Featured

    Featured Posts

JUMUIYA YA WAFANYABIASHARA KARIAKOO YAIOMBA TRA KUWA NA TIMU MOJA YA UKAGUZI WA KODI

Na Mwandishi Maalum
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Martine Mbwana, ameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwa na timu moja ya ukaguzi wa kodi Kariakoo.

Mbwana alisema hayo, wakati wa uzinduzi wa vitambulisho vya kuwatambua wafanyabiasha wa kariakoo, Dar es Salaam, jana.

Alisema kuwekuwa na timu nyingi za ukaguzi na kusababisha usumbufu kwa wafanyabiashara pindi mizigo yao inaposhikiriwa na TRA.

"Mfanyabiashara mmoja anakaguliwa na maofisa wa TRA zaidi ya mmoja kutoka maeneo mbalimbali, ushauri wetu kama jumuiya ya wafanyabiashara kariakoo ni moja, TRA nayo iwe moja na hizo timu mnazoziweka ziwajibike katika TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo", alisema.

Alisema mzigo unaweza kukamatwa Jangwani, ukiufuatilia unaambiwa nenda TRA Kipata, huko nako utaambiwa nenda Roho ngumu utaukuta mzigo wago, hiyo ni kreo na usumbufu wanaokutanao wafanyabiashara wa Kariakoo.s

Mbwana suala la kuwa na timu nyingi za ukaguzi inaweza kusababishwa kuwepo kwa rushwa na ukosefu wa nidhamu kwa baadhi ya vijana.

Pia Mbwana alisema ikitokea mfanyabiashara mwenyekitambulisho ya jumuiya amepata shida, ameomba mamlaka zimtambue na wampe ushirikiano au huduma anayohitaji.

Naye Mwenyekiti wa Machinga Kariakoo, Stephen Lusinde, amempongeza Rais Dk. Saimia Suluhu Hassan, kwa kuwaondolea kikwazo katika suala ulipaji kodi.

Alisema kitendo cha Dk. Rais Samia kuruhusu mfanyabiashara anapoanza biashara yake, kuzungumza na TRA wampe muda wa kulipa kodi za serikali, huku akiendelea na kufanyabiashara, kitawasaidia wao kukua kibiashara na kuweza kulipa kodi za serikali kwa wakati.

"Nichukue fursa hii sisi Wamachinga Taifa na Kariakoo, kumpongeza Dk. Rais Samia, kwa kutuondolea kikwazo hicho, kwani hapo awali unafungua biashara leo na ukienda TRA unaambiwa mambo mengi, ukirudi huendi tena, alisema.

Kwa upande wa Meneja wa TRA Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Alex Katundu, vitambulisho hivyo ni muhimu katika ushirikiano wa TRA na wafanyabiashara wa Kariakoo.

Alisema hilo ni daraja zuri la kushirikiana pande zote mbili katika kutatua changamoto zilizopo baina ya TRA na wafanyabiashara.

Katundu alisema kitambulisho hicho ni utambulisho utakaosaidia endapo kutatokea changamoto baina yao ni rahisi kuwafahamu kwa kuwapata.

"Kwa changamoto ndogo tunaweza kukuacha ukaendelea na kufanya biashara na endapo tutakuhitaji ni rahisi kukupata, kupitia Jumuiya ya Wafanyabiashara Karikoo, tukajadiliana kwa kutatua hizo changamoto", alisema.

Pia Katundu alisema baadhi ya changamoto zilizowasilishwa na wafanyabiashara hao, ataziwasilishwa kunakohusika ili zifanyiwe kazi ikiwemo kukutana na viongozi wao.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), Martin Mbwana, akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa vitambulisho vya wafanyabiashara Kariakoo, Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Alex Katundu na kulia ni Mkuu wa Polisi  Wilaya ya Kariakoo, William Solla.
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kikodi Kariakoo, Alex Katundu, akizungumza akitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wafanyabiashara wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK), wakati wa uzinduzi wa vitambulisho vya jumuiya hiyo.
KATIBU Tawala wa Wilaya ya Ilala, Chalangwa Makwilo, akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Dharura ya Jumuiaya ya Wafanya Kariakoo (JWK), Hamidu Maftaha, kitambulisho cha jumuia hiyo, Dar es Salaam, jana. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa JWK, Martin Mbwana na Makamu Mwenyekiti wa jumuia hiyo, Yahaya Ally.
KATIBU Tawala wa Wilaya ya Ilala, Chalangwa Makwilo, akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Maadili ya Jumuiya ya Wafanya Kariakoo (JWK), Kusirie Mwasha, kitambulisho cha jumuia hiyo, Dar es Salaam, jana. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa JWK, Martin Mbwana na Makamu Mwenyekiti wa jumuia hiyo, Yahaya Ally
Wanachama ya Jumiya ya Wafanyabiashara Kariakoo (JWK), wakiwa katika mkutano wa uzinduzi wa vitambulisho vya jumuiya hiyo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana