Featured

    Featured Posts

MAMIA YA WAUMINI KANISA HALISI WANOLEWA KUBOBEA KATIKA UJASIRIAMALI, BABA HALISI AWATAKA KESHO KUHUDHURIA KWA WINGI ZAIDI

Na Bashir Nkoromo, Tegeta
Wakati Uzao (waumini) zaidi ya 1000 wa Kanisa Halisi la Mungu Baba tangu Machi 22, 2023 wamekuwa wakinolewa na wataalamu ili kubobea katika Ujasiriamali na utengenezaji bidhaa mbalimbali za fani hiyo, Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo Baba Halisi leo amewataka kesho kuhudhuria kwa wingi zaidi kwenye mafunzo hayo.

Amewataka wahudhurie kwa wingi zaidi baada ya Mwalimu mbobevu kutoka Chuo cha Elimu kwa wote cha Mbagala Saravai Rashid, anayeendesha mafubzo hayo kueleza kwamba kesho ndiyo yeye na jopo lake watatoa mafunzo kwa vitendo.

Katika kuweka msisitizo Baba Halisi aliwaita mbele yake watekeleza sauti (viongozi wa Vituo vya Kanisa Halisi) kusogea mbele yake, na baada ya kufanya hivyo akawapa maelekezo maalum ya kila mmoja wao kuhakikisha kila uzao katika kituo chake anafika kesho kuhudhuria mafunzo hayo.

"wenyewe mmeona mnavyopata mafunzo haya kwa ubora unaotakiwa, sasa mafunzo haya mnatakiwa wote myapate ili mpokee kwa vitendo somo ambalo nimekuwa nikitoa hapa Kanisani kwamba Ibada ni Uzalishaji kama Muumba wa yote na vyote anavyoelekeza, basi kesho nataka mfike kwa wingi zaidi na ninyi watekeleza sauti simamieni vya kutosha kujumu hili", akasema Baba Halisi.

Katika masomo hayo, Mwalimu Rashid na jpo lake wamkuwa wakifundisha namna bora ya kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo sabuni za usafi wa vyoo, wa majumbani na utengenezaji wa batiki na mazulia madogo na makubwa.

Akiahirisha mafunzo ya leo Mwalimu Raishidi alimpongeza Baba Halisi kwa kundisha kwamba Ibada ni uzalishaji. akasema, " Baba Halisi nakushukuru na kukupongeza sana, kwa mafindisho yako kwa ndugu zangu hawa kwamba Ibada ni Uzalishaji, hakika upo sahihi mno, hebu mpigieni makofi".

"Nawambieni haya mafunzo mkiyashika na kuyafanyia kazi hasa ninyi vijana, mtakuwa mtatoka kifedha, maana pamoja na mafunzo haya lakini pia hapa Kanisa Halisi mpo mahali sahihi tena katika mikono salama, hivyo komaeni msirudi nyuma", akasema Mwalimu Rashid

Baada ya Mwalimu Rashidi kuahirisha mafunzo ya leo, Baba Halisi aliendelea kuendesha Ibada mbayo somo lilikuwa kupokea faili la uheri wa mambo yote mema.

Mwalimu mbobevu kutoka Chuo cha Elimu kwa wote cha Mbagala Saravai Rashid, akifafanua jambo wakati akitoa elimu ya ujasiriamali tangu namna ya kutengeneza bidhaa na kuzitafutia soko, alipopewa nafasi hiyo na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi wakati wa Ibada iliyofanyika leo Makao Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga, Dar es Salaam. Zaidi ya Waumini 100 wamehudhuria mafunzo hayo yaliyoanza siku tano zilizopita na yanaendeleo kesho.
Mwalimu mbobevu kutoka Chuo cha Elimu kwa wote cha Mbagala Saravai Rashid, akionyesha moja na hitaji la kuchanyanyia na mahitaji mengine wakati wa kutengeneza sabuni ya maji,
Mwalimu Charles Mbaga akionyesha namna ya uchanganyaji wa mahitaji katika kutengeneza sabuni.
Mwalimu Saravai Rashid, akionyesha vitabu alivyotunga vyenye maarifa ya utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za ujasiriamali ikiwemo sabuni za maji.
Mwalimu Charles Mbaga akielezea namna ya kutengeneza zulia kwa kutumia magunia..
Wakionyesha gunia ambalo likishashonwa inatokea zuria la thamani kubwa.
"Sasa ili uweze kuruhusiwa na serikali kutengeneza bidhaa hizi kama sabauni, kwa kuwa zinatumia kemikali kutengenezwa lazima uwe na cheti kinachothibitisha kuwa umepata mafunzo, cheti chenyewe ni kama hiki, kesho mtakapokuja kila mmoja anje na sh. 5,000 tu za kupata cheti hiki", akasema  Mwalimu Rashid wakati akiahirisha mafunzo leo.
Bada ya mafunzo kuahirishwa Baba Halisi akamshukuru Mwalimu Rashidi lakini pia akasema, "Nilipowaambia kuwa huyu Mwalimu anaitwa Rashid sikuona hata mmoja wenu aliyeshtuka maana huyu si Mkristu, Hii imenipa imani kwamba kumbe niapowaambia kuwa Wakristu na Watoto wa Ishmael ni ndugu huwa mnanielewa. Tunamshukuru sana Rashid na bila Shaka Chanzo Halisi yumo ndani yake".
Mwalimu Rashid (Wapili kushoto) akapokea shukurani za Baba Halisi.
Uzao pia wakapokea.

Kisha Baba Halisi akafanya shukurani kabla ya kuachilia kupokea faili. baada ya hapo akasema, " Sasa kabla ya kuachilia somo la kupokea faili waimbaji watupigie wimbo wa 'Uhalisi wa Kanisa ni Uzalaishaji'....ukapigwa Ikawa kuselebuka na kushangilia👇






Mwisho wa kusrebuke na kushangilia
Baba Halisi akawaita watekeleza Sauti wa Chunya na Katavi akisema, "Mkiwakumbuka hawa mtakuwa pia mnakumbuka tukio la leo".
Baba Halisi akawabariki kwa damu safi nyeupe.
Halafu akawaita watekeleza sauti wote na kuwapa maelekezo ya kuhakikisha kesho uzao wanafika kwa wingi kwenye mafunzisho ya ujasiriamali.
Mwishoni Uzao wakinunua vitabu vya ujasiriamali waliofundishwa.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana