Nyamanzi, Zanzibar
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umeendelea kutoa elimu ya Hifadhi ya Jamii kwenye Maonesho ya 10 ya Biashara ya Kimataifa ya Zanzibar yanayofanyika kwenye viwanja vya Nyamanzi, Wilaya ya Magaharibi, Zanzibar.
Maonesho hayo yalizinduliwa na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi, Januari 10, 2024, yakiwa ni sehemu ya shamrashamra za Sherehe ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo ilele chake ilifanyika juzi, Januari 12, 2024.
Maonesho hayo ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Biashara Mtandao kwa Maendeleo ya Biashara na Uwekezaji” yanawashiriki zaidi ya 500 kutoka taasisi mbalimbali za bara na visiwani, wakiwemo wajasiriamali na yanatarajiwa kufikia kilele Januari 19, 2024.
PSSSF imetumia fursa hiyo kuwahudumia wananchama wake ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya matumizi ya teknolojia katika kupata huduma za Mfuko, kupitia PSSSF Kiganjani.
Huduma hizo ni pamoja na kupata taarifa za Mafao yatolewayo na Mfuko, Taarifa za Michango, Taarifa za Uwekezaji ikiwa ni pamoja na Wastaafu kujihakiki.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba (katikati) akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo katika banda la PSSSF kwenye Maonesho ya 10 ya Biashara ya Kimataifa ya Zanzibar, kwenye viwanja vya Nyamanzi, kisiwani Unguja Januari 14, 2024.
Post a Comment