Na Yahya Msangi, Togo
Bwawa la kwanza la kufua umeme wa maji (hydropower dam) lilijengwa Uingereza mwaka 1878.
Liliweza kuwasha balbu moja tu. Mafanikio ya bwawa hili ndiyo yalihamasisha ujenzi wa mabwawa duniani. Haraka mabwawa yakaanza kujengwa Marekani - Grand Rapids, Michigan (1880), Ottawa, Ontario (1881), Dolgeville, New York (1881), and Niagara Falls, New York (1881).
Kazi kuu ya umeme kutoka mabwawa hayo ilikuwa kutoa nishati kwenye vinu vya pamba na makazi ya wenye mashamba na vinu vya pamba. Kwa watumwa ilikuwa marufuku kupewa umeme.
Hebu fikiri kipindi bwawa linawasha balbu moja tu? Hali ilikuwaje haswa kwa walalamishi sampuli yako?
Nyumbu sampuli yako ilimuonaje huyo mwenye balbu? Ni matusi kilo ngapi zilimshushia mwenye balbu?
Historia hii inakufundisha nini weye nyumbu?
Nawatakia sikukuu yenye umeme nyumbu wote.
Asanteni kwa usikivu na uvumilivu.
Yahya Msangi
Post a Comment