Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa (UWT) Mary Chatanda amesikitishwa na namna ya utendaji kazi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Ndg. Veronica Vicent Sayore.
Chatanda ameyazungunza hayo mapema leo alipokuwa akiagana na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega sambamba na watumishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Busega.
"Nimesikitishwa sana na tabia ya Mkurugenzi wa hapa Busega amekuwa sio mtu wa kushirikiana na wenzake, hili suala halikubaliki kwani viongozi wa Chama ndio wenye Ilani ya CCM hivyo basi anapashwa kuwa shirikisha kwenye kila suala linalohusu maendeleo kwenye Wilaya hii"
Mwenyekiti wa UWT Taifa amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku moja Wilayani Busega ambapo leo anatarajia kuendelea na ziara yake Wilaya ya Bariadi.
Post a Comment