Songea, Ruvuma
Aliyewahi kuwa Mpambe wa Rais (ADC) wakati wa Rais Dk. Jakata Kikwete na Hayati Dk. John Magufuli, Meja Jenerali Mbaraka Mkeremi, ametunikiwa Shahada ya Uzamivu ya Udaktari wa Falsafa (Doctor of Philosophy-PhD) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Ametunukiwa PhD hiyo katika Mahfali ya Chuo Kikuu hicho, yaliyofanyika katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma, leo Disemba 14, 2023.
Eneo lake la utafiti aliofanya lilikuwa ni “Assessing the effectiveness of the United Nations Peacekeeping Operations: The case of Democratic Republic of Congo and Sudan. Mahafali hayo yamefanyika katika Uwanja wa Majimaji Songea.
Kutoka kuwa ADC alipanda cheo na kuanza majukumu mengine.
Meja Jenerali Dk. Mbaraka Mkeremi akifurahi baada ya kutunukiwa PhD, leo.




Post a Comment