Featured

    Featured Posts

MENEJA TARURA KYERWA AOMBWA KUONGEZA KASI UJENZI WA BARABARA

Na Lydia Lugakila, Kyerwa.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya  Kyerwa Mkoani Kagera wamemuomba Meneja wa wakala wa barabara za Vijijini na mjini -TARURA wilayani humo kuongeza kasi ya utengenezaji wa barabara na Karavati ili kurahisisha usafirishaji kwa haraka katika maeneo korofi.


Hayo yalibainishwa  katika kikao cha   hitimisho cha baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Rweru Plaza.


Wakizungumza katika kikao hicho baadhi ya madiwani ,Diwani akiwemo diwani wa kata ya Kakanja Clepin Bernard, na Diwani wa Kata Nyaruzumbura Joel Stephen wamemtaka Meneja TARURA kuwasiliana na madiwani kabla ya matengenezo ya karavati ili kumuonyesha maeneo korofi zaidi.


Naye Diwani wa Kata ya Bugara Ferdinand Bishanga amehoji ni lini utakamilika  ujenzi wa barabara km 8.47 ya kibwera-Mugaba 


Akijibu hoja za Madiwani Fundi Sanifu Mkuu, Filbert Eustace amesema wanaendelea kuongeza kasi ili kuhakikisha barabara zote ziilizotengewa fedha zinakamilika kwa wakati pamoja na ujenzi wa makaravati.


Eustace pia amezitaja changamoto hasa katika barabara zinazofunguliwa kuwa ni pamoja na Wananchi kutotoa ushirikiano na kulalamika kuwa wanaharibiwa mazao,pamoja na ujenzi wa nyumba kando na barabara.



author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana