Featured

    Featured Posts

TIRA YATAKA SOKO LA BIMA LISILO NA UTAPELI, YAWAALIKA WAANDISHI KUYAMULIKA KWA KARIBU MATUKIO YANAYOJIRI KATIKA SOKO HILO

Na Bashir Nkoromo, Official CCM Blog
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ni kati ya Mashirika ya Umma yanayosimamiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OMH), yenye dhamana ya kusimamia mali na uwekezaji wote wa Serikali kupitia taasisi au mashirika ya Umma takribani 300 ambayo kati yake 248 serikali inayamiliki kwa asilimia 100.

Kwa taarifa za hivi karibuni za Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu, maboresho yanayofanywa na ofisi yake yanalenga kuhakikisha mashirika yanatoa gawio linalofikia asilimia 10 ya bajeti ya serikali kutoka asilimia tatu tu ya sasa. Kwa sasa, uwekezaji wote wa Serikali katika Taasisi na Mashirika ya Umma ni zaidi ya Sh. Trilioni 70.

Bila shaka, kutokana na uwekezaji huo mkubwa wa Serikali katika Taasisi na mashirika hayo, lazima Msajili wa Hazina 'akomae' vilivyo, na pia vongozi wa Taasisi na Mashirika hayo nao lazima wapambane vilivyo ili serikali isiingie hasara kizembe.

Moja ya hatua kati ya nyingi ambazo Msajili wa Hazina amezichukua, ni kuzielekeza Taasisi na Mashirika ya Umma kuwa na utaratibu wa kuujulisha umma utendaji, njia mojawapo ambayo ameichukua kukidhi hilo ni Taasisi na Mashirika hayo kuwasilisha taarifa ya utendaji wake  kwa Wahariri wa vyombo vya habari, kupitia mikutano maalum.

Katika muktadha huo, tayari Taasisi na Mashirika kadhaa yameshafanya hiyo, kupitia mikutano iliyoandaliwa na Msajili wa Hazina, na jana, Septemba 18, 2023 ilikuwa zamu ya TIRA ambayo uongozi wake wa juu uliweza kuwasilisha taarifa ya utendaji wa Mamlaka hiyo katika uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Katika mkutano huo, Kamishna wa Bima Dk. Baghayo Saqware ambaye alifuatana na Naibu Kamishna Khadija Said kutoka Zanzibar, alieleza kwa kina utendaji wa TIRA, ikiwemo malengo wanayojipanga kufanya ili Mamlaka iweze kuwa kukidhi zaidi uwepo wake.

Kutoka katika taarifa yake Dk. Saqware, alisema, Mamlaka kwa kushirikiana na Bodi ya Taifa ya Bima itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwenye Sekta ya Bima kwa ajili ya kuendeleza na kusimamia soko la Bima kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.

"Mamlaka inapenda kuona soko la Bima lisilokuwa na udanganyifu, lenye ushindani, soko linalofuata weledi na soko lenye kuleta faida. Napenda kuwaalika wandishi wote wa habari kuendeleza sekta ya bima kwa kuitangaza mara kwa mara na kufuatilia matukio mbalimbali yanayoendelea kwenye soko la bima" akasema Dk. Saqware.

Kwa jumla Dk. Saqware aliwasilisha mambo mengi mazuri yaliyorandana na Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pia ikiwemo kukidhi malengo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuinua huduma na uchumi wa nchi kupitia sekta mbalimbali, hali kadhalika kukidhi malengo ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi hasa katika kuushajihisha Uchumi wa Buluu.

Msimamizi Mkuu wa Blog hii ya Taifa ya CCM (Official CCM Blog), alikuwa miongoni mwa Wahariri zaidi ya 40 waliohudhuria Mkutano huo na TIRA. Hivyo kwa kuwa unayo haki ya kuyajua kwa kina aliyosema DK. Saqware, tumeweka hapa taarifa yote kama alivyoiwasilisha.  

Tafadhali isome hapo👇

MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BIMA TANZANIA (TIRA)
TAARIFA YA KAMISHNA WA BIMA DKT. BAGHAYO A. SAQWARE KWA WAANDISHI WA HABARI TAREHE 18 SEPTEMBA 2023 - SERENA HOTELI - DAR ES SALAAM SEPTEMBA, 2023


1.0 UTANGULIZI
1.1 Uanzishwaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania na Majukumu yake.


Mamlaka imeanzishwa kwa Sheria ya Bima ya mwaka 2009 Sura Na. 394 ikiwa na majukumu yafuatayo:
i. Kusajili na kutoa leseni kwa watoa huduma za bima;
ii. Kuandaa na kutoa Kanuni na Miongozo mbalimbali ya kusimamia soko la Bima na Kurekebisha Sheria;
iii. Kutoa elimu ya bima kwa Umma;
iv. Kulinda haki za mteja wa Bima;
v. Kushauri Serikali kuhusu mambo ya Bima.


1.2 Muundo wa Mamlaka
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima ni Taasisi ya Muungano chini ya Wizara ya Fedha na inaongozwa na Kamishna wa Bima akisaidiwa na Naibu Kamishna na inasimamiwa na Bodi ya Taifa ya Bima inayoongozwa na Mwenyekiti wa Bodi.


Muundo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) uliidhinishwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo tarehe 11 Septemba 2021. Muundo ulioidhinishwa unajumuisha Ofisi ya Msuluhishi wa Migogoro ya Bima (TIO), Kurugenzi tatu (3), Ofisi ya Zanzibar, Ofisi za Kanda na Vitengo saba (7).


Ofisi za Mamlaka
Ili kuongeza tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake na kusogeza huduma kwa wananchi, Mamlaka hadi kufikia sasa ina ofisi zifuatazo;
i. Makao Makuu Dodoma;
ii. Ofisi ya Zanzibar;
iii. Ofisi ya Dar es Salaam;
iv. Kanda ya Magharibi (Tabora, Katavi na Kigoma)
v. Kanda ya Mashariki (Dar es Salaam, Pwani na Morogoro);
vi. Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya, Njombe, Rukwa, Iringa na Songwe);
vii. Kanda ya Ziwa (Mwanza, Mara, Shinyanga, Kagera, Simiyu na Geita);

viii. Kanda ya Kaskazini (Arusha, Kilimanjaro na Tanga)
ix. Kanda ya Kati (Dodoma, Singida na Manyara); na
x. Kanda ya Kusini (Lindi, Mtwara, na Ruvuma).


1.3 Kuandaa na kutoa Kanuni na Miongozo mbalimbali ya kusimamia soko la Bima na Kurekebisha Sheria:
Soko la bima linaongozwa kwa Sheria, Kanuni, Miongozo na taratibu mbalimbali.


Kati ya mwaka 2022 na 2023 Mamlaka kwa kushirikiana na wadau wa bima wamefanikiwa kuandaa Miongozo mbalimbali kwa ajili ya kusimamia na kuendeleza soko la bima. Miongozo hiyo ni pamoja na:
i. Mwongozo wa Usimamizi wa Ubakizaji wa Bima na Bima Mtawanyo;
ii. Mwongozo wa Bima ya Afya na usajili wa Watoa Huduma za Afya;
iii. Mwongozo wa Utoaji wa Ithibati kwa Warekebishaji na Watengenezaji wa Vyombo vya Moto katika Sekta ya Bima;
iv. Mwongozo wa Uendeshaji huduma za Takaful;
v. Mwongozo wa Utoaji Huduma za Bima Kidijitali;
vi. Mwongozo wa Maafisa Wauza Bima;
vii. Mwongozo wa Utekelezaji wa viwango vya kimataifa vya taarifa ya kifedha kuhusu mikataba ya Bima (IFRS 17);
viii. Mwongozo wa Uwekezaji na Usimamizi wa Ukwasi;
ix. Mwongozo wa Kushughulikia Madai ya Bima;
x. Mwongozo wa Uendeshaji wa Biasharaya Benkiwakala;
xi. Mwongozo wa Viwango Elekezi vya Fidia ya Bima kwa Madai ya Majeraha ya Mwili na Vifo kwa mtu wa tatu kutokana na ajali za 1.4 Kusajili na kutoa leseni kwa watoa huduma za bima:
Mamlaka imefanikiwa kusajili watoa huduma za Bima na Majukumu yao kama ifuatavyo:


KAMPUNI IDADI MAJUKUMU KWENYE MNYORORO WA
BIMA

Kampuni za Bima Mtawanyo (Reinsurance Companies)
Kubeba dhamana ya Kampuni ya Bima kulipa mafao na fidia.


Kampuni za Bima Mtawanyo kibali cha Biashara-Nje ya Nchi
35 Kampuni za Bima 33 Kulipa mafao na fidia kwa mkata bima
Kuwekeza tozo za bima (premiums)

KAMPUNI IDADI MAJUKUMU KWENYE MNYORORO WA
BIMA

Wataalamu wa Ushauri wa Bima Mtawanyo (Reinsurance Brokers)

Washauri wa mkata bima kwa kampuni ya bima Wataalamu wa Ushauri wa Bima Mtawanyo waliopewa kibali cha kufanya Biashara-Nje ya Nchi 24 Wataalamu wa Ushauri wa Bima (Insurance Brokers)100 Hutoa usahuri kwa wakata bima
Mawakala wa Bima (Insurance Agencies) 930 Mwakilishi wa mkata bima kwa Kampuni ya imaBenkiwakala(Bancassurance Agency) 31 Wauza Bima Kidijitali (Insurance Digital Platform)
9 Kutoa huduma ya uuzaji/ununuaji wa bima kwa njia za kidigitali kwa niaba ya Kampuni za bima Wakadiriaji Hasara 46 Kukadiria hasara ya janga lilitokea kwa ajili ya malipo ya bima
Kampuni za Takwimu Bima (Actuarial Firms)


Kutathmini na Kuthaminisha mali za bima Wachunguzi Binafsi  Kupata ukweli wa kuhusu madai ya wateja Maafisa Wauza Bima 100 Wawakilishi wa wateja wa Kampuni za Bima na Wataalam wa Washauri wa Bima


2.3 Utoaji wa Elimu kwa Umma
2.3.1 Mamlaka inaendelea na mkakati wake wa utoaji wa elimu kwa umma kwa kushirikisha wadau wote kwenye sekta. Lengo ni kufikia asilimia 80% ya watanzania wote wenye umri wa miaka zaidi ya kumi na nane (18) ifikapo mwaka 2030.


2.3.Aidha, Mamlaka inaendelea na utekelezaji wa mkakati wa utoaji Elimu na Uhamasishaji kwa Wizara na Taasisi za Umma kutekeleza SHERIA YA BIMA SURA NA. 394 YA 2009, NA SHERIA YA MANUNUZI, NA.7 YA 2011.
i. Lengo la mkakati ni utoaji elimu ya bima na uhamasishaji wa Serikali, Idara, Taasisi za Umma ili ziweze kuzingatia Sheria ya Bima Sura 394, kif.133 (1) hadi (3), kif.140 na Sheria ya Umma Na. 7 ya Mwaka 2011, kif. 4 (2) (b).
ii. Hadi mwezi Julai 2023, Mamlaka imezitembelea Wizara za Kilimo;
Wizara ya Nishati na Wizara ya Uchukuzi na Ujenzi na TAMISEMI.
iii. Mkakati huu ni endelevu na utazifikia Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali za Umma.

2.4 Kulinda haki za mteja wa Bima
i. Mamlaka imeendelea kuzisimamia kampuni za bima kuhakikisha zinalipa madai na fidia stahiki kwa wakati na kwa haki. Hadi sasa ulipaji wa madai na fidia stahiki kwa wateja wa bima yamefikia asilimia 95 hivyo kupungua kwa malalamiko. Hata hivyo asilimia 5 ya madai na fidia yana changamoto ambazo TIRA inafuatilia na kutoa suluhisho.


ii. Kwa mfano, ulipaji wa madai ya bima za kawaida uliongezeka kwa asilimia 10.1 kutoka shilingi bilioni 301.9 mwaka 2021 hadi shilingi bilioni 332.09 mwaka 2022.
iii. Malipo ya madai na mafao ya bima za maisha yaliongezeka kwa asilimia 29.3 kutoka bilioni 95.7 mwaka 2021 hadi bilioni 123.71 mwaka 2022.


iv. Jumla ya kiasi cha madai kilicholipwa mwaka 2022 ni shilingi bilioni 455.80 hivyo, kupunguza umaskini kwa wanufaika na kufanya biashara kuwa endelevu.
v. Aidha, Mamlaka inaendelea na uendeshaji wa mikutano ya kupokea na kusikiliza malalamiko ya bima kwa wananchi ambapo hivi karibuni Mamlaka imefanikiwa kuandaa mikutano mitano katika kanda zote za Mamlaka.


2.5 Kuishauri Serikali kuhusu bima
Mamlaka imeendelea kuishauri Serikali katika mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na; eneo la ukatiaji wa bima za lazima, ukatiaji wa bima kwa mali za serikali na Bima ya Afya kwa wote ,n.k


2.6 Ukuaji wa Sekta ya Bima
Sekta ya Bima imekua kwa wastani wa asilimia 12.8% kwa mwaka ambapo kwa kipindi cha miaka mitano mauzo ghafi ya bima yameongezeka kutoka Tsh. Bilioni 691.9 mwaka 2018 hadi kufikia takribani Trilion 1.2 mwaka 2022.


Mchango wa Sekta ya Bima kwenye pato la Taifa unazidi kuongezeka kutoka asilimia 0.56% kwa mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 1.68% kwa mwaka 2021.


Mamlaka imeendelea kuongeza gawio Serikalini ambapo kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Juni 2023 Mamlaka imeweza kulipa gawio kwa Serikali la jumla ya Tsh. Bilioni 2.9.
Sekta ya bima imechangia kwenye ajira kwa vijana ambapo hadi Septemba 2022 imetoa ajira za kudumu kwa Watanzania 4, 173.


3.0 UTEKELEZAJI WA MIRADI
3.1 Mradi wa TIRAMIS na TIRA-ORS
TIRAMIS na TIRA-ORS ni kifupi cha TIRA Management Information System na TIRA Online Registration System.
(i) Mamlaka, kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2019/2020 hadi 2021/2022, imetekeleza miradi miwili ya Mifumo ya TEHAMA (TIRAMIS na TIRA-ORS), mifumo hii yote imejengwa na watumishi wa umma.


(ii) Mifumo yote miwili inafanya kazi na imesaidia kuleta manufaa kadhaa kwenye
soko ikiwa ni pamoja na:
• Kurahisisha huduma za utumaji na upokeaji wa taarifa za kibima miongoni mwa wadau;
• Kurahisisha usimamizi wa biashara ya bima nchini;
• Kuharakisha uchambuzi wa takwimu na utaoji wa taarifa.


4.0 MAFANIKIO YALIYOPATIKANA
Katika kipindi cha mwaka wa Fedha wa 2022/2023 Mamlaka imepata mafanikio kadhaa ikiwa ni pamoja na:
4.1 Uanzishaji wa Konsotia ya Bima ya Kilimo
i. Ili kutekeleza skimu ya bima ya Kilimo Tanzania kwa ufanisi, tarehe 01 Julai 2023, kulizinduliwa Konsotia ya Bima ya kilimo (Agriculture Insurance Consortium). Uzinduzi huo ulifanyika Mkoani Tabora ambapo ulifanywa na Mh. Waziri Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo katika kilele cha Siku ya Ushirika Duniani (SUD).
ii. Konsotia ya Bima ya Kilimo imeanzishwa ili kuweka ufanisi katika utekelezaji wa Skimu ya Taifa ya Bima ya Kilimo (TAIS) na kuongeza uwezo wa kimtaji wa soko la bima nchini kwa ajili ya kukinga majanga kwenye sekta ya kilimo.

iii. Ushiriki na mtaji kwa kila Kampuni Konsotia ya Bima ya Kilimo imeundwa na kampuni za bima zinazotoa bima ya kilimo zipatazo 15 ikiwa ni pamoja na kampuni za Bima mtawanyo zilizosajiliwa nchini na za kikanda zipatazo tatu (3) ziitwazo Tanzania Reinsurance Company (TAN-RE), Africa Reinsurance Corporation (Africa Re), na PTA Reinsurance Company (ZEP-RE). Mtaji wa kukinga majanga yenye thamani ya shilingi bilioni 300 umetengwa kwa ajili ya kukinga majanga kwenye sekta ya kilimo.
iv. Faida na mategemeo ya Konsotia ya Bima ya kilimo ni pamoja na:
a) Kuongezeka kwa upatikanaji wa mtaji unaohitajika na kutumika katika ulipaji wa fidia na madai ya Bima kwenye sekta ya kilimo;
b) Kuongeza kasi ya utekelezaji wa Mpango na Mikakati ya Kitaifa kama vile: Agricultural Sector Development Programme (ASDP II),
Financial Sector Development Master Plan (FSDMP-2030),
National Five Year Development Plan (FYDP III) na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (2020-2025).
c) Kushirikiana katika ubunifu, uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma za bima ya kilimo rahisi, zinazoaminika, na za bei nafuu;
d) Kuongezeka kwa nguvu ya pamoja ya kutafuta huduma za Bima mtawanyo za bei nafuu zaidi kwa ajili ya bima za kilimo;
e) Kumrahisishia mkulima, mfugaji, mvuvi na mazao ya misitu kupata huduma ya Bima;
f) Kurahisisha ulipaji wa madai ya mkulima mara janga linapotokea;
g) Kuweka mfumo mzuri wa ushirikiano kati ya Serikali na kampuni za bima katika kumsaidia mkulima kwenye ulipaji wa ada ya Bima;
h) Kuongezeka kwa imani kwa mkulima kuhusiana na umuhimu na matumizi ya bima;
i) Kuchochea ukuaji wa sekta ya kilimo na sekta ya bima;
j) Kuvutia uwekezaji kwenye sekta ya kilimo na sekta ya Bima;
k) Jukwaa sahihi la kupambana na athari na mabadiliko ya tabia nchi;
l) Kukinga mtikisiko kwenye mnyororo wa thamani wa kilimo
(agricultural value chain-AVC) unaojumuisha uzalishaji, uvunaji, uhifadhi, usafirishaji, uongezaji thamani na soko la uhakika;

m) Kuvutia mabenki kukopesha wakulima, wafugaji na wavuvi;
n) Kuongeza ajira kwa Watanzania;
4.2 Uanzishaji wa Konsotia ya Bima ya Mafuta na Gesi Tanzania
i. Konsotia ya Bima ya Mafuta na Gesi ilizinduliwa tarehe 16 Novemba 2022 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha- Mhe. Hamad H. Chande.
ii. Vihatarishi vyote vya nishati vinavyotoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama vile vihatarishi kutoka kwa mradi wa LNG vitakatiwa bima kupitia Konsotia ya bima ya nishati ya mafuta na gesi Tanzania 

iii. Mantiki ya kuanzisha konsotia ni:
a) Kuhakikisha miradi yote ya gesi na mafuta inabakiza sio chini ya asilimia 45 ada zitokanazo na gesi na mafuta;
b) Kufuatia kutokuwa na uwezo wa soko la ndani, vihatarishi vya nishati, vilielekezwa nje ya Nchi kwa asilimia 100. Jambo ambalo sio na lisilo na tija kwenye uchumi wa nchi;
c) Aidha, kuanzishwa kwa miradi mikubwa ya nishati kama vile
bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) ni fursa
kwenye sekta ya bima kujipanga kwa ajili ya kuongeza tija, uchumi na ajira nchini.
iv. Malengo ya kuanzisha konsotia ni:
a) Kutoa fursa kampuni za bima za ndani kushiriki na kuandika
vihatarishi vya nishati ya Gesi na Mafuta ndani ya nchi;
b) Kushiriki katika bima ya mradi wa LNG, unaokadiriwa kuwa na gharama ya uwekezaji wa Dola za Kimarekani Shilingi Bilioni 40.
v. Hali ya Utekelezaji wa Konsotia hadi sasa:
a) Kampuni 22 za Bima zimesaini Mkataba wa Muungano huo wa Bima ya Nishati ya Mafuta na Gesi Tanzania zenye jumla ya laini (hisa) 238;
b) Kila laini (hisa) ina thamani ya Dola za Kimarekani (USD) 25,000 ambayo ni jumla ya uwezo wa muungano wa kiasi cha mtaji cha USD 6,000,000;
c) Konsotia itasimamiwa na kampuni ya bima Mtawanyo ya
Tanzania Reinsurance Company Limited (Tan Re);
d) Kampuni ya Bima ya Phoenix ya Tanzania ni kampuni Kiongozi (leader) wa konsotia;
e) Kamati ya Kiufundi ya Konsotia imeundwa na wanachama
kutoka makampuni 10 ya bima (yaani Phoenix, Shirika la Bima
la Taifa (NIC), Jubilee, Britam, Heritage, Reliance, UAP, Alliance Insurance Corporation, Tanzania, na Shirika la Bima la Taifa (ZIC);
f) Wajumbe wa kamati wana idadi ya laini (hisa) kuanzia 5 mpaka 95 katika muungano wao.
vi. Faida za moja kwa moja za Konsotia kwa Nchi yetu:
a) Kuhakikisha miradi yote ya gesi na mafuta inabakiza sio chini ya asilimia 45 ada zitokanazo na gesi na mafuta.
b) Kuongezeka kwa malipo ya jumla ya bima ya kila mwaka na
kamisheni za faida;
c) Kuongezeka kwa uwezo wa kiufundi wa ndani na utaalam katika uandikishaji wa vihatarishi vya bima ya nishati ya mafuta na gesi katika soko la bima;
d) Ufikiaji ulioboreshwa wa usaidizi maalum wa usimamizi wa
vihatarishi na hatua zilizoimarishwa za usalama na kuzuia hasara;
e) Kuimarishwa kwa usimamizi wa vihatarishi na ulinzi wa mali na uendeshaji wa watoa huduma;
f) Kuongezeka kwa uwezo wa kifedha kugharamia sekta ya nishati;
g) Ukuaji wa huduma za bima;
h) Kuongezeka kwa mchango wa bima katika Pato la Taifa;
i) Kuongezeka kwa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja katika sekta ya bima ya nishati ya mafuta na gesi. (mradi wa LNG nk).


4.3 Marekebisho ya sheria ya Bima na Kanuni zake.
▪ Katika mwaka huu wa fedha wa 2023/24 Mamlaka imeanzisha mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi ili kuifanyia marekebisho sheria ya Bima na Kanuni zake.
▪ Mchakato huu umeanzishwa kufuatia maboresho ya mifumo ya usimamizi wa Bima na maendeleo ya soko la bima nchini.


5.0 MIPANGO IJAYO YA MAMLAKA HADI MWAKA 2025/26
TIRA kwa kushirikiana na wadau wa Bima inaendelea na utekelezaji wa Mipango na mikakati ya Taifa ambayo ni pamoja na Mpango wa Miaka Mitano wa Maendeleo ya Taifa (FYDPII-2020-2025) , Mpango Mkuu wa Taifa wa kuendeleza Sekta ya Fedha Nchini (FSDMP 2020-2030), Ilani ya Chama cha Mapinduzi (2020-2025), Sera ya Uchumi wa Buluu Zanzibar, Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh. Dkt.Samia Suluhu Hassan wakati akilihutubia Bunge mwezi April 2021, maelekezo ya Mh. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za Bima Septemba 2022 na Maelekezo ya Spika wa Bunge la Jumhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Novemba 2022 wakati wa semina ya Elimu ya Bima na Usalama Barabarani kwa Waheshimiwa Wabunge. Baadhi ya mipango ijayo ya Mamlaka ni pamoja na:


5.0 Kuanzisha na kutekeleza Mpango wa kitaifa wa Bima ya Kilimo (Tanzania Agriculture Insurance Scheme);
5.1 Uanzishwaji wa bodi ya wataalamu wa Bima, Hifadhi ya Jamii na Takwimu Bima;


5.2 Kuunganisha mifumo ya kidigitali na Taasisi mbalimbali za umma ikiwa ni pamoja na Jeshi la Polisi, LATRA, NIDA, TASAC, TRA, PTA, ZRA.


Lengo ni kuongeza usimamizi na maendeleo ya soko la Bima;
5.3 Kuendelea na utoaji wa elimu ya bima kwa umma na wadau mbalimbali.


Kwa mfano Mamlaka imeandaa Semina ya Pili ya Makatibu Wakuu wote Nchini kwa lengo la kutoa elimu ya umuhimu wa ukataji bima. Semina imepangwa kufanyika tarehe 27 Oktoba 2023.


5.4 Kufungua ofisi za Bima Mtawanyo za Kikanda ambazo Serikali ya Tanzania inamiliki hisa za moja kwa moja au kupitia Taasisi zake ili kampuni hizo ziweze kufungua ofisi nchini kwa utaratibu wa Mikataba ya Uenyeji (Hosting Agreements).


5.5 Kuendelea kukusanya maoni ya wananchi kwa lengo la kuhuisha Sheria ya Bima Sura 394.


6.0 PONGEZI NA SHUKURANI
i. Naomba kumpongeze na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa
uongozi bora na kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji ikiwa ni pamoja na kwenye sekta ya bima.
ii. Pongezi zingine zimfikie Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa melekezo yake na kwa ushirikiano wake.
iii. Aidha, pongezi ziwaendee waandaaji wa mkutano huu ambao ni:
Ofisi ya Msajili wa Hazina (TR) pamoja na nyie Waandishi wa Habari kwa kuweza kufanikisha wazo hili la upelekaji wa taarifa na elimu ya Bima kwa umma.


7.0 HITIMISHO
Mamlaka kwa kushirikiana na Bodi ya Taifa ya Bima itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwenye Sekta ya Bima kwa ajili ya kuendeleza na kusimamia soko la Bima kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.


Mamlaka inapenda kuona soko la Bima lisilokuwa na udanganyifu, lenye ushindani, soko linalofuata uweledi na soko lenye kuleta faida.


Baada ya kusema hayo, napenda kuwaalika wandishi wote wa habari kuendeleza sekta ya bima kwa kuitangaza mara kwa mara na kufuatilia matukio mbalimbali yanayoendelea kwenye soko la bima.


Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
....................................................
DKT. BAGHAYO A. SAQWARE
KAMISHNA WA BIMA

============================

HABARI PICHA👇

Kamishna wa Bima Dk. Baghayo Saqware akizungumza na Wahariri katika Mkutano uliofanyika jana, Septemba 18, 2023, Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kulia ni  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Deodatus Nalile na Eric Mkuti, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano Ofisi ya Msajili wa Hazina.Kamishna wa Bima Dk. Baghayo Saqware akipongezwa na Eric Mkuti, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano Ofisi ya Msajili wa Hazina, baada ya kuzungumza na Wahariri katika Mkutano uliofanyika jana, Septemba 18, 2023, Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam. Kulia ni  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Deodatus Nalile. 
Afisa Uhusiano na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri, akizungumza utangulizi na baadaye kumkaribisha Kamishna wa Bima Dk. Baghayo Saqware kuzungumza katika mkutano huo.
Baadhi ya Wahariri waliohudhuria Mkutano huo.
Baadhi ya Wahariri waliohudhuria Mkutano huo.

Afisa Uhusiano na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri, akitoa nafasi ya Wahariri kuuliza maswali au kutoa ushauri baada ya Kamishna wa Bima Dk. Baghayo Saqware kuzungumza.

Baadhi ya Wahariri wakiuliza maswali na wengine kutoa ushauri👇

Kamishna wa Bima Dk. Baghayo Saqware akikusanya dondoo za maswali aliyokuwa akiulizwa na wahariri kwenye mkutano huo. Kulia ni Eric Mkuti, Mkuu wa Kitengo cha Habari, Mawasiliano na Uhusiano Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Kamishna wa Bima Dk. Baghayo Saqware akijibu maswali aliyoulizwa na wahariri kwenye mkutano huo.

Kamishna wa Bima Dk. Baghayo Saqware akijibu maswali aliyoulizwa na wahariri kwenye mkutano huo.

Naibu Kamishna Khadija Said kutoka Zanzibar, akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mwenyekiti Jukwaa la wahariru Deodatus Balile akitoa neno la shukurani kwa Msajili wa Hazina kuandaa mkutano huo na pia kwa Kamishna wa Bima kuwasilisha vema taarifa ya utendaji wa TIRA katika Mkutano huo.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano Ofisi ya Msajili wa Hazina Sabato Kosuri, akifunga mkutano huo na kuwashukuru Wahariri kwa ushiriki mwema.
Eric na Balile wakionekana kuridhishwa na namna mkutano ulivyofanyika kwa ufanisi.

ENDS!

 ©Sept. 2023 Official CCM Blog/Bashir Nkoromo

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana