Featured

    Featured Posts

CHATANDA AKAGUA UJENZI WA JENGO LA MAMA NA MTOTO KONDOA




 


Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Taifa UWT na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa Mhe. Marry Chatanda, leo tarehe 22 Novemba 2023 ametembelea Hospitali ya Mji Kondoa ikiwa ni ziara yake kwa Halmashauri hiyo kujionea Miradi mbalimbali iliyotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita.


Akiwa Hospitalini, hapo Mhe. Chatanda amewajulia hali wagonjwa waliokuwepo kwenye jengo la dharura ambalo limejengwa kwa zaidi ya Shilingi Milioni 300 ikiwa ni fedha kutoka Serikali Kuu chini ya Mpango wa UVIKO.


Aidha, Mhe. Chatanda ametembelea jengo jipya la Mama na Mtoto ambalo lipo katika hatua za mwisho za utekelezaji wake baada ya kupata fedha kiasi cha Shilingi Milioni 900 za ukarabati wa Hospitali ya Mji ambapo majengo matatu yamejengwa ikiwemo jengo la upasuaji, mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia Maiti (Mochwari).


Hata hivyo, ameagiza kufanyiwa marekebisho yaliyoonekana katika majengo hayo ikiwemo kumalizia jengo la mama na mtoto ili wananchi waanze kupata huduma katika jengo hilo ikiwa ni pamoja na wahandisi kusaidia kutoa utaalam ili kujenga majengo yaliyo bora.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana