Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi katika ufafanuzi wake juu ya ziara aliyoifanya tarehe 10 Julai 2021 kwa wakaazi wa nyumba chakavu za Kilimani kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Katika mkutano wake na waandishi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari ambao umefanyika leo tarehe 29 Aprili 2023 Ikulu Zanzibar Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali itasubiri mapendekezo kutoka kwa kamati ya wakaazi wa Kilimani ambayo itasimamia maoni ya wananchi na baadae yawasilishwe Serikalini.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amefananua kuwa lengo la Serikali ni kuendelea kutoa huduma bila malipo na kuboresha huduma za afya kwa sekta binafsi ili kuleta ufanisi na uharaka wa huduma hizi za Afya ikiwemo huduma ya vipimo vya maabara, mionzi, utoaji wa huduma za chakula, usafi na kutoa dawa.
Pia, Dk. Mwinyi amezungumzia mkataba wa uchimbaji wa mafuta na gesi Zanzibar kwa kampuni ya RAK GAS, ambayo iliingia mkataba na Serikali ya awamu iliyopita. Kampuni hiyo imeshindwa kutekeleza makubaliano ya mkataba ya awali ikiwemo kuchimba kisima cha kwanza kwa mujibu wa mkataba na hatua nyinginezo.
Hivyo, Serikali imewataka RAK GAS kuandika barua kueleza hatua waliyofikia kuhusu kuendelea na mkataba huo.
Post a Comment