Na Bashir Nkoromo, Tegeta
Wafanyabishara wa Tegeta, Jumamosi ya leo, wanatarajiwa kumfaidi Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba na Vituo vyote vya Kanisa hilo Ndani na Nje ya Tanzania Baba Halisi, atakaponena nao makuu, kuwafungulia 'Tumbo la Utajiri', huku akishiriki nao chakula cha mchana, kwenye Viwanja vya Nyuki, Dar es Salaam.
Baba Halisi anakutana nao kuanzia saa 6 hadi saa 8 mchana katika hema aliloandaa, ikiwa ni siku ya saba, ya mfululizo wa mikutano ya Ibada ya 'Wiki ya Wiki ya Ukombozi wako', iliyoanza kurindima kwenye viwanja hivyo vya Tegeta Nyuki, tangu Jumapili iliyopita.
Katika mialiko Baba Halisi amesema' "Mpendwa Mfanyabiashara, Sikushawishi kwa jambo lolote. maana unaitwa mfanyabiashara. Ukija kwenye mazungumzo haya ya kujua Majira tuishimo ni ya namna gani, ndiyo utajua kuwa unadanganywa au unaambiwa lililosahihi.
Mimi nakukaribisha kwa upendo uliopitiliza. Njii maana unastahili kuwa tajiri mkubwa uliko ulivyo sasa hivi: Amsema Baba Halisi kwenye kadi ya mwaliko".
Katika Mkutano wa Ibada hiyo jana, Baba Halisi aliwaamuru Uzao kupeleka kadi hizo za mwaliko kwa kila mfanyabiashara wa eneo la Tegeta Nyuki na Tegeta kwa Ndevu ambapo aliwapa Kadi zaidi ya 100.
"Mimi nimeishi hapa Tegeta kwa karibu miaka mitano, kwa hiyo hawa ni majirani zangu, hakikisheni wote mnawafikishia mwaliko huu, maana nawahitaji wafike hapa nile nao chakula na kuwafungulia tumbo la utajiri. Mnaona pale chakula kimeshaanza kupikwa na hema la kukutania lile pale linaandaliwa, kila kitu kesho kitakuwa motomoto", akasema Baba Halisi.
Mnara Mmoja Halisi akiwapa kadi Uzao kwa ajili ya kuwaalika Wafanyabiashara, wakati wa Mkutano wa Ibada, iliyofanyika jana, katika Viwanja vya Tegeta Nyuki, Dar es Salaam, Kulia ni Baba Halisi.
"Anzeni kuwapa kadi za mwaliko wale paleee", akaagiza Baba Halisi.
Mfanyabiashara ya Bodaboda akisoma kadi yake ya mwaliko aliyopewa. kwenye stendi ya Nyuki.
Mfanyabiashara ya Samaki na dagaa Soko la Tegeta Nyukiakisoma kadi yake ya Mwaliko.
Maandalizi ya Hema la kukutana Baba Halisi na Wafanyabiashara katika chakula cha mchana leo, yakifanyika jana kwenye Viwanja vya Tegeta Nyuki.
Post a Comment