Featured

    Featured Posts

TRA YAAGIZWA KUTOWATOZA KODI KABLA WAJASIRIAMALI WAPYA

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), akijibu swali bungeni jijini Dodoma la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani, kuhusu malipo ya Kodi kwa Wajasiriamali kabla ya kuanza rasmi kufanya biashara.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma)

 


Na. Peter Haule, WFM, Dodoma

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) amemuagiza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha wajasiriamali wapya hawatozwi kodi kabla ya kuanza kufanya biashara. 

Mhe. Chande ametoa agizo hilo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Ng'wasi Damas Kamani, alipotaka kujua ni lini Serikali itaona haja ya kuondoa malipo ya kodi kwa wajasiriamali kabla ya kuanza rasmi kufanya biashara.

Mhe. Chande alisema kuwa Serikali kupitia Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2019, Kifungu cha 43 imetoa unafuu wa kutolipa kodi kwa kipindi cha miezi sita  kwa biashara mpya tangu muhusika anapopewa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi,  lengo likiwa kumpa mjasiriamali nafasi ya kustawi kibiashara.


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana