Featured

    Featured Posts

KAMATI YA BUNGE YAPONGEZA MRADI WA KITUO JUMUISHI CHA TAASISI ZA KISHERIA ZA SERIKARI

Na Mwandishi  Maalum, Busweru-Mwanza
Wajumbe wa Kamati  ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wameupongeza mradi wa ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Taasisi za Kisheria za Serikali na kuuelezea kuwa ni mradi wa mfano wa kuigwa.

Wametoa pongezi hizo leo Alhamisi, Machi 16, 2023, walipoutembelea mradi huo unaojengwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, katika Kata ya Busweru Wilaya ya Ilemela hapa mkoani Mwanza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupata maelezo ya mradi huo na kisha kuutembelea, Wabunge hao wametaka mradi huo ukamilike kwa wakati kama ilivyo kwenye mpango kazi.

Zaidi ya wabunge tisa (9) wa Kamati hiyo waliuliza maswali mbalimbali kwa  Mkandarasi (SUMA-JKT) na Mshauri elekezi (TBA), mengi ya maswali hayo yaliyoambatana na pongezi na yayotaka ufafanuzi kuhusu  mradi.

Akizungumza baada ya wabunge hao kupata fursa ya kuuliza maswali, Makamu  Mwenyekiti wa Kamati hiyo  Mhe. Florent Laurenti Kyombo (Mb) alimtaka Waziri wa Katiba na Sheria  kuyafanyia kazi baadhi ya masuala yaliyoibuliwa na wabunge hao.

“Mhe. Waziri (Ndumbaro) sisi Kamati ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria tumeridhishwa na kazi inayoendelea hapa, huu ni mradi mzuri na wa viwango, tunakupongeza sana sasa ukayafanyie kazi yale  masuala madogomadogo tuliyoyaeleza hapa” akasema Makamu  Mwenyekiti wa Kamati.

Akaongeza kusema, "miradi kama hii inayosogeza huduma za kisheria karibu na wananchi ambayo ndiyo dhamira ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kisheria  bila usumbufu wowote.

Miradi  kama hii ambayo ni ya mfano inatupatia sisi wajumbe nguvu ya kwenda kuizungumzia kwenye Kamati zetu na kuziombea fedha ili iweze kuenea nchi nzima”.

Akijibu maswali na hoja za wabunge hao ikiwamo ya mapendekezo ya mkandarasi kuongezewa muda kwa kile walichosema mradi upo nyuma kwa miezi miwili,  Waziri alisema, “ Waheshimiwa wabunge  niwashukuru sana kwa kuutembelea mradi huu na kwa ushauri mlioutoa kuhusu suala la kumuongezea muda mkandarasi.

Nieleza wazi kabisa, Serikali haikusudii na wala haitamuongezea muda, mkandarasi afanye analoweza kufanya aukamilishe mradi huu kulingana na makubalianao ambapo ni mwezi Octoba  Mwaka huu.”
 
Waziri aliongeza kuwa Serikali  itaendelea kutoa ushirikiano  kwa mkandarasi na mshauri mwelekezi wakati wowote watakapokuwa wana tatizo na ikibidi  hata kubadili mfumo wa malipo.

Akatahadharisha  akisema, endepo  mkandarasi hatakamilisha mradi huo kwa wakati basi itampasa kuilipa serikali kama taratibu zinavyotaka.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Kudumu  ya Utawala,  Katiba na Sheria ilikuwa mkoani  Mwanza ambapo pamoja na  kuutembelea mradi wa Ofisi ya Mwanasheria wa Serikali  pia wametembelea  Jengo  Jumuishi la Utoaji  haki la Mahakama ya Tanzania.

Kabla kutembelea miradi hiyo walimtembelea Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe Kigoma  Malima,  ambapo walipokea taarifa ya mkoa.

Wajumbea wa Kamati hiyo ya Bunge  kabla ya kufika Mkaoni Mwanza,  walikuwa  Mkoa wa Shinyanga na Tabora.

MATUKIO KATIKA PICHA 👇

Wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bungea ya Utawala, Katiba na Sheria, wakipata maelezo kuhusu ujenzi wa jengo la Kituo Jumuishi cha Taasisi za Kisheria za Serikali kinachojengwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  katika eneo la Busweru wilayani Ilemela mkoani Mwanza, leo.
Wajumbe wa  Kamati ya Kudumu ya Bungea ya Utawala, Katiba na Sheria walipokuwa wakienda kukagua jengo la Kituo hicho Jumuishi cha Taasisi za Kisheria za Serikali kinachojengwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali  katika eneo la Busweru wilayani Ilemela mkoani Mwanza, leo..
Kampteni Sila kutoka Suma JKT akitoa maelezo ya utekeleza wa mradi huo kama mkandasari na kuahidi kwamba wataongeza juhudi  kuhakikisha mradi huo unakamilika ifikapo  Octoba 23 2023.
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Utawala, Katiba na Sheria  akiuliza swali kuhusu mradi wa Kituo Jumuishi cha Taasisi za Sheria za Serikali  jumla ya Wabunge  tisa (9) waliuliza maswali mbalimbli mbali.

Taarifa hii, Imeandaliwa na kutumwa kwetu na Kitengo cha Mawasiliano.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana