RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Alim Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuufungua Msikiti wa Masjid Maryan Mtende Wilaya ya Kusini Unguja kushoto Mfanyabiashara Maarufu Zanzibar Bw. Said Salim Bakhressa, hafla hiyo imefanyika katika Kijiji hicho leo Aprili 5, 2019. Rais wa Zanzibar na Mwenyekitin wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia Waumini wa Dini ya Kiislam wa Kijiji cha Mtende Wilaya ya Kusini Unguja wakati wa hafla hiyo ya Ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende, uzinduzi huo umefanyika leo 5-4-2019. Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akisoma dua baada ya kumalizika hafla ya Ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende Wilaya ya Kusinu Unguja, kushoto Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, Mfanya Biashara Maarafu Tanzania Bw. Said Salim Bakhressa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Khamis Maalim Juma na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe Said Hassan, wakiitikia dua wakati wa hafla hiyo. Baadhi ya Wananchi wa Mtende Wilaya ya Kusini Unguja wakifuatilia hutuba ya ufunguzi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, wakati wa ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende Mkoa wa Kusini Unguja leo 5-4-2019. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora na Utumishi wa Umma Zanzibar na Mwakilishi wa Jimbo la Makunduzi Mhe. Haroun Ali Suleiman akitowa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa Masjid Maryam Mtende Wilaya ya Kusini Unguja leo, baada ya uzinduzi wake leo.
Mwananchi wa Kijiji cha Mtende Wilaya ya Kusini Unguja Sheikh Khamis Ramadhan Mbarak. akisoma risara ya Wananchi wa Kijiji cha Mtende wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi wa Msikiti wao Mpya uliojengwa kwa Ufadhili wa Bw. Said Salim Bakhressa..(PICHA NA IKULU YA ZANZIBAR).
Author Name
Author Description!
Get Free Email Updates to your Inbox!
Post a Comment