kwake.
Aidha katika hatua nyingine ameagiza uongozi wa hostari ya wilaya ya Igunga kufanya haraka kuweka vifaa kwenye jengo la ICU ambalo limekalimaka ili kuondoa uchakavu kabla ya kuanza kutumika.
Alisema serikali imefanya kazi kubwa katika kujenga jengo hili la ICU hofu yangu likiendelea kukaa bila ya kuwekewa vifaa vinavyohitajika litaanza kuchakaa kabla ya kutumika hivyo mnatakiwa kufanya haraka kuweka vifaa vyote muhimu na jengo lianze kazi mara moja.
Kwa upande Wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dr. Batrida Buriani amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujenga madarasa ya kutoshereza ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi 2020/2025
Alisema katika kusherekea miaka 46 inasadifu mafanikio makubwa ya CCM katika Nyanja mbalmbali za maendeleo kutokan na serikali ya awamu ya sita kutekeleza miradi kwa vitendo hasa kwa kugusa maisha ya watu moja kwa moja.
Alisema katika kutekeleza ilani ya Uchaguzi serikali imejenga miundombinu bora ya Shule,Zahanati,Vituo vya Afya Hospitari ya wilaya na Rufaa ikiwa ni pamoja na kuongeza huduma ya upatikanaji wa maji vijijini kwa asilimia zaidi ya 85 huku miundombinu ya barabara ikiendelea kuboreshwa.
Hata hivyo ameagiza kusaka watoto nyumba kwa nyumba wenye umri wa kujiandikisha kwenda shule ambao bado hawajapelekwa shuleni ikiwezekana hatua za kisheria zichukuliwe kwa wazazi ambao watashindwa kuwapeleka watoto shule.
“ Serikali inatoa elimu bure inashangaza sana kuona kuna baadhi ya wazazi wanaoshindwa kuwapeleka watoto wao shule huku hata kama hana sale anaruhusiwa kuanza masoma wakati unajipanga kumnunulia”alihoji Burian
Post a Comment