Featured

    Featured Posts

UWT YATOA MSAADA KWA ALMANUSURA WA MAFURIKO ALIYEJIFUNGUA HANANG







Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake Tanzania UWT, Mary Chatanda ameongoza na  Kundi la wanawake  wa Jumuiya hiyo  kwenda  kukabidhi zawadi  kwa Mama aliyejifungua mara baada ya  kutolewa  kwenye  tope.


Akizungumza  leo  Mara baada ya Kukabidhi Vifaa hivyo Mwenyekiti Chatanda amesema UWT  imeamua kurudi tena kuja kukabidhi Nguo za mama  , mtoto mchanga na mabinti wawili wa mama huyo ambae ni wahanga mara baada ya kuona kuwa anahuhitaji wa haraka hili kuweza kumsitiri mama huyo na watoto wake.


"Leo tumekuja  na magodoro, Blanketi, shuka, Nguo za Mtoto, nguo za Mama, nguo za watoto wa kike waliookolewa mabeseni, fedha taslimu laki sita na ishirini pamoja na mahitaji mengine ambayo yatamsaidia kuanzia maisha  kwa sasa “amesema Chatanda 


Aidha katika  Msafara huo wa Mwenyekiti Chatanda ameongozana na Wadau  wa Maendeleo Husein Gonga ambae ametoa Bati 50 kwa ajili ya Mama huyo ajengewe nyumba  na ahadi mbali mbali kutoka kwa Wabunge wanawake walioambatana nae .

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana