Na Bashir Nkoromo, Blog ya Taifa ya CCM
Licha ya kuwa siyo taasisi ya kibiashara, Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), imeweza kuuchangia zaidi ya Sh. Bilioni 2 (Sh.2,289,500,000) Mfuko Mkuu wa Serikali katika miaka miwili ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia Suluhu Hassan, miaka ya bajeti ya 21/22 na 22/23.
Hayo yamesemwa na Mkemia Mkuu wa Serikali Dk. Fidelice Mafumiko, wakati akitoa wasilisho kueleza Mafanikio ya Mamlaka hiyo (GCLA) kwa miaka miwili ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia, katika Kikao Kazi baina ya GCLA na Wahariri wa Habari, kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa hazina (OTR) na kufanyika Jijini Dar es Salaam, leo Novemba 30, 2023.
Kwa mujibu wa OTR inayosimamia Uwekezaji wa Serikali na mali nyingine za Serikali katika Mashirika ya Umma na Kampuni ambazo Serikali ina hisa au maslahi ya Umma kwa niaba ya Rais na kwa ajili ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kampuni na Mashirika au taasisi za kibishara ndizo ambazo huhitajika kuuchangia Mfuko Mkuu wa Serikali.
Unataka kujua mengi zaidi yaliyofanywa na GCLA katika miaka miwili ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia? Taarifa kamili ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dk. Mafumiko hii hapo👇



































 |
| Mkemia Mkuu wa Serikali Dk. Fidelice Mafumiko, akitoa wasilisho kueleza Mafanikio ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kwa miaka miwili ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia, katika Kikao Kazi baina ya GCLA na Wahariri wa Habari sanjari na waandishi wa habari, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, leo Novemba 30, 2023. |
 |
| Mkuu wa Kitengo cha Habari na Masiliano ya Umma kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Thobias Makoba, akizungumza katika kikao kazi baina ya GCLA na Wahariri, Waandishi wa Habari, ulioratibiwa na OTR na kufanyika jijini Dar es Salaam, leo Novemba 30, 2023. |
 |
| Afisa Mwandamizi wa Habari na Masiliano ya Umma kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Sabato Kosuri, akiongoza kikao kazi baina ya GCLA na Wahariri, Waandishi wa Habari, ulioratibiwa na OTR na kufanyika jijini Dar es Salaam, leo Novemba 30, 2023. |
 |
| Mkemia Mkuu wa Serikali Dk. Fidelice Mafumiko (katikati), akiwa yuko meza kuu tayari kuwasiliaha wasilisho kueleza Mafanikio ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) kwa miaka miwili ya Uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita Dk. Samia, katika Kikao Kazi baina ya GCLA na Wahariri wa Habari sanjari na waandishi wa habari, kilichofanyika Jijini Dar es Salaam, leo Novemba 30, 2023. |
 |
BBaadhi ya wakuu wa Idara za GCLA wakiwa kwenye kikao hicho
|
 |
Baadhi ya Wahariri na waandishi wa habari wakiwa kweye kikao kazi hicho.
|
 |
| Baadhi ya Wahariri na waandishi wa habari wakiwa kweye kikao kazi hicho. |
 |
| Baadhi ya Wahariri na waandishi wa habari wakiwa kweye kikao kazi hicho. |
 |
| Mkemia Mkuu wa Serikali Dk. Fidelice Mafumiko, akijibu maswali ya baadhi ya wahariri na waandishi wa habari, baada ya kuwasilisha wasilisho kwenye kikao hicho. |
 |
| Afisa Mwandamizi wa Habari na Masiliano ya Umma kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTR) Sabato Kosuri akisikiliza kwa makini wakati Mkemia Mkuu wa serikali akijibu maswali, |
 |
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Angelina Akilimali akitoa salamu za shukurani mwishoni mwa kikao kazi hicho, alianza kwa kuomba wote kusimama na 'kupasha' makofi kupongeza wasilisho alilotoa Mkemia Mkuu..
|
Author Name
Author Description!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment