Featured

    Featured Posts

MBUNGE KOKA AVALIA NJUGA UMEME, MAJI


Na Dismas Lyassa, Kibaha

MBUNGE wa Jimbo la Mjini, Silvestry Koka ameahidi kulivalia njuga suala la huduma ya nishati ya umeme na maji ambalo limekuwa kero katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo.

Akizungumza kwenye semina ya mafunzo kwa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Kibaha Mjini amesema lengo kubwa ni Kuhakikisha anawatatulia wananchi changamoto zinazowakabili katika sekta mbali mbali.

Kadhalika aliwaomba wananchi waweze kuendelea kushirikiana na Serikali ili waweze kupatiwa miradi mbali mbali ya kimaendeleo kwa manufaa ya wananchi wa Jimbo la Kibaha mji na Taifa kwa ujumla.

Mbunge huyo hakusita kuwakumbusha viongozi kijitahidi kwa hali na mali katika kuongeza idadi ya wanachama lengo ikiwa ni katika kukiimarisha chama zaidi kiweze kushinda katika chaguzi mbali mbali.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana