Featured

    Featured Posts

WAZIRI AWESO AMWAKILISHA VYEMA RAIS SAMIA MKUTANO WA MAJI UMOJA WA MATAIFA


Waziri wa Maji, Jumaa Aweso akihutubia alipomwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maji.





Waziri wa Maji, Aweso akiwa na mgeni rasmi katika mkutano huo Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa GWPSA.  

Na Mwandishi Maalumu, New York

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ameishauri kuona umuhimu wa Jumuiya ya Kimataifa kukaa pamoja kusimamia ajenda ya maji kwa kuongeza uwekezaji katika sekta hiyo.


Amebainisha hayo alipokuwa akihutubia alipomwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Maji unaofanyika Umoja wa Mataifa, New York, Machi 22-24, 2023.


Katika hotuba yake amesisitiza  kusimamia agenda ya maji; thamani ya maji katika maisha na uchumi; kuongeza uwekezaji katika eneo la maji; ushirikiano wa kimataifa katika maji; pamoja na utafutaji wa fedha kwa ajili ya maji.


Aidha, Katika mkutano, Tanzania imebeba agenda mbili ambazo ni utekelezaji wa Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji Awamu ya Tatu (Water Sector Development Programe I…

"Nimeshiriki Kikao kilichoratibiwa Benki ya Dunia New YorkMarekani kinachohusu Maii na Mazingira kilichohusisha mawaziri wa maji wa Nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja Ministerial Roundtable pamoia na wadau wa maji ikiwa ni muendelezo wa vikao vya juu vya mawaziri wa Maji kwa ajili kuongeza msukumo na mabadiliko katika kufikia dhima ya watu kupata maji safi, salama na ya kutosheleza katika Ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika." Amesema Aweso.

Akizungumza katika mkutano huo amebainisha umuhimu wa dunia kukaa pamoja na kusimamia ajenda ya maji; thamani ya maji katika maisha na uchumi; kuongeza uwekezaji katika eneo la maji; ushirikiano wa kimataifa katika maji; pamoja na utafutaji wa fedha kwa ajili ya maji.


Baada ya kuwasilisha hotuba ya Tanzania katika Mkutano waMaji wa Umoja wa Mataifa, alishiriki katika mjadala wa Uongozi na Usimamizi wa Masuala ya Maji, ambao uliandaliwa na Nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania na Afrika Kusini pamoja na mashirika mbalimbali ikiwemo GWP, UNICEF na UNDP.

Mgeni rasmi katika mkutano huo alikuwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa GWPSA  Mwenyekiti mwenza wa Jopo la viongozi maarufu kuhusu Uwekezaji katika Sekta ya Maji.


"Katika mchango wangu, nilibainisha Uongozi imara wa Dkt.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania katika agenda ya kuongeza msukomo na utashi wa kisiasa, kuongeza bajeti ya maji; na kuimarisha taasisi zinazohusiana na usimamizi wa huduma za maji na utekelezaji wa miradi ya maji."


Aidha, aliainisha pia namna ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan ameibeba agenda ya maji kwa kutambua kuwa kupitia upatikanaji wa maji safi na salama, kutachangia moja kwa moia kumuinua mtoto wa kike na mwanamke ili waweze kutumia muda zaidi katika elimu na shughuli za kiuchumi hivyo kufanikisha ajenda ya Rais ya Samia kumtua mama ndoo kichwani na kufikia usawa wa kijinsia katika maendeleo.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana