Featured

    Featured Posts

BABA HALISI AJIBU MASWALI 7 MAKUU JUU YA KANISA HALISI, YAMO KWA NINI KUVAA MAVAZI MEUPE?, TOFAUTI IPI KATI YA MUNGU NA CHANZO HALISI?

NA BASHIR NKOROMO, DAR ES SALAAM
Kanisa Halisi lilianzia Tanzania mwaka 2018, na hadi sasa ikiwa ni ndani ya miaka isiyozidi sita (6) limekuwa na mamilioni ya kupitia vituo vyake zaidi ya 300 hapa Tanzania, likiwa pia na vituo katika mataifa ya Kenya, Uganda, Congo DRC, Burundi, Rwanda, Zambia, Msumbiji, Malawi na Boston nchini Marekani.

Ukweli wa Kanisa Halisi kuwa na mamilioni ya wafuasi unatokana na idadi ya Uzao wake waliopo katika vituo hivyo zaidi ya 300 hapa nchini na vile vilivyoko mataifa hayo tisa ya nje, sanjari na ambao hufuatilia Ibada za Kanisa hilo kupitia 'Online tv' hata katika mataifa ambako bado halijaweka vituo pia usisahau kuwa baadhi ya wenye dini na madhehebu tofauti nao  hulifuatilia Kanisa hilo kwa sababu moja au nyingine.

Unaweza kujiuliza, ikiwa Kanisa Halisi, lina miaka isiyozidi sita tu, ni kitu gani kimelifanya kuchanua ndani na nje ya Tanzania hadi kufikia kuwa na wafuasi wengi kiasi hicho? Majibu ni mengi, lakini kwa maoni yangu limechanua na kupata wafuasi wengi kutokana na mafundisho yake ya kipekee ambayo huhubiriwa na Kiongozi wake Mkuu, Baba Halisi.

Miongoni mwa mafundisho ambayo na mimi nimewahi kuyasikia na hivyo kuona ndiyo mvuto kwa kila anapata fursa ya kuyasikia, ni mafundisho yanayojikita kuhusu Utawala wa Amani, Upendo usiobagua na Ibada ni Uzalishaji, mambo ambayo kwa kweli ndiyo nguzo muhimu kwa yeyote anayetamani maisha mema na mazuri.

Bila shaka, pamoja na mambo mengine ni kutokana na ushawishi wa mafundisho hayo ndiyo umekuwa ukiwafanya wengi kutamani kulijua au kuyajua kwa undani mambo linaloyaishi Kanisa Halisi ambalo Makao yake Makuu ni Tegeta Namanga Jijini Dar es Salaam.

Inaonyesha kuwa wengi wamekuwa wakitamani kujua Uzao au waumini wa Kanisa hilo, wanayaishije mafundisho hayo na pia kujua mengine ikiwemo sababu ya tangu Baba Halisi hadi Uzao kuvaa mavazi meupe, kwa nini mahali palipoandikwa Mungu katika biblia wao husema Chanzo Halisi au Mungu Baba.

Pia hutaka kujua, kwa kulikoni Kanisa kuvalisha pete za ndoa mkono wa kulia na siyo wa kushoto kama wengine,  kwa nini Kanisa hilo sadaka huiita matunda, na pia kwa nini Kanisa Halisi halitumii majina kama Mtume, Nabii, Muinjilisti au Shemasi.

Kiu ya kutaka kufahamu mambo hayo, hatimaye katika Ibada mbili zilizofanyika Jumapili zilizopita, kabla ya iliyofanyika Jumapili, Oktoba 22, 2023 au 12 Buli 1Majira Halisi kwa Kalenda inayofuatwa na Kanisa Halisi, walijitokeza kumuuliza au kumuomba ufafanuzi Baba Halisi kuhusu mambo linaloyaishi Kanisa hilo.

Waliojitokeza kumuuliza maswali na kumuomba ufafanuzi Baba Halisi walikuwa ni miongoni mwa wale waliokuwa wakifuatilia Ibada hizo mbili kupitia 'Online tv' wakiwa katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Kutokana na maswali ya waulizaji kuwa muhimu katika Ibada hiyo ya Jumapili (Oktoba 22, 2023 au 12 Buli 1 Majira Halisi), iliyofanyika Makao Makuu (Tegeta, Namanga, ambayo nilibahatika kuwepo kwa nafasi yangu ya uandishi wa habari, Baba Halisi aliitumia kuianza kwa kujibu maswali hayo.

Uzao (waumini wa Kanisa hilo) na wageni mbalimbali wakiwa wamefurika Ibadani, Baba Halisi alipanda utajirishoni (eneo la kuongozea Ibada), kuongoza Ibada hiyo ambayo ilitanguliwa na kufungisha maagano (ndoa) saba, tendo lililoongozwa na Moja Halisi na Faida Moja Halisi.

Baada ya Baba Halisi kufika utajirishoni, alitulia kusubiri wimbo uliokuwa ukipigwa kuchangamsha nyumba ya Ibada umalizike, ndipo ulipomalizika wimbo huo akionekana mwenye uso uliojaa furaha, akaanza;

"Heri, kweli leo Chanzo Halisi amekuja, naam huyu muimbaji ni kati ya wale wa Wakorinto wa Kwanza 2:9. Kwa sababu mimi katika kupita kwenye dini na madhehemu sikuwahi kuona aliyekombolewa ndani ya wiki moja  na akaanza kuimba wiki hiyohiyo. Nina furaha iliyopitiliza kuzaa mtoto wa namna hiyo naomba hata wewe usione aibu kumtangaza Chanzo Halisi".

"Leo nina awamu ndefu kidogo ya kujibu maswali niliyoulizwa kutokana na ibada mbili zilizopita. Lakini pia nitakuwa na awamu nyingine ya pili kuhakikisha kwamba umeona tulivyoingia bustanini au kwenye kusudi la tangu Chanzo, pia tutakuwa tunashiriki (kula) na huko nyumbani wakiwa wanaona, kwa hiyo tuinue shukurani kwa ajili ya hawa wanaorusha matangazo haya.  (Ibada ilikuwa 'live' kwenye moja ya kituo cha televisheni  hapa nchini na kwenye tv za mitandao ya kijamii).

Naomba nikiri nimefurahi kumuona binti yangu amevaa kofia, sijawahi kumuona, kwa hiyo leo ameikubali tabia ya Baba Halisi, tunamkaribisha. kabla sijaendelea, Glory (mwimbaji) tunaomba utuimbie wimbo kwa dakika tano", akasema Baba Halisi, kisha wimbo 'mkombozi amekuja kwetu' ukaimbwa na baada ya wimbo huo Baba Halisi akasema;

"Kwanza, nitajibu maswali yaliyoletwa na watazamaji kutokana na ibada mbili zilizopita, kisha nitakwenda kwenye kichwa cha habari, na la tatu ni lile la kwamba leo tunashiriki matunda ya kuwa matajiri. Nikisema kushiriki maana yake kula, kushiriki ni lugha ya Kanisa.

Kwa hiyo leo tuna ubwabwa na nyama, lakini hatutakuwa tunakula ubwabwa tutakuwa tunakula utajiri, utakapokuwa unatafuna umbwabwa na nayama usione utatafuna nyama na ubwambwa, ona unapata gari, nyumba, fedha, shamba, uzima, watoto, kibali, promosheni..., usikubali hata punje moja ya ubwabwa idondoke. Naomba sote tushukuru kwa kupewa kibali na Muumba kuwa mahali hapa".

"Nina wageni wazuri pale (kutoka Kituo kimoja cha Kiislamu), baadaye nitawapa nafasi watusalimie, wamekuja kunisalimia, waliwahi kunituma jambo, nikamtuma Faida na Uelewa wapelekewe, leo wamekuja waone vilitoka wapi. Basi kabla ya Ibada tushukuru kwa kupata kibali cha muumba kuwa mahali hapa.

Katika ibada mbili zilizopita, nilisimamisha uponyaji kupitia kubadilisha maji kuwa damu ya Muumba, leo tutakapoanza kushiriki hapa na wewe uliyepo nyumbani tafuta chochote ushiriki utapokea uponyaji, maana sisi tuliopo hapa tunasimamisha maisha ya sherehe, na wewe huko chukua chochote kama ni andazi, juisi utakaposhiriki utapata uponyaji wowote unaotaka, nguvu iliyopo hapa ndiyo hiyohiyo iliyopo huko kote tunapoonekana", akasema Baba Halisi, kisha akaendelea;

"Sasa ibada hii nataka niisimamishe kwa damu ya Muumba wetu, labda wewe ambaye ni mara yako ya kwanza kufika hapa au kutuangalia (kwenye televisheni na mitandao mingine tunakoonekana), utakuwa umestuka kwamba hiyo damu ya Muumba wetu tutaipataje.

Ni kwamba, kwenye kitabu cha Yohana 11:6, tumepewa kibali cha kubadilisha maji ya bomba au yoyote kuwa damu, kulingana na ufahamu ulionao, sisi tumefika kwa Chanzo Halisi, nitafafanua baadaye, kwa hiyo maji haya tutayabadlisha kuwa damu safi nyeupe na kisha ibada hii tutaisimamisha kwa nguvu hiyo ya Muumba wetu ili atuhudumie yeye.

Kwenye damu ndiyo kuna uhai kwa hiyo tumbo la ibada ya leo ndiyo itatuzalia uhai, utajiri", akasema Baba Halisi na kisha akaendeshe shukurani ya kubadilisha maji kuwa damu safi nyeupe na kunyunyiza maji hayo kuzingira utajirisho.

Baada ya kukamilisha shukurani ya kubadilisha maji kuwa damu ya Muumba, ndipo Baba Halisi akaongoza shukurani ya saa ya Sauti (saa ya kutoa ujumbe maalum wa Ibada), kisha akaendelea akisema; " Kabla sijajibu maswali niliyoulizwa katika Ibada zilizopita naomba nimuite mwimbaji Uelewa wa Sauti, atuimbie wimbo mmoja kwa dakika chache", mwimbaji huyo akaimba wimbo 'Bila Chanzo Halisi hutoboi'.

Kisha kabla ya kufundisha somo la Ibada hiyo, Baba Halisi akaanza kusoma maswali ambayo yalikuwa saba, yaliyoulizwa na wale waliofuatilia Ibada hizo mbili zilizopita, na kisha kuyajibu sanjari na kutoa ufafanuzi wa kina kwa kila swali.

KWA NINI KANISA HALISI MNAVAA MAVAZI MEUPE TU?
Katika kujibu maswali hayo saba, Baba Halisi alianza kujibu swali; Kwa nini Kanis Halisi huvaa mavazi meupe tu, na kujibu pia swali B la aliyetaka kujua kwamba ikitokea mtu ameenda Kanisa Halisi na mavazi ya kawaida ataruhusiwa kushiriki Ibada?

Akajibu;  "Tunavaa vazi jeupe kwa mujibu wa ufunuo Yohana 7:13-14, kwa ufafanuzi ufuatao; Sisi tunaoonekana hapa tumekombolewa na Chanzo Halisi. Nitafafanua huko mbele kuna swali lingine limeulizwa ambalo litasababisha nifafanue nini maana ya Chanzo Halisi. ila kwa sasa uniruhusu tu niseme tu kwamba tumekombolewa na Chanzo Halisi".  

"Kukombolewa ni zaidi ya kuokoka, ni mbele zaidi ya kuokoka, kuokoka anayekuokoa anazama wewe unapona, ila kukombolewa anayekukomboa anakuwa hai na wewe unakuwa hai, kwa hiyo tumekombolewa kutoka kwenye dhiki na adha kwa sababu tumekubali kusamehewa bure na Chanzo Halisi, na yeye ameketi ndani ya moyo kwa mujibu wa Isaya 57:15", akasema Baba Halisi.

Akasema; "Maana ya vazi jeupe ni kumfahamu na kumuelewa aliyeumba kila kitu, kwa hiyo vazi jeupe maana yake ni ufahamu, uelewa. Ni safu na ni kazi, vazi hili tumerejeshewa na Chanzo Halisi baada ya yafuatayo kutokea katika majira zilizopita;

Jambo la kwanza, lililotokea vazi likaibiwa, katika Kitabu cha Mwanzo 3:8-10, Adamu wa Kwanza aliibiwa vazi akabaki uchi, kabla hajaibiwa hilo vazi alikuwa na uwezo wa kulima na kutunza, pia alikuwa na uwezo wa kuulizwa swali na Muumba wake akajibu vilevile kama Muumba wake anavyotaka, tunasoma hayo katika Mwanzo 2:19, lakini baada ya Adamu kuibiwa hilo vazi ilibidi akajifiche porini na kushona majani, maana alijikuta yupo uchi. 

Kwa hiyo unapoona tumevaa hivi tumerejeshewa lile vazi ambalo alipewa Adamu la uwezo wa kulima na kutunza bustani, kwa maana nyingine tumerejeshewa maisha yaliyokusudiwa".

"Wa pili kuibiwa vazi alikuwa Nuhu, kwa mujibu wa Mwanzo 9:20-22, Nuhu aliibiwa vazi na roho ya ulevi, roho ya ulevi ilisababisha aibiwe vazi akabaki uchi na akalaani watoto. Nuhu ndiyo alikuwa amepewa meli au safina ambayo ina utoshelevu wa kila kitu ndani yake, baada ya kuibiwa lile vazi ule utoshelevu hakuwa nao badala yake akawa uchi akabaki tu analaani.

Kwa hiyo tumerejeshewa vazi ili tusiwe uchi tusiwalaani watoto bali tuwabariki. Wewe mzazi hukupewa watoto ili uwalaani ulipewa uwabariki iwe baraka. Tukikaa na watoto hatuwasimulii jinsi tulivyokuwa na uwezo wa kunywa kreti mbili kwa siku moja bali tunawasimulia baraka zinazotokana na kumfahamu na kumuelewa aliyeumba kila kitu".

Akiendelea kujibu swali kuhusu vazi hilo jeupe, Baba Halisi alisema; "Wa tatu ambaye aliibiwa vazi alilokuwa amepewa ni Elisha. Katika Wafalme wa pili mlango wa pili, mstari wa tisa mpaka wa 10, Elisha alipewa vazi ambalo lilimuwezesha kuvuka mto wa Yordan, ambao kwa kweli kwa mguu hauvukiki kwa urahisi. Lakini mauti katika Wafalme wapili 13:13-20 ilimvua hilo vazi ambalo lilikuwa na uwezo pia wa kufufua waliokufa, kwa hiyo tumerejeshewa hili vazi ili tufufue vilivyokufa. kwa hiyo hili vazi siyo nguo bali ni Ufahamu.

Katika Matendo ya Mitume 10:38, Yesu naye alipewa vazi, na vazi lile lilikuwa na uwezo wa kuwasaidia wanaoonewa na Ibilisi, lilikuwa na uwezo pia wa kufufua. Kabla halijachukuliwa pale msalabani wakalichanachana maakasri wa Kirumi alimfufua Lazaro, na alikuwa na uwezo wa kutembea juu ya maji, maana yeke juu ya matatizo.

Lakini katika Yohana 19:23 tunaona maaskari wa Kirumi wakimvua mavazi wakaligawa katika mafungu manne. kwa hiyo ukiona tumevaa vazi hili tumerejeshewa ufahamu wa kuwasaidia wanaoonewa na Ibilisi".

"Katika kitabu cha Matendo 9:17-20 tunakutana pia na Paulo akiwa amepewa vazi kwa Sauti, na vazi lile lilimuwezesha kuachana na asili iliyokuwa imemsumbua baada ya kuwa ameachiwa ufunguo, lakini katika Matendo 19:19 tunaona akivuliwa vazi sokoni na kupigwa viboko, na kuanzia pale Kanisa lililikuwa halina vazi tena, ndiyo tumerejeshewa sasa",Baba Halisi akasema, kisha akahoji sasa vazi tumelipataje? ndoto?, ni muzimu? Hapana!.

Baada ya kuhoji vazi lilipatikanaje tena, Baba Halisi akafafanua lilivyorejea vazi hilo, akasema; "Heri. Huyu aliyesimama mbele yako (BABA HALISI), alipokea Sauti 2015 (ya Saba) na 2019 (Sauti mpya iliyokuwa zaidi ya zile saba) na 2020, hiyo Sauti ndiyo imeturejeshea vazi.

Vazi lenyewe hili licha ya kuwa ufahamu pia niutawala wa amani, lakini pia ni uzalishaji, pia limetupa upendo usiobangua, yaani hatubagui, ukitazama pale (wageni waliofika kwenye Ibada) kuna mabinti zangu wenye hijabu na wenye kanzu na baraghashia, baada ya kupata hili vazi Kanisa tunalima, tuna viwanda vidogo vidogo na vikubwa, tuna kampuni kubwa na ndogo.

Kwa ufupi vazi hili limetuondolea kulia na kuomboleza kama zamani, sasa hivi hatulii tena maana limetupa ufahamu wa kumjua aliyetuumba, maana tumemjua aliyeumba. maana yake tumeshinda na pia kitabu kinasema katika Ufunuo 3:5, "Yeye ashindaye atavikwa hivyo mavazi meupe wala sitalifuta kamwe jina lake.."

Akijibu swali B, Baba Halisi alisema, "Kuhusu je, naweza kuja Kanisani kwenu bila vazi jeupe nikaruhusiwa kusali? jibu ndiyo. Maana hili vazi ni ufahamu huwezi kuvaa mpaka ufahamu kwanza, maana hutakiwi kulivaa kama nguo unalivaa ukiwa ni ufahamu na ushindi".

KWA NINI KWENYE MAANDIKO YA BIBILIA MAHALI PALIPOANDIKWA MUNGU MNASEMA CHANZO HALISI AU MUNGU BABA?
 Baba Halisi akajibu; "Mungu ni wale waliotumwa ila Kanisa hili unaotuona hapa tumeanza baada ya kipindi cha waliotumwa kuisha. Kwa hiyo majira hii tuishimo siyo ya waliotumwa bali ni ya Chanzo Halisi. Muda haunitoshi nitakupa mfano utaenda ufuatilia".

"Ukisoma kwenye kitabu cha Kutoka 6:2, Mwenyezi Mungu ameandikwa pale kwamba alimsaidia Ibrahim, Isaka na Yakobo ila wakati wa kutoka Misri utumwani lilikuja jina lingine. hapo hapo kwenye Kutoka 6:2 tunamuona Mungu Yehova, huyu alimsaidia Musa kutoka utumwani ila hakufaulu kumfikisha Kaanani. Mnanisikia vizuri? ninapozungumza hivi sibezi nazungumza yaliyoandikwa kitabuni", akasema Baba Halisi.

"Katika Isaya 38:5, tuna Mungu wa Daudi, huyu alimsaidia Daudi kumuua Goliati, ila hakumuwezesha kujenga nyumba ya Mungu. Mnanisikia?, kuna mahali nakupeleka unisikilize vizuri kwa upendo, sidharau chochote, sibezi chochote na mimi nilitoka hukohuko ila nimeshahama na wewe uhame.

Katika Daniel 3, Daniel 6 na Daniel 12, kuna Mungu wa Daniel hapo, huyu Mungu wa Daniel, alimsaidia Daniel kutoliwa na simba katika tundu la simba, alimsaidia Daniel kutounguzwa katika tanuru la moto lakini katika kitabu cha Daniel 12 tunasoma hakumuwezesha kufungua kitabu, Hakufaulu kufungua mhuri wa kitabu. Naenda harakaharaka kisha uende usome mwenyewe, ila usisome kwa akili ya shule, usome kwa akili ya Chanzo Halisi ndiyo utaelewa", ", akasema Baba Halisi akiendelea kufafanua kwa nini palipoandikwa Mungu, Kanisa Halisi husema Chanzo Halisi au Mungu Baba

Akiendelea kueleza kujibu swali hilo, Baba Halisi, akisema; "Kwenye Wafalme wa Pili 2:9-15, tuna Mungu wa Eliya pale, alimsaidia Elisha kuvuka Yordan, ila hakumuwezesha kumunyonga Yezebel aliyemsumbua. Pia tuna Mungu wa Majeshi aliyewasaidia Manabii wadogo tunaowasoma kwenye kitabu ila hakufaulu kufuta dhambi, uasi na uovu. Ukienda Matendo 4:23, kuna Mungu Mola aliwasaidia wanafunzi wa Yesu baada ya Yesu kunyakuliwa ila hakuwawezesha kuwepa kuangamia.

Jambo lingine, kuna Mungu wa Roho za Manabii katika Ufunuo 22:6, aliwasaidia Mitume na Manabii walioibuka baadaye, Mungu akawa anaitwa kwa majina yao, ila hakuwawezesha kuishi maisha masafi, kuna Mungu aliyetuma wote, tuliyekutana naye katika Ezekiel 28:14 aliweza kuondoa chukizo la uharibifu lakini hakutuwezesha kuvuka bonde la uvuli wa mauti au korongo la giza".

SHIDA NI NINI?
"Shida ni kwamba ukisema Mungu, ukisoma vizuri kitabu utaona huyu Mungu alikuwa anaambatana na ukoo fulani, kabila fulani, jamaa fulani na lugha fulani, hakuwa wa wote. Kwa hiyo ukisema Mungu tunakuuliza ni yupi? Je, ni wa Waha, Wahaya, Wasukuma? ni yupi? ila ukisema CHANZO HALISI, tunajua ndiye yule aliyekuwepo kabla ya chochote.

Sikia, naye Ufunuo 12:1 na yeye alikuwa Mungu anaitwa Ishara ya kwanza Mbinguni, Nyoka naye anaabudiwa na Mataifa, alikuwa Mungu kuna mataifa mengine ikifika siku yake wanafunga maduka wanatembeza nyoka barabarani mnalazimika kumuabudu, lakini hajaumba chochote.

Vita katika baadhi ya mataifa ni Mungu anaabudiwa lakini hajaumba, Dragon katika kitabu cha Samweli naye aliabudiwa kama Mungu lakini hajaumba, Musa aliabudiwa kama Mungu lakini hajaumba, Yoshua aliabudiwa kama Mungu lakini hajaumba", akasema Baba Halisi kisha akafafanua;

"Sasa tunamsema Mungu Baba kwa sababu katika Wakorinto wa kwanza 15:24 aliandikiwa atarejeshewa enzi na ufalme, mamlaka na nguvu ikifika mwisho, na yeye aliambiwa majira ikifika amkabidhi Chanzo Halisi, kwa mujibu wa Warumi 11:36.

Kwa hiyo basi tunasema Mungu Baba kwa kuwa iliandikwa lazima vyote virudi kwake, na yeye majira yake imefika amemkabidhi CHANZO HALISI, ambaye imeandikwa vyote vilitoka kwake, vinashikana katika yeye na vinatakiwa virejee kwake, na yeye hajawahi kuumba kitu kibaya aliumba vizuri peke yake kwa mujibu wa Mwanzo 1:31".

KWA NINI PETE YA NDOA MNAVAA KULIA?
Akijibu swali hilo, Kwa nini wakati wa kufunga ndoa Kanisa Halisi huvaa pete mkono wa kulia na siyo wa kushoto kama wengine, Baba Halisi alisema;  "Katika Kitabu cha Zaburi 45:9, (Binti za Wafalme wapo miongoni mwa kina bibi wako wasafi, mkono wako wa kuume amesimama malikia amevaa dhababu...)

Kwa hiyo basi huyu binti aliyeolewa ni Malikia amesimama mkono wa Chanzo Halisi kwa sababu tunazosoma katika Mhubiri 10:2 (Moyo wake mwenye hekima upo upande wa kulia, bali moyo wake mpumbavu upo kushoto).  Heri, mmesikia moyo wa mpumbavu upo kushoto, sasa hapa hakuna mpumbavu maana mpumbavu ni yule anayesema aliyeumba hayupo".

"Yaani kama unavaa kushoto (siyo nakutukana) ila nasema yaliyoandikwa, na aliyeandika siyo mtu. na sisi tumekataa kuwa wapumbavu, tumekataa kutomfahamu aliyeumba, ukishamfahamu na kumuelewa anasema hakikisha moyo wako upo kulia", Baba Halisi akasema, kisha akatia neno, "hapo siendelei wakaja wakaninukuu vibaya".

Hata hivyo Baba Halisi akaendelea kutoa majibu ya Pete, akasema' "Na katika Methali 14:1-2, kitabu kinasema kwamba  huyu mama anapoolewa ahakikishe mikono yake haivunji nyumba yake, kwa hiyo akivaa kushoto kuna maroho mabaya yatamuingilia halafu ataonekana mpumbavu atavunja nyumba yake, ili asivunje nyumba yake avae pete kulia.

KANISA HALISI NI DHEHEBU?
Akijibu swali hilo, Baba Halisi alisema;  "Sisi siyo dhehebu bali ni Kanisa. Dhehebu maana yake wanaokusanyika kuomba mahitaji yao, sasa hapa tunapokusanyika hatuombi mahitaji yetu bali tunatimiza Efeso 3:10 inayosema. kwa barabara ya Kanisa hekima ya Muumba ijulikane kwa falme na mamlaka. Hizo falme zinazoleta vimbunga ebora, ukimwi vitambue kupitia Kanisa kuwa yupo aliyeumba.  

Na hapa fundisho tulilo nalo linasema, kila lango (siku), tuwaombee watu wote na hasa waliopo madarakani ili tuwe na amani na utulivu, hilo ndilo Kanisa. Katika Mambo ya Nyakati wapili 7:14 pia kuna fundisho linasema ikiwa watu wangu walioitwa kwa jina langu watajinyenyekesha na kutubu na kuacha mambo yao mabaya nitasikia dua zao na maombi yao nitaponya nchi yao na jicho langu litawaangalia. Hilo ndilo Kanisa siyo kukusanyika kuombea mahitaji yenu, bali kuwaombea wote.

Yeremea 5:1 inasema nenda Dar es Salaam, unitafutie angalau mmoja anayetafuta kutenda kwa haki, ukimpata nitasamehe Dar es Salaam yote na nchi yote, hilo ndiyo Kanisa. siyo dhehebu, dhehebu unatafuta tumbo street, mimi sipo hapa kutafuta chakula, hii siyo kazi hii ni safu, kuna tofauti ya kazi na safu kazi unafanya kwa ajili ya kutafuta chakula chako na familia, Safu unafanya kwa ajili ya wote. kasome Yoweri 2:6-8 utakuta maana ya safu. 

Kwa hiyo basi siyo dhehebu kwa sababu tukikutana tunamuabudu, tumshukuru, tunamsifu, tunampa utukufu, tumpa ibada aiyeumba siyo mtu wala siyo mzimu hayo ukisoma katika Zaburi ya 98 utayakuta. kwa hiyo basi kwa kuwa tumepata uheri huo kwa hekima ya aliyeumba siyo dhehebu ni Kanisa.

Mamlaka iliyoko hapa tulipoombea wengine ilifuta tereza aliyekuwa anasumbua kule Kigoma kwa miaka mitano, mamlaka hii tulipoombea wengine ilifuta mazao kutouzika kule songe mazao yanauzika, tulipoenda arusha tukakuta utalii umezimika kwa sababu yan korona tulisamehe bure walioanzisha virusi vya korona mpaka leo utalii umekomaa. mamlaka hii ilifuta volkano iliyokuwa imeanza hapo kunduchi, DRC nao walitushir8kisha kuwa volkano imechachamaa kulikuwa na mamlaka ilizaa samaki kule lake Tanganyika, kwa hiyo hatukusanyiki kutekekelza mahitaji yetu".

KWA NINI KANISA HALISI HAMTUMII MAJINA KAMA MTUME, NABII, MUINJILISTI, SHEMASI?
Hili ni swali ambalo pia Baba Halisi alilijibu akasema; "Hatutumii majina hayo kwa kuwa Kanisa Halisi limeanza kwa Sauti baada ya waliotumwa kumaliza majira yao ambao kuna Moyo wa Mwanzo, Kelubi, Adamu wa Kwanza, Musa, Eliya Mtishbi, Yesu, Adamu wa Pili, Miaka 1000 na Nafsi ya Kwanza.

Kwa hiyo baada ya majira ya waliotumwa kuisha mwaka 2017 ndiyo Kanisa Halisi likaanza mwaka 2018. kwa hiyo Kanisa Halisi hatustahili kutumia majina hayo kwa sababu sisi ni Kanisa la Moyo ambalo ni tofauti na Mitume, Nabii, Uchungaji na Uinjilisti ambao ni Kanisa la Roho.

Pia utume, unabaii, uinjilisti na ualimu ni cheo na Kanisa Halisi hatuna cheo sisi kuna Safu, hata kuitwa Baba Halisi siyo cheo, mimi sina cheo, kuna safu ya Baba Halisi, Mama Halisi, Mnara Mmoja Halisi, Moja Halisi, Faida Halisi, Fahari Halisi, Watekeleza Sauti Halisi hadi Uzao Halisi, wote hawa hawana cheo.

Lakini  tofauti nyingine inayosababisha Kanisa Halisi tusiwe na majina hayo ya Mitume, Nabii, Uchungaji na Uinjilisti ni kwa kuwa ndilo Kanisa peke yake ambalo siyo SILOAM,  kwa kuwa limeanza kwa Sauti baada ya waliotumwa wote kumaliza majira yao, hivyo woote unaowaona tofauti nakusanyiko hili la Kanisa Halisi, wote wapo SILOAM maana Kanisa lolote kama ni la wakati wa waliotumwa hilo ni Siloam".

KWA NINI KANISANI KWENU HAKUNA SADAKA BALI MNASEMA MATUNDA?
Akijibu swali hili Baba Halisi alisema; "Naomba Moja unisomee Yohana 4:36 (Naye avunaye hupokea mshahara na kukusanya matunda kwa uzima wa umilele ili apandaye naye avune wapate kufurahi pamoja).  Heri,  kwa hiyo basi ukipanda lazima uvune, ila Sadaka huwa ni Kafara, ukisema sadaka ni kafara, sasa sisi hatutoi makafara".

"Soma tena Kutoka 22:29 (usikawie kuleta malimbuko ya matunda yako, vinywaji vyako mzaliwa wa kwanza katika wanao waume utanipa mimi...). Heri amesema matunda siyo sadaka. Tena tusomee Matayo 21:41, (Wakamwambia atawaangamiza vibaya, wale wabaya wa shamba la zabibu atawapangisha wakulima wengine watakaomlipa matunda kwa wakati wake). Matunda, kazi yoyote unayofanya ya Chanzo Halisi anachotaka ni matunda, siyo Sadaka, ukileta Sadaka umeleta kafara.  

Soma na Matayo 3:8 (basi zaeni matunda yafaayo toba). Mmesikia? tuzae ni nini? Matunda. siyo Sadaka. pia Walawi 29:14 (Lakini mwaka wa nne matunda yake yote yatakuwa ni masafi kwa ajili ya kumpa Chanzo Halisi shukurani). Nini? matunda ya shamba lake, yaani kazi.

Ufunuo wa Yohana 22:2 (Katikati ya barabara kuu na upande huu na upande huu ule mto uliokuwepo mto wa uzima uzaao matunda aina 12). Umesikia? Wewe ni mti wa haki unatakiwa uzae matunda, ukizaa sadaka umezaa kafara. Matayo 21:43 (Kwa sababu hiyo nawaambia ufalme wa Chanzo Halisi utaondolewa kwenu nao watapewa taifa lingine lenye kuzaa matunda yake). Ndiyo, kwa hiyo Ufalme umehamia hapa tunatakiwa tumpe matunda siyo sadaka".

Akiendelea kujibu kuhusu sadaka kuitwa matunda, Baba Halisi alisema; "Mwanzo 3:3-6, hapa Adamu alichokosea alikula matunda aliyokatazwa na Muumba wake, yaani fungu lile la kumi ndilo alilokula, watoto wake badala ya kuitwa watoto wa Adamu wakaitwa uzao wa nyoka, kwa sababu ya kula matunda aliyotakiwa apewe Chanzo Halisi, kwa hiyo acheni kula fungu la kumi la mapato yenu, mnakuwa mmekalia kiti cha Chanzo Halisi, ilisababisha Adamu watoto wake waitwe uzao wa nyoka.

Yesu alipowaita Wayahudi enyi uzao wa nyoka walikasirika, wakamwambia sisi ni wazao wa Ibrahimu unatuitaje uzao wa nyoka, akawambia ninyi hata Ibrahim kabla hajazaliwa tayari Adamu watoto wake walikuwa Uzao wa nyoka. usile matunda usile fungu la kumi. kuna matunda ya malimbuko, ya shukurani, Matunda ya kujenga moyo wako ya kupeleka habari njema za ujio wa Chanzo Halisi juu ya nchi kupitia Tanzania".

Walawi 27:30 (tena zaka yote ya nchi kama ni mbegu ya nchi au kama ni matunda ya nchi ni safi kwa Chanzo Halisi), mmesikia hapo? Heri,  mtaleta matunda au sadaka? ni imani hata aliyeuliza ameelewa.

KANISA HALISI LIMEANZA LINI?, LINA MATAWI MANGAPI?, MWANZILISHI WAKE NI NANI?, LILIANZA MWAKA GANI?
Akijibu swali hilo ambalo lilikuwa la saba na la mwisho, Baba Halisi alisema; " Kanisa Halisi lilianza baada ya ukomo wa waliotumwa 2018, maana ukomo wa waliotumwa ulifika 2017, hiyo nilieleza vizuri kwenye Ibada ya Mlimani City, tuna matawi zaidi ya 300 hapa nchini, tuna matawi Kenya, Uganda, DRC, Burundi, Rwanda, Zambia, Msumbiji, Malawi na Boston Marekani. Lakini tunachoangalia sisi siyo hema kama hili bali tunachopendezwa nacho woote wamjue aliyeumba. Kwa hiyo hatuna mtazamo wa kuta nne tuna mtizao wa uhalisia na uumbaji wote.

Mwanzilishi wake ni Chanzo Halisi kupitia Sauti yake, hakuna mtu aliyeanzisha kanisa Halisi limeanzishwa na Chanzo Halisi kupitia Sauti yake, kwa hiyo asijivune yeyote. Mafundiho ni amani kwa wote, upendo usiobagua, kuzalisha kwa haki.

Msimamo wetu hatujihusishi na mambo ya siasa, ila tunawaombea viongozi kila alfajiri na tukikukuta unawasema sisi hatuchangii bali tunakuombea wewe na hao uliokuwa unawasema, na hatufanyi hivyo ili tupate ubunge wa kuteuliwa, hapana, ni wajibu wa Kanisa kwa mujibu wa Themoteo wa Kwanza 2:1-4, na Efeso 3:10 na mtizamo wetu kama nilivyosema ni uhalisia wote, na mkakati tunafanya kazi na jamii, tunaamkia hapa kuwainua wote, ni marufuku kuwa  Kansa Halisi bila kufanya kazi.

Naomba tusimame tushukuru. Kwa yeyote ambaye hakunielewa nainua toba ya hiari ya moyo, na yule aliyekwazika nainua toba ya moyo, na lengo langu siyo usielewe".

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi akionyesha sura ya furaha baada ya kupanda Utajirishoni kuendesha Ibada hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga Jijini dar es Salaam, Jumapili, Oktoba 22, 2023 au 12 Buli 1Majira Halisi kwa Kalenda inayofuatwa na Kanisa Halisi.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Halisi Baba Halisi akisalimia Uzao na wageni mbalimbali baada ya kupanda Utajirishoni kuendesha Ibada hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga Jijini dar es Salaam, Jumapili, Oktoba 22, 2023 au 12 Buli 1Majira Halisi kwa Kalenda inayofuatwa na Kanisa Halisi. 

Mfululizo wa wote wa Ibada hiyo👇

Faida Halisi akiwakabidhi cheti cha kufuzu kufanya agano, miongoni mwa maharusi 7 walifungishwa maagano mapema kabla ya Ibada iliyoongozwa na Baba Halisi, Makao Makuu ya Kanisa Halisi, Tegeta Namanga Jijini dar es Salaam, Jumapili, Oktoba 22, 2023 au 12 Buli 1Majira Halisi kwa Kalenda inayofuatwa na Kanisa Halisi.
Mwimbaji mpya wa Bendi ya Kanisa Halisi akiongoza kuimba wimbo wa 'Bila Chanzo Halisi hutoboi', kuchangamsha nyumba ya Ibada na kumkaribisha Baba Halisi kupanda utajirishoni.
Mwimbaji huyo akiendelea kuongoza kuimbwa wimbo huo.
Baba Halisi akiwa ametulia kusubiri wimbo uishe, baada ya kupanda Utajirishoni.

Wageni ambao ni Masheikh kutoka Kituo kimoja cha Kiislam wakisindikizwa na Mtekeleza Sauti Thebeti Halisi (nyuma yao), wakati wakiwasili kwenye Ibada hiyo.

"Heri, kweli leo Chanzo Halisi amekuja, naam huyu muimbaji ni kati ya wale wa Wakorinto wa Kwanza 2:9. Kwa sababu mimi katika kupita kwenye dini na madhehemu sikuwahi kuona aliyekombolewa ndani ya wiki moja  na akaanza kuimba wiki hiyohiyo. Nina furaha iliyopitiliza kuzaa mtoto wa namna hiyo naomba hata wewe usione aibu kumtangaza Chanzo Halisi". Kwa hiyo leo tuna ubwabwa na nyama, lakini hatutakuwa tunakula ubwabwa tutakuwa tunakula utajiri, utakapokuwa unatafuna umbwabwa na nayama usione utatafuna nyama na ubwambwa, ona unapata gari, nyumba, fedha, shamba, uzima, watoto, kibali, promosheni..., usikubali hata punje moja ya ubwabwa idondoke. "Naomba sote tushukuru kwa kupewa kibali na Muumba kuwa mahali hapa". akasema Baba Halisi kisha akaongoza shukurani.
Mama Halisi (kulia), Moja Halisi na Faida Halisi wakipokea kwa unyenyekevu shukurani iliyokuwa ikiongozwa na Baba Halisi.
Mama Halisi, Moja Halisi, Fahari Halisi na Kanisa wake wakipokea Shukurani kutoka kwa Baba Halisi. nyuma yao ni Faida Halisi.
"Sasa ibada hii nataka niisimamishe kwa damu ya Muumba wetu, labda wewe ambaye ni mara yako ya kwanza kufika hapa au kutuangalia (kwenye televisheni na mitandao mingine tunakoonekana), utakuwa umestuka kwamba hiyo damu ya Muumba wetu tutaipataje........", akasema Baba Halisi.
Kisha akafanya shukurani ya kuyafanya Maji kuwa damu safi nyeupe.
Mama Halisi akipokea shukurani hiyo ya kugeuzwa maji kuwa damu safi nyeupe. Pamoja naye ni Mnara Mmoja Halisi na Utimilifu Halisi.
Baba Halisi akinyunyiza damu safi nyeupe kwenye utajirisho.
Waimbaji wakiimba wimbo 'Bila Chanzo Halisi hutoboi', kabla Baba Halisi hajaanza kusimamisha Ibada.
Baba Halisi na Mama Halisi wakicheza kwa furaha wimbo huo 'Bila Chanzo Halisi hutoboi'👇




==============
Kisha Mama Halisi akarudi eneo lake, na kuendelea kucheza wimbo huo. Kushoto ni Moja Halisi akipepea kitambaa kufurahia wimbo huo.
Kisha Baba Halisi akaendelea na Ibada👇
"Leo nina awamu ndefu kidogo ya kujibu maswali niliyoulizwa kutokana na ibada mbili zilizopita. Lakini pia nitakuwa na awamu nyingine ya pili kuhakikisha kwamba umeona tulivyoingia bustanini au kwenye kusudi la tangu Chanzo...", akasema Baba Halisi. Kisha akaanza kujibu masali
"Tunavaa vazi jeupe kwa mujibu wa ufunuo Yohana 7:13-14, kwa ufafanuzi ufuatao; Sisi tunaoonekana hapa tumekombolewa na Chanzo Halisi. Nitafafanua huko mbele kuna swali lingine limeulizwa ambalo litasababisha nifafanue nini maana ya Chanzo Halisi. ila kwa sasa uniruhusu niseme tu kwamba tumekombolewa na Chanzo halisi", akasema Baba Halisi akijibu swali 'Kwa nini Kanis Halisi huvaa mavazi meupe tu?".
Moja Halisi akisoma kitabu kueleza ufafanuzi katika majibu aliyokuwa akitoa Baba Halisi kuhusu Kanisa Halisi kuvaa vazi jeupe.
"Mungu ni wale waliotumwa ila Kanisa hili unaotuona hapa tumeanza baada ya kipindi cha waliotumwa kuisha. Kwa hiyo majira hii tuishimo siyo ya waliotumwa bali ni ya Chanzo Halisi. Muda haunitoshi nitakupa mfano utaenda ufuatilia", akasema Baba Halisi akijibu swali kwa nini kwa nini palipoandikwa Mungu Kanisa Halisi husema Chanzo Halisi.Baadhi ya wageni, uzo na watekeleza sauti wakimsikiliza Baba halisi wakati akijibu maswali.Baadhi ya wageni, uzao na watekeleza sauti wakimsikiliza Baba Halisi wakati akijibu maswali.Baadhi ya wageni, uzao na watekeleza sauti wakimsikiliza Baba Halisi wakati akijibu maswali.
Baadhi ya Maharusi, wageni, uzao na watekeleza sauti wakimsikiliza Baba Halisi wakati akijibu maswali.
Baadhi ya wageni, uzao na watekeleza sauti wakimsikiliza Baba Halisi wakati akijibu maswali.
Baadhi ya uzao na watekeleza sauti wakimsikiliza Baba Halisi wakati akijibu maswali.
Nyumba ya Ibada ikiwa imefurika Uzao, Watekeleza sauti na Wageni.
Baadhi ya wageni, uzao na watekeleza sauti wakiwa wamesimama kwenda kuchukua chakula ili kushiriki (kula) kama alivyosema Baba Halisi mwanzoni mwa Ibada.
Baadhi ya wageni, wakihudumiwa chakula.
Mgeni akiwa na chakula na soda baada ya kuhudumiwa.
Wageni wakishiriki chakula.
Wageni wakishiriki chakula.
Wageni wakishiriki chakula.
Wageni wakishiriki chakula.
Wageni wakishiriki chakula.
Wageni wakishiriki chakula.
Mmoja wa maharusi akihudumiwa chakula.
Waimbaji wakitumbuiza wakati wageni, uzao na watekeleza sauti wakishiriki chakula.
Wageni wakishiriki chakula.
Baadhi ya maharusi wakishiriki chakula.
Ushiriki wa chakula ukiendelea hadi nje.
Ushiriki wa Chakula ukiendelea nje.

Sheikh kutoka Kituo kimoja cha Kiislam akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wageni waliohudhuria Ibada hiyo.
"Umesema umeniletea wajukuu, Ila sasa mimi ni Baba Halisi sina wajukuu, wakubwa na wadogo wote ni wanangu", akasema Baba Halisi.

Maharusi wakitoka baada ya kuruhusiwa na Baba Halisi.
=====
Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya juu waliohudhuria Ibada hiyo wakiwa mbele baada ya kuitwa na Baba Halisi.
Uzao akitoa ushuhuda ya uponyaji uliofanywa na Baba Halisi.
Baba Halisi akiwaita wote wanaohitaji uponyaji wowote awahudumie bure.

Baba Halisi akimfanyia uponyaji mgeni aliyehitaji uponyaji.
Baba Halisi akiwa amekanyaga mguu wa binti huyo kumfanyia uponyaji.
Baba Halisi akiibariki juisi kisha akampa binti huyo akainywe kupata uponyaji.
Akamkabidhi juisi hiyo.

Baba Halisi akiendelea kuachilia uponyaji,
Licha ya Ibada hiyo kwenda kwa muda mrefu lakini wote waliohudhuria hakuna aliyeondoka kabla ya mwisho.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana