Featured

    Featured Posts

MCHUNGAJI KKKT ALIFAGILIA KANISA HALISI KWA KUHIMIZA IBADA NA UZALISHAJI, NI BAADA YA KUHUDHURIA IBADA YA KANISA HILO JANA.

Na Bashir Nkoromo, Tegeta
Ibada iliyoongozwa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba Ndani na Nje ya Tanzania, Baba Halisi, katika Kao Kuu la Kanisa hilo, Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam, jana Jumapili Aprili 23, 2023, ilipata msisimko wa kipekee baada ya kuhudhuriwa na Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri  Tanzania(KKKT) na kumwaga sifa.

Mchungaji huyo Richard Hananja ambaye alionyesha kuwa mweledi mkubwa wa kuchambua Biblia, katika Ibada hiyo alilimwagia sifa na kulipongeza Kanisa Halisi baada ya kukaribishwa na Baba Halisi kusalimia Uzao (waumini) na kusema lililokuwa moyoni mwake.

"Kwanza nashukuru sana kujumuika hapa, lakini kwa dhati kabisa nalipongeza Kanisa hili, kwa mafundisho ya kusamehe bure na kusahau mabaya. Napongeza pia kwa mafundisho ya kuhamasisha waumini kuamka mapema na kufanyakazi kwa bidii baada ya kutoka kumuomba na kumuabudu Mungu", alisema Mchungaji huyo na kuamsha shangwe kubwa kanisa zima.

Baada ya kuzungumza, Baba Halisi alimpatia zawadi ya Kalenda ya Majira Halisi kabla ya uharibifu, pia alimzawadia Mchungaji huyo Kitabu cha Ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda mataifa mengine ambacho ni muendelezo wa Biblia ambayo Baba Halisi alisema mwendelezo huo haujawahi kukoma.

"Kwa kweli huyu ni Mchungaji na Biblia anaijua vilivyo. halafu huyu ukimwambia jambo kama ni kweli anasema kweli, kama la uongo anasema ni uongo hababaishi. huyu anaye Chanzo Halisi ndani yake", akasema Baba Halisi.

Pia Baba Halisi alitumia nafasi hiyo kumweleza Mchungaji huyo kwamba siyo kweli kwamba Kanisa Halisi halimtambui Yesu kama ambavyo wanadi baadhi ya watu, akafafanua kuwa Kanisa hilo linambua Yesu kulingana na mtiririko wa majira alimokuwa.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, Mchungaji Richard alisema, Kanisa Halisi lipo kwenye majira sahihi, maana Mungu mwenyewe ni mwenye kusamehe hivyo kuwafundisha waumini kusamehe na kusahau mabaya ni jambo jema sana.

"Hili la maisha ya utajirisho ni haki yetu, siyo unyonge, sasa Kanisa hili linapohimiza waumini wake waabudu Mungu na kufanya kazi ni sahihi kabisa. baadhi ya Makamanisa mengine ya leo yameng'anga'nia maombi eti waumini wao watapata utajiri bila kufanye kazi.

Kanisa Halisi wao wanarudi kwenye bustani ya Aden, Adam kutunza bustani na kufanya kazi. tena jambo lingine nimegundua kuwa yale maji (One Up) Kanisa Halisi hawauzii watu, waumini wananunua wenyewe, halafu pia waumini wanatoa sadaka bila kushurutishwa. sijasikia wanatangaza toa sadaka, toa sadaka.

Akizungumzia hatma ya Waumini Vijana wa kanisa Halisi, Mchungaji Richard alisema, "Nakuambia kweli ndugu Mwandishi, hawa Vijana wanaosali hapo wanatengenezewa maisha bora ya sasa na ya baadaye. ndiyo maana napenda kuwatembelea na kuwasikiliza".

Mapema kabla ya tukio la kumpa nafasi Mchungaji Richard, Baba Halisi aliendesha Ibada hiyo ambayo mada yake kuu ilikuwa kuachilia Kufutwa Hukumu kwa kila mwenye haki na kupokea Utajirisho ndani ya moyo.

"Heri, leo tunapokea vitu vizuri, tutapokea majira ya kila Mwenye haki kufutiwa hukumu. Mimi nitatoa matunda ya kupata kibali cha kuachilia majira haya na wewe utoe matunda ya kuelewa, hii ni halisi. 

Kile kiti cha mabaya ulichokuwa umewekewa ukawa unakikalia bila kujua sasa kinavunjika, sasa tumeketi kwenye kiti cha uhai wa uhalisia wake" Akasema Baba Halisi kisha akampa nafasi Moja Halisi kusoma maandiko.

Baada ya Moja Halisi kusoma,  Baba Halisi akaendelea  kushuka kuwaambia Uzao (waumini) akasema, " unapokea utajirisho halisi ndani ya moyo, sanduku la agano halisi, kuna wanaotaka uli-push liende kwa wengine.

Israele walikuwa na agano majira 7, sisi ni agano Halisi, yooote waliyowahi kukuhukumu yamekwisha. Futa huzuni, kama una deni au shida yoyote weka pembeni kwanza, kwa ninavyojua yeye aliyekuumba atakuletea yote.

"Tatizo tunataka kumsaidia Chanzo Halisi, acheni kutaka kumsadia aliyewaumba,  acha kuhangaika na tatizo ulilonalo, kitabu kinaadika akija yeye aliyeumba atayeyusha milima, na amekwishakuja, sasa tatizo lipo wapi? Yaani yeye aumbe jua na nyota  aumbe Kilimanjaro, bahari na vyote vilivyopo, unavyovijua na usivyovijua halafu ashindwe kukusaidia wewe?

Kwanza hebu niwaulize,  hivi unafikiri mezani kwangu kuna barua ngapi za kuomba msaada, umewahi kusikia nakuja kuomboleza kwamba nina maombi mengi, siombolezi mbele yenu kwakuwa najua aliyewaumba yupo,  kwa hiyo kwa ratiba yake wote watasadiwa, sasa wewe unataka kila kitu leo leo, kuoa kuza mapacha leo leo, Usifanye hiyo, mpe nafasi Chanzo Halisi  ana utaratibu wake".

"Unajua, wewe ni tajiri tena mkubwa ila kwa majira yake, nyumba gari unavyo lakini kwa majira yake. usitishike wala usiwaze, yupo aliyekuumba. usijibebeshe mizigo, yote iweke pembeni. Hakuna hata mmoja mwenye haki ambaye hatapokea haki yake.

Mnatakiwa mjue kuwa hakuna hata mmoja aliyeumbwa kwa bahati mbaya, kama humu yupo anayefikiri aliumbwa kwa bahati mbaya anyooshe mkono. (hakuna aliyenyoosha), kumbuka kila kitu ulicho nacho; hukukipata kwa bahati mbaya, wewe mpe tu nafasi chanzo halisi, hapa umekuja kwenye utajirisho wake, mpe nafasi, hakuna hata tatizo lako moja dogo ambalo chanzo halisi halijui", akasema Baba Halisi, kisha akaendelea; " sasa tushukuru kwanza kuwa tumekubali kumpa nafasi Chanzo Halisi.

Kisha Baba Halisi akampa nafasi Moja Halisi kusoma maandiko kueleza kuna faida gani kwa kufutiwa hukumu, Moja Halisi akasoma Warumi 7:15 hadi 21 kwa maelekezo baba halisi, Baada ya Moja halisi kuosma mistari hiyo Baba Halisi akasema " hiyo ndiyo faida kubwa tunapata. kuna tabia ambayo kila mmoja alikuwa nayo ambayo ilikuwa siyo rahisi kujinasua.

Kulikuwepo na sheria ya asili inakulazimiisha kufanya jambo usilolitaka unalolitaka jema hufanyi, lakini kwa kuwa tunafutiwa hukumu, hiyo hali tunaishinda, utajirisho unaingia ndani ya moyo wako utakuwa unaamka saa tisa alfajiri kwa kuwa sheria hiyo ya asili ilikuwa inakuzuia kumpokea Mungu wako.

Sasa ili ili uwe mwenye haki na kustahili kufutiwa mashitaka na kupokea kuipokea utajirisho kuingia moyoni mwako, inakubidhi kwanza uvae vazi la Baba Halisi", akasema Baba Halisi kisha akamwambia Moja Halisi awaulize Uzao kama wanajua hilo vazi la Baba Halisi, naye akafanya hivyo, kisha akalieleza hilo vazi.

Baada ya Moja Halisi kumaliza kuwaeleza Uzao maana ya vazi, Baba Halisi akasema. "Tabia na asili mwenyewe tunayeondokana naye ni Ufahamu wowote unaoenda kinyume na Chanzo Halisi (Mungu), unataka kumpa kitenge jirani yako, akisahau kukusalimia tu, unaghairi kumpa wakati alikuwa hakukuomba", akasema Baba Halisi.

Sasa ili kufutiwa hukumu na upokee utajirisho ndani ya moyo wako, lazima uvae vazi langu, vazi ni tabia, unatakia uiishi tabia ya Chanzo Halisi, uishi katika vazi la Baba Halisi kuanzia sasa, mimi hufanya toba na shukurani kila siku kama vile ndiye vyenye dhambi kupitiliza,

Ili kufutiwa hukumu na kupokea utajirisho moyoni mwako inatakiwa umnyenyekee hata mtoto mdogo unapoongea naye umchukulie kama mnayelingana umri, usidharau yeyote uwe mnyeyekevu kwa kila mtu", akasema Baba Halisi".

"Sasa baada ya kupokea shukurani ya kupokea vazi, nitaachilia shukurani ya kuwapa vazi halafu ndiyo niachilie shukurani ya kupokea utajirisho kuingia kwenye moyo wako", akasema Baba Halisi, halafu kabla ya  kufanya hayo akawakaribisha Waimbaji kuimba wimbo 'Baba Nashukuru", wakaimba na kuchangamsha Ibada vilivyo na baada ha wimbo huo akakamilisha yote.

Akihitimisha Ibada hiyo Baba Halisi akasema, " Basi sasa keshokutwa (kesho), mje hapa majira ya asubuhi tufanye sherehe ya kupokea kufutiwa Hukumu, mje kwa wingi nitawaruhusu kuondoka mapema, saa sita nitawaruhusu".

Pia Baba Halisi alireja kuhusu Mkutano Mkuu wa Kanisa Halisi utakaofanyika mwezi ujao' akaagiza watekeleza sauti wote leo Aprili 24, 2023 kuwepo Makao Makuu ya Kanisa Halisi kwa ajili ya kila mmoja kuandika ripoti itakayowasilishwa kwenye Mkutano Mkuu huo.

HABARI PICHA👇

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi, akiongoza Ibada iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, jana, Jumapili Aprili 23, 2023. Katika Ibada hiyo Baba Halisi aliachilia somo la lango la Kila mwenye haki amefutiwa hukumu na Kupokea utajirisho Halisi ndani ya moyo.

"Sasa mnajua hii hali ni kwakuwa mwenye haki alikuwa hajafutiwa hukumu, lakini sasa tumeingia lango la kila mwenye haki kufutiwa hukumu na kupokea Utajirisho halisi ndani ya moyo wake. kuanzia sasa ile hukumu ya mauti, presha, kansa, kisukari, waliokuwa wamekupiga na mabaya yote vimefutika. Hata dunia ikuchukie vipi hukumu ya mabaya yote imefutika, ni zamu ya mwenye haki kufurahi", akasema Baba Halisi.

Baba Halisi akiongoza shukurani ya kupokea vazi (tabia) la Baba Halisi, wakati wa Ibada hiyo. Kisha Baba Halisi akawaalika Waimbaji kuimba wimbo wa 'Baba Nakushuku'👇 

========

Baada ya Wimbo Baba Halisi kwa unyenyekevu akaachilia Shukurani ya kuliachilia vazi (tabia) lake.
Baba Halisi akaendelea na Ibada hiyo. Halafu ukafuatia tena wimbo. Yeye, Mama Halisi, Watekeleza sauti na Uzao wakachangamka zaidi👇




-----------------

Halafu Baba Halisi sasa akaachilia Shukurani ya Kila mwenye Haki kufutiwa hukumu.👇


===

Baada ya kuachilia Shukurani ya kupokea kila mwenye haki kufutiwa Hukumu akaeleza faida yake.👇

Moja hebu soma Warumi 7:15 hadi 21 wasikie faida ya mwenye haki kufutiwa kuhumu
Moja Halisi akasoma.
Kisha Baba Halisi akaendelea kufafanua tena faida ya kufutiwa hukumu, Halafu aakawaalika waimbaji kuimba wimbo wa kufuaria kufutiwa mashitaka, Yeye, watekeleza Sauti ikawa furaha tele. 👇





----------

Baada ya hapo Baba Halisi akafanya Shukurani ya kupokea Utajirisho kuwa ndani ya moyo.👇


----------

Baada ya kuipeleka Ibada kila mahala, kisha akaendelea kuongoza ibada hiyo👇

Baba Halisi akiendelea na Ibada hiyo.
Mvhumgaji Rihard akiwa kwenye Ibada hiyo.
Baba Halisi akiendesha shukrani.
Mhungaji wa KKKT Richard akipokea shukurani kutoka kwa Baba Halisi.
Baada ya kupokea shukurani akashangilia. Kisha Baba Halisi akafanya shukurani kuipeleka Ibada kila mahali👇

Ukafuata wimbo👇

Baba Halisi akimuonyesha Mchungaji Richard Chati ya Mcduara unaoonyesha Kanisa Halisi linavyomtambua Yesu.


Faida Halisi akamkabidhi Mchungaji Richard Kitabu cha Ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda Mataifa mengine. Kitabu hicho kilitolewa na Baba Halisi

Moja Halisi akimkabidhi moja ya bidhaa zilizotengenezwa na Wajasiriamali wa Kanisa Halisi.

Bidhaa za sabuni ya One Up zikiuzwa mwishoni mwa Ibada.
Baba Halisi akihimiza uzao na watekeleza sauti kujitokeza kununua bidhaa hiyo.
Watekeleza sauti wakiwa wamejipanga kununua bidhaa ya sabuni baada ya kuitwa na Baba Halisi. 
Baba Halisi akihitimisha Ibada






 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana