Ikulu, Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Disemba 19, 2023, ameivunja Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kumteua Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Benki ya Azania Dk. Rhimo Simeon Nyansaho kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo.
Taarifa ya Ikulu imesema, Rais amefanya uamuzi na uteuzi huo kufuatia nafasi hiyo kubaki wazi baada ya Disemba 18, 2023 kumteua aliyekuwa akishika nafasi hiyo Meja Jenerali Paul Kisesa Simuli kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda.
Taarifa imesema Uteuzi huu unaanza mara moja.

Post a Comment