Mkuu wa wilaya ya Same Kaslida Mgeni leo ametembelea na kukagua Majengo ya shule ya Msingi Kalemane ambayo baadhi ya paa zake za madarasa zimepeperushwa na upepo Mkali pia na kushuhudia usalama Mdogo wa wanafunzi ambao wanasoma katika Shule hiyo
Baada ya kuwasili katika Shule ya Msingi Kalemane iliyopo kata ya Maore wilaya ya Same, Dc Kaslida amewapongeza wananchi kwa kuonesha juhudi kubwa wanazozifanya hili kuchangia majengo hayo kujegwa kwa haraka.
Akizungumza na viongozi wa shule hiyo na kuwatoa wasiwasi kuwa serikali ipo bega kwa bega pamoja na wananchi wao waliojitokeza katika kushirikiana kwa pamoja kwa kuchangia ujenzi wa madarasa hayo na ameiagiza Ofisi ya Halmashauri ya wilaya hiyo kushirikiana na wananchi lengo wanafunzi waweze kupata Madarasa bora na kusoma bila ya Matatizo yoyote
DC Kaslida ametoa maagizo kwa Ofisi ya Almashauri ya Same pia kubomoa Majengo hayo haraka hiwezekavyo ambayo yametokana na kupata nyufa kwa ndani na nje kwenye hizi Mvua zinazoendelea kunyesha hili kukarabatiwa Upya na kuepusha usumbufu wanaopata baadhi ya wanafunzi kwenda kusoma shule ya jirani.
Mbali na hayo yote DC Kaslida amemshukuru Afisa Elimu kata ya Maore kihoko Stephen pamoja na wananchi kwa ujumla wao kwa kuonesha ushirikiano wa kuweza kutoa hamasa ya michango wa ujenzi wa madarasa hayo na kuwahaidi kuwa serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na Rais wetu Samiha Suluhu Hassani itashirikiana nao kwa pamoja hili majengo hayo yaweze kujegwa kwa haraka zaidi
Post a Comment