Featured

    Featured Posts

UCSAF YACHANJA MBUGA KUHAKIKISHA HUDUMA ZA MAWASILINO ZINAMVAA KILA MTANZANIA, YAJIPANGA KUKOPESHA SIMU WANYONGE VIJIJINI

Na Bashir Nkoromo, Blog ya Taifa ya CCM, Dar es Salaam
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ulianzishwa na Serikali kwa Sheria ya Bunge nambari 11 ya mwaka 2006 Sura ya 422 kwa lengo la kupeleka na kufanikisha huduma ya mawasiliano kwa wananchi waishio katika maeneo machache ya mijini na maeneo mengi yaliyo mbali vijijini yasio na mvuto wa kibiashara kwa watoa huduma ya mawasiliano, Mwaka 2009 kanuni za kuhuisha Mfuko zilipitishwa na Mfuko kuanza kazi Julai  Mosi, 2009.

Pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu malengo mengine ya (UCSAF) ni kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu na pia kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu.

Malengo mengine ya (UCSAF) ni kutengeneza mfumo kwa ajili ya upatikanaji wa mitandao ya mawasiliano na huduma rahisi na zenye ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji katika soko la kiushindani, kuhamasisha utoaji wa huduma bora katika viwango nafuu na kuhakikisha kuwa teknolojia ya habari na mawasilianpo inapatikana vijijini na sehemu za mijini zenye mawasiliano hafifu kwa bei nafuu, kuhakikisha upatikanaji wa huduma za wote kwa kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano kupitia ushiriki wa sekta binafsi.

Miongoni mwa kazi ilizopewa (UCSAF) ni kubaini maeneo ya miradi ya mawasiliano ambayo yanaweza kupata ruzuku kutoka katika Mfuko, kuweka vigezo vya utambuzi wa maeneo ya vijiji vinavyohitaji na ambavyo haviwezi kupata huduma ya mawasiliano kwa sababu havina mvuto wa kibiashara, kuweka vigezo sahihi vya utoaji wa ruzuku kwa watoa huduma za Mawasiliano kwa ajili ya kupeleka mawasiliano katika maeneo yaliyoainishwa.

Kutathmini miradi ya mawasiliano inayowasilishwa na waatoa huduma ili kupewa ruzuku na Mfuko, kufanya tafiti mbalimbali na kufuatilia maendeleo ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na yale yasiyo na mvuto wa kibiashara, kuishauri Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusiana na mambo yanayohusu Mawasiliano kwa wote.

Kuangalia njia sahihi za kutoa ruzuku kwa ajili ya kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini na katika maeneo yasiyo na mvuto kibiashara, kusimamia kisheria mikataba ya utekelezaji wa majukumu ya utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote, kuweka utaratibu mzuri wa kusimamia, kukokotoa na kukusanya tozo za Mawasiliano kwa wote kutoka kwa watoa huduma, kukokotoa, kupanga na kugawanya ruzuku za mawasiliano kwa wote.

Hali kadhali, kupendekeza sera madhubuti za Mfuko kwa Waziri wa Sekta ya Mawasiliano, kushauriana na Kushirikiana na Wizara za Serikali, Idara au Mamlaka inayojitegemea kuhusiana na masuala ya huduma kwa wote.

Sasa ikiwa hayo ndiyo malengo ya serikali kuanzisha UCSAF,  Je, Mfuko huo hadi sasa umeweza kukidhi kiu ya serikali hasa hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuhakikisha huduma za Mawasiliamo zinamfikia kila Mtamzania?

Nafahamu wapo wanaoweza kukiri kwamba hakika UCSAF imekidhi kiu ya serikali, lakini pia wapo ambao hawawezi kukiri hilo na sababu kubwa itakuwa ni kwa sababu hawaiapata fursa ya kuujua utendaji na yale yaliyokwisha fanywa na yanayoendelea kufanywa na Mfuko huo uhakikisha unakidhi kiu hiyo ya serikali.

Mimi nilikuwa miongoni mwa waliokuwa hawajui kwamba kwa muda mrefu tayari UCSAF imeshafanya mambo makubwa ambayo kila atakayeyajua bila shaka ataupa kongole Mfuko huo, na kukiri kwamba, naam UCSAF serikali yaikukosea kuianzisha.

Leo Novemba 21, 2023 ndiyo nimebahatika kuyajua kindakindaki yale ambayo imekuwa ikiyafanya UCSAF, wakati Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo wa Mawasiliano kwa wote Justina Mashiba, alipoeleza kwa zaidi 45 utendaji wa Mfuko huo, katika kikao kazi baina ya UCSAF na Wahariri, Waandishi wa Habari ambao nilihudhuria wa mwaliko rasmi kwa nafasi yangu ya Msimamizi Mkuu wa Blog hii ya Taifa ya CCM.

Kikao kazi hicho, ambacho kililenga kuujengea umma uelewa mpana juu ya utendaji wa Mfuko huo kupitia Wahariri wa Habari, kiliandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR), na kufanyika jijini Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam, OTR ikiwa imewakilishwa na Mkuu wa Kitengo cha Masiliano ya Umma Thobias Makoba na Afisa Habari Mwandamizi Sabato Kosuri.

Hakika katika maelezo ya Afisa Mtendaji Mkuu Justina Masiba alieleza yaliyoshiba, ambayo kwa kweli yote yalivutia mno ikiwemo alilosema mwamba UCSAF inajipanga kuwakopesha simu wananchi wa Vijijini ili kuhakikisha wanakuwa na mawasiliano.

Kwa kuwa nahofia kutia au kupunguza sukari mazuri aliyosema Afisa Mtendaji Mkuu huyo, nakumba baada ya picha na 'Captions' usome wasilisho lake lote aliloliwasilisha kwenye kikao kazi hicho.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Justina Mashiba, akiwasilisha utendaji wa Mfuko huo, katika kikao kazi baina ya UCSAF na Wahariri, Waandishi wa Habari, ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) na kufanyika jijini Dar es Salaam, leo Novemba 21, 2023. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji UCSAF Albert Richard, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari Tanzania (TEF) Deodatus Balile, Mkuu wa Kitengo cha Masiliano ya Umma OTR Thobias Makoba na Afisa Habari Mwandamizi OTR Sabato Kosuri. (Picha zaidi BOFYA HAPA)

SASA WASILISHO LA UCSAF HILI HAPA👇

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana