Kinondoni, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Rajabu Mbwambo amewahimiza wananchi kuzidi kumuunga mkono na kumpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi anazofanya kuhakikisha huduma za jamii katika mkoa huo zinafika kote.
Mwajabu amewahimiza wananchi hao jana katika mkutano uliohudhuriwa na wajumbe wapatao 400, wakiwemo Wenyekiti, Makatibu wa Kata na matawi, wa Jumuiya hiyo Wilayani Kinondoni, katika mwendelezo wa ziara aliyofanya katika Wilaya hiyo akiongozana na Kamati ya Utekelezaji UWT mkoa huo. Wiyala ya Kinondoni ina majimbo mawili, Kata 20, matawi 141na mashina 1,537 ya CCM na mitaa 106.
Katika mkutano huo Mwenyekiti Mwajabu aliwakumbusha viongozi hao kuwa na mikakati madhubuti kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 na kuhamasisha wanawake na kuwajengea uwezo wale wenye sifa ili waweze kuwania uongozi wa wenyekiti wa serikali za mitaa katka mitaa 106, ikiwa ni utekelezaji kwa vitendo ajenda ya 50 kwa 50.
Mwenyekiti Mwajabu aliwaasa viongozi wa UWT kuanzia wilaya, kata na matawi kuhakikisha wanaiweka kwenye vitendo falsafa ya 4R iliyo asisiwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika utendaji wao wa majukumu ya kila siku na pia kuwa mstari wa mbele kuyasemea mema yanayofanywa na serikali ya awamu ya sita ndani ya wilaya ya kianondoni.
Pamoja na Mkutano huo, katika ziara hiyo walitembelea miradi minane (8) katika wilaya hiyo, yote ikiwa imetekelezwa kwa kiwango cha juu ikiwa ni juhudi za Rais Dk. Samia kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi wa wilaya hiyo ya kinondoni, ambazo ni vituo vya afya, shule za msingi na sekondari, na miradi ya maji.
Wajumbe wakimsikiliza Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Mwajabu Rajabu Mbwambo wakati akizungumza nao katika mkutano huo. Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Mwajabu Rajabu Mbwambo akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kufika Ofisi ya UWT Wilaya ya Kindoni, jana.
Mwenyekiti Mwajabu akitazama bidhaa za mjasiliamali
Mwenyekiti Mwajabu akikagua miradi mbalimbali iliyofanyika katika utekelezaji wa Ilani ya CCM Kinondoni👇










Post a Comment