Featured

    Featured Posts

MNEC HAMOUD: VIJANA UVCCM MSITAKE NJIA ZA MKATO, FUATENI NYAZO ZA KINA KIKWENTE, DK. NCHIMBI

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Abuu Jumaa amewataka  Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wasitake njia za mkato kufikia wanakotaka, bali waende hatua kwa hatua kama viongozi wengi waliopitia UVCCM akiwemo Rais Mstaafu Jakata Kikwete.

"Mkitaka njia za mkato hamtafika salama mnakotarajia. lazima mpite tatua kwa hatua, kama walivyofanya vongozi wetu ambao hivi sasa wapo ngazi za juu kama Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Dk. Balozi Emmanuel Nchimbi na wengine wengi, ambao ni matunda ya UVCCM", akasema M-NEC Hamoud Jumaa.

Hamoud alisema hayo, leo, akizungumza katika Kikao cha Baraza la UVCCM Wilaya ya Ilala, kilichofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, Jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na mamia ya Viongozi na wajumbe.

"Najua kila mmoja wenu anataka afike ngazi kubwa ya uongozi, ili kufikia hapo hakikisheni mnakuwa mstari wa mbele kufanyakazi za Chama wakati wowote, ukitumwa uwe mwepesi. Maana ukitumwa ndiyo unakutana hata na viongozi ambao usingweza kukutana nao , kwa hiyo kutumwa pia ni fursa.

"Mimi kuna wakati fulani nilikuwa nafanyakazi gereji, nikawa natumwa mara kachukue hiki, mara shika hiki. kweli nilikuwa nachoka, lakini sasa hivi nawashukuru waliokuwa wakinituma maana baada ya pale nikawa fundi mkubwa wa magari, lakini pia nikafahamiana na wafanyabiashara wengi na sasa ni mfanyabiashara.

Na ninyi viongozi hawa vijana lazima muwe mnawatuma bila kubagua kwamba hii ni ngumu kwa huyu na hili ni njyepesi kwa huku, watumeni wote kuwa kuzingatia kuwa wote ni Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM", akasema MNEC hamoud.

Kuhusu maadili MNEC Hamoud aliwaasa Vijana kuachana na tabia za hovyo kama ulevi, ushoga, kutumia dawa za kulevya na kuzungumza maneno yanayokiuka maadili, ikiwa wanahitaji kuja kuwa viongozi bora wa baadaye.

Aliwataka kuwa mstari wa mbele katika kukipambania Chama Cha Mapinduzi, ikiwemo kuyaeleza mambo mema makubwa yanayofanywa na serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambayo alisema, yote yanajulikana.

Pia aliwataka Vijana hao wa UVCCM kuachana na yaliyotokea wakati wa Uchaguzi uliopita kwa kuwa kuendelea kuyakumbatia na kujengeana uhasama kwa sababu ya tofauti zilizotokea wakati wa uchaguzi huo ni kukiumiza Chama.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala Juma Mizungu alisema, katika Kikao hicho cha Kikatiba, Wameazimia kumpongeza Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia kwa kutimiza miaka miwili madarakani kwa mafanikio makubwa.

"Katika kikao hiki, tumejadili mambo mbalimbali, lakini kubwa zaidi tumejadili kuhusu Mwenyekiti wetu Rais Samia namna alivyoweza kuivusha nchi ndani ya miaka miwili tu, hivyo tumeamua kwa pamoja kutoa pongezi maalum kwake", alisema,

Katika kikao hicho, MNEC Hamoud aliendesha mchango kwa ajili ya ujezi nyumba ya mtumishi wa UVCCM kama zinavyotakiwa kufanya Jumuiya zote za CCM , ambapo zzilitolewa ahadi ya zaidi ya Sh. milioni 16, Ma tofali zaidi ya 600 na bati zaidi ya 50.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Abuu Jumaa, akizungumza katika Kikao cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kilichofanyika katika Ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Salaam, leo.
Wajumbea wakimsikiliza kwa utulivu mkubwa MNEC Hamoud Jumaa.
Wajumbea wakimsikiliza kwa utulivu mkubwa MNEC Hamoud Jumaa.
Wajumbea wakimsikiliza kwa utulivu mkubwa MNEC Hamoud Jumaa.
MNEC Hamoud akikabidhi fedha za ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa UVCCM kwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala Juma Mizungu baada ya kuhutubia na kuendesha harambee wa ujenzi wa nyumba hiyo.
MNEC hamoud akionyesha chaeti cha shukurani kwa mchango wa kuiinua UVCCM Wilaya ya Ilala, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa UVCCM wilaya hiyo.
MNEC Hamoud akikabidhi cheti cha shukurani kwa mchango wa kuiinua UVCCM Wilaya ya Ilala, kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya hiyo Sabry Abdallah Sharif wakati wa Kikao hicho. Watu kadhaa pia walikabidhiwa cheti kama hicho kwa mchango huo.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala Juma Mizungu akiteta jambo na Katibu wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam Michael Msuya wakati wa Kikao hicho.

MNEC Hamoud akiwa na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ilala Juma Mizungu na baadhi ya Viongozi, alipowasili kwenye Kikao hicho kuwa Mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa UVCCM Ilala Juma Mizungu, akitambulisha baadhi ya Viongozi kwa MNEC Hamod.
MNEC Hamoud akiwa katika picha ya kumbukumbu naviongozi wa UVCCM Wilaya ya Ilala kabla ya kuingia ukumbini. Habari/Picha na Bashir Nkoromo-CCM Blog
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana