Marekani imekifuta kibali cha kuingia nchini humo cha mwendesha mashitaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC, Fatou Bensouda baada ya mwanasheria huyo kuanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano wa vikosi vya Marekani kufanya uhalifu wa kivita nchini Afghanistan.
Wataalamu wa haki za binadaamu wa Umoja wa Mataifa wameiita hatua hiyo kuwa ni uingiliaji usiofaa kwa mahakama hiyo ya kudumu ya kimataifa inayoshughulikia uhalifu wa kivita.
Hata hivyo wamesema wanajua hatua hiyo haitaathiri uwezekano wa Bensouda kuingia Marekani kufanya majukumu yake katika Umoja wa Mataifa.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo mwezi uliopita alielezea uwezekano wa Marekani kuchukua hatua hiyo kwa watumishi wa ICC wanaochunguza madai kama hayo dhidi ya Marekani na washirika wake.
Post a Comment