Featured

    Featured Posts

RC KINDAMBA AZITAKA HALMASHAURI TANGA KUTOA KIPAUMBELE UKUSANYAJI MAPATO, KUSIMAMIA MIRADI

Na Salma Amour, Tanga 

Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba, amewataka Viongozi na Watendaji mkoani hapa kufanya kazi kwa weledi na juhudi katika kukuza uchumi kuleta maendeleo kupitia ukusanyaji wa  mapato kwenye Halmashauri zote 11.


Akizungumza na watumishi, Wakurugenzi na Makatibu Tawala wa Wilaya kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na Rais Samia  Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa mkoa huo, RC Kindamba alisema ili maendeleo yaweze kuonekana ni lazima kuwe na viongozi bora watakaoshikilia usukani wa kuleta mabadiliko ikiwemo ukusanyaji wa mapato ambayo ndio lango kuu la  kukuza uchumi wa nchi.


Pia aliwataka kusimamia shughuli za miradi mbalimbali ya maendeleo ipasavyo kama ya Elimu, Afya na Maji ili kuwezesha Wananchi kuguswa na maendeleo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia.


" Niwaombe tu viongozi na watumishi  kusimamia vyema ukusanyaji wa mapato katika  kuimarisha mkoa wetu kuwa ni mkoa  wa maendeleo,  na imani hili suala mutaweza kulipokea na kulifanyia kazi kuanzia sasa.


Wananchi wana hamu ya kuona matokeo mazuri ya mabadiliko kwenye ngazi tofauti tofauti za kiutendaji na sio vinginevyo", alisema RC Kindamba.


Aliongeza kuwa ili kuleta mabadiliko kwa  kufikia lengo ni lazima viongozi washirikiane bega kwa bega  katika mambo muhimu ya kuuboresha mkoa huo kuwa na maendeleo.


"Mpaka kufikia sasa mikoa wa Tanga umekusanya  asilimia 56 ya mapato, ili kuweze kufikia lengo ni lazima tufanya kazi kwa bidii ili tufikishe asilimia 100", alisisitiza RC Kindamba. 


Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa huo Pili Mnyema, aliahidi kutoa ushirikiano na viongozi wengine katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo kwa kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii kama alivyoagiza Rais Samia, kuwa Tanzania ya maendeleo kwa Taifa.


" Ninaahidi mimi pamoja na watumishi wenzangu na viongozi mbalimbali ambao wako kwenye jiji letu la Tanga kuwa tunaendelea kushirikiana na kupambana kwa pamoja  kwenye mambo mbalimbali ya kutuletea mabadiliko.


Kama ambavyo Serikali yetu ilivyotuamini basi hatuna budi kuidumisha imani hiyo kwa kutenda yale yenye msingi lakini pia nikutoe hofu, kuwa mkoa wa Tanga ndio Mama wa ukusanyaji wa mapato, tutapambana vyema katika kuhakikisha kuwa Halmashauri zote zinafnya vizuri.


"Tusisubiri mpaka viongozi wa  kitaifa  kuja kutukosoa, tunatakiwa  sisi wenyewe kukaguana katika kutekeleza shughuli za kuleta maendeleo kwenye jamii yetu Ili tuwe mfano mzuri, mikoa mingine waweze kuiga  namna ya uendeshaji wa shughuli zetu", alisema RC Kindamba.


RC Kindamba pia alilitaka Jeshi la Polisi kutoa kipaumbele katika kupambana na  watu wanaokiuka sheria za nchi kwa kwa kujihusisha na vitendo vya uuzaji dawa za kulevya ambazo zinaathiri vijana wengi mkoani hapo ikiwa ndio nguvu kazi ya Taifa.


"Niwaombe Jeshi la polisi kuwa macho wakati wote na kufuatilia kwa umakini wale wote wanaouza na wanaotumia dawa za kulevya na kuwachukulia hatua za kisheria Ili kuwanusuru vijana wetu katika  mambo yasiyofaa.


Pia aliwataka Polisi kuendelea kupambana na watu wakaidi ambao wanafanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii akibainisha kuwa ulawiti, ubakaji na ushoga vimekuwa gumzo hatarishi katika jiji  la Tanga.


"Hata hivyo niwapongeze Jeshi la Polisi  kwa jitihada mnazofanya kupambana na maovu kama mkoa huu", alisema RC Kindamba.

RC Kindamba akizungumza.
RC Kindamba akisalimia watumishi.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana