Na Bashir Nkoromo, CCM Blog JNICC
Kituo cha Mikutano cha Mimataifa Arusha (AICC) kilianzishwa chini ya sheria namba 17 ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1969 chini ya mamlaka ya rais, kupitia tangazo la Serikali namba 115 lililochapishwa Agosti 25, 1978.
Ni kituo kinachofanyakazi kama shirika kamili la umma linalojiendesha kibishara, biashara kuu ikiwa ni uanadaaji mikutano na matukio ya kitaifa, kikanda na kimataifa.
Bila shaka mikutano inapofanyika nchini mafanikio huwa hayako katika kituo hicho peke yake bali washiriki wote katika mnyororo wa thamani na wakiwemo wafanyabiashara za bidhaa na huduma ikiwemo utalii, usafiri, malazi, uuzaji wa mavazi na vyakula.
Akizungumza katika mkutano na Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari, katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijni Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa AICC Epraim Mafuru anasema, AICC mbali na kuingiza mapato kwa kutumia Kituo hicho kilichopo Arusha, kinaingiza pia fedha kupitia Ukumbi wa JNICC ambao upo chini yake.
Mafuru anasema, hadi sasa kwa pamoja kumbi za AICC na JNICC wanao uwezo wa kuandaa mikutano yenye uwezo wa kuchukua watu 1300 kwa wakati mmoja, japokuwa anasema bado siyo kiasi ambacho kinakidhi malengo.
"Maono ya AICC ni kuwa mfano na kiungo muhimu katika biashara ya utalii nchini pia AICC inayo dhamira ya kukuza na kutoa huduma bora za biashara ya utalii kwa wateja wa kitaifa na kimataifa kwa ajili ya kuimarisha maendeleo ya kitaifa, kijamii na kiuchum", anasema Mafuru.
Anasema AICC kama shirika la umma lenye mtizamo mpana wa kukuza diplomasia ya uchumi kama anavyoielekeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuamini katika uwekezaji wa mkubwa wa kisasa katika uandaaji wa matukio na mikutano ya kimataifa kwa viwango vya hali ya juu,
Mafuru anasema, katika moja ya hatua za kufanikisha adhma hiyo AICC imejipanga kujenga kituo kipya cha mikutano jijini Arusha kitakachojulikana kwa jina la Kilimanjaro Intrnation Confrerence Centre (KICC) kitakachokuwa na uwezo wa kuchukua watu hadi 3000 na kuwa na kumbi ndogo ndogo na pia kujenga hoteli ya nyota tano ya kisasa.
Anasisitiza kuwa AICC inatambuwa kuwa Uchumi wa mikutano ni moja kati ya avyanzo vizuri ya fedha za kigeni ambazo dunia nzima hivi sasa ina shida nazo, akisema leo hii ukitaka dola milioni moja kwa haraka huwezi kuzipata katika nchi zilizo nyingi.
Mafuru anasema, pamoja na Uchumi wa mikutano kuwa kati ya vyanzo vya fedha za kigeni lakini pia ni moja ya njia za kutekeleza diplomasia ya uchumi, inayosimamiwa na Rais Dk. Samia ambaye tayari ameshafanya jitihada za kuifungua dunia kidiplomasia.
Akifafanua Uchumi wa mikutano unavyoweza kuinngizia nchi fedha, Mafuru anasema; "wastani wa mgeni mmoja huweza kutumia sh. milioni moja kwa siku, kwa kula na manunuzi ya bihaa mbalimbali hivyo wakiwa zaidi ya 3000 na wakakaa siku sita ni fedaa nyingi ambayo inaingia Tanzania.
Mfuru akieleza mikakati ya AICC alisema katika kutana huduma zake, inafanyika mipango ya kujenga ukumbi mkubwa zaidi wa JNICC jijini Dar es Salaam, mbali na ule unaotarajiwa kujengwa jijini Arusha wa KICC), hivyo akaomba Watanzania kuunga mkono harakati wa ukuaji wa Kituo hicho cha AICC.
Pia katika kuwajuza Wahariri katika mkutano huo, alidokeza kuwa upo mpango wa kufanya 'mwavuli' utakaosimamia kwa pamoja AICC na JNICC tofauti na sasa ambapo JNICC inafanya kazi chini ya AICC.
Akizungumzia changamoto, Mafuru alisema, ni pamoja na madeni ya fedha kiasi cha Sh. bilioni 7.4 na ambao AICC izidai taasisi mbali mbali, akifafanua kwamba katika ya madeni hayo taasisi za serikali zinadaiwa sh. bilioni 4.76 ambayo ni sawa asilimia 65 ya madeni yote, huku Sh. bilioni 3.22 likiwa ni deni la zaidi ya miazi sita. na kuongeza kuwa kati ya 'top 20' 17 ndiyo taasisi hizo za serikali.
Mafuru alisema, changamoto iliyopo kwenye madeni hayo ni kwamba AICC Kama Shirika la Umma haiwezi kutumia nguvu kuzidai taasisi za serikali kama inavyofanya kwa taasisi binafsi, hivyo akawasihi wakuu wa taasisi za kuona umuhimu wa kulipa madeni hayo kwa kuwa ni fedha ambazo zitachangia uchumi wa taifa.
Msikilize hapo Mafulu hapo👇.
Post a Comment