Featured

    Featured Posts

WACHINA, WATANZANIA NA WAZAMBIA WAADHIMISHA MIAKA 45 YA TAZARA

NA PASCHAL DOTTO-MAELEZO

Ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zambia na Jamhuri ya Watu wa China, Wazadi kuimarika kutokana na uwepo wa miundombinu ya ushafirishaji  kupitia  Tanzania Zambia Railway TAZARA, iliyojengwa kwa ushirikiano wa Tanzania, Zambia na China mwaka 1975.na  Wasisi wa mataifa hayo ni Mwalimu Julius  Nyerere (Tanzania), Dkt. Kenneth Kaunda (Zambia)  na Mao ze Dong Rais wa Jamhuri ya Watu wa China.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Paramagamba kabudi,leo ameongoza maadhimisho ya kumbukizi ya Mashujaa waliojenga reli ya TAZARA, ambapo yamefanyika   katika makaburi ya mashujaa hao yaliyoko Gongo la Mboto, Jijini Dar es Salaam.

Akielezea historia ya reli hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Paramagamba Kabudi alisema Ujenzi wa reli hiyo ni muhimu kwa sababu, Benki ya Dunia wakati huo walikataa kujenga wakisema haukuwa na faida, kadhalika nchi za Ulaya zilikataa zikidai ujenzi huo haikuwa na faida, Lakini taifa la wakina likawa tayari kujenga.

“Mwalimu Julius  Nyerere, Dkt. Kenneth Kaunda Rais wa Zambia pamoja na Mao ze Dong Rais wa Jamhuri ya Watu wa China waliamua kujenga reli hii, siyo kwamba China walikuwa tajiri sana kama walivyo sasa, hapana walifunga mkanda, kwa hiyo siku ya leo ni muhimu sana kiuchumi, kiutamaduni na kijamii”,  Prof. Paramagamba kabudi , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amekumbushia

Prof. Kabudi alisema kuwa katika maadhimisho ya  mwaka huu, ni muhimu kwa Tanzania, kwani kwa sasa China ina mpango wa kutekeleza mradi mkubwa uitwao Sea Belt and Road Initiatives unaolenga ujenzi wa miundombinu kuunganisha Afrika, Asia, Ulaya kwa kutumia miundombinu ya barabara, ndege pamoja na reli ambapo Tanzania itapata ushirikiano mzuri katika masuala ya usafiri wa anga.

Aidha Prof. Kabudi alisema kuwa katika maadhimisho ya mwaka marejeo yataweza kuimarisha ushirikiano na kuwa ni msingi bora wa kuanzisha mahusiano mapya, hususani katika usafiri wa anga na akaongeza kuwa mwaka huu Shirika la ndege la Tanzania litaanza safari zake toka Dar es Salaam mpaka Wanzhu Nchini China.

“kwa sisi mwaka huu sherehe hii ni muhimu sana, kwani tunatarajia kuanza safari za ndege yetu Air Tanzania kuruka moja kwa moja kutoka Dar es Salaam mpaka Wanzhu nchini China, hivi karibuni yaweza kuwa mwaka huu (utekelezaji) katika taratibu zote zitakamilika na safari zitaanza rasmi.”, Prof. Paramagamba

WaziriKabudi aliongeza kuwa safari hiyo ya ndege ya Air Tanzania itaongeza idadi ya watalii kuwa wengi kuja Tanzania kutoka China, wafanyabiashara kutoka ndani na nje na kuweza kwenda moja kwa moja Wanzhu, akasema pia wawekezaji kutoka China watawezesha Serikali kupata mapato mengi.

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke alisema kuwa siku ya kumbukizi kwa mashujaa wa ujenzi wa reli ya TAZARA ni siku muhimu na kwamba  inaleta kumbukumbu ya uhusiano kati ya nchi hizo tatu.

“hii ni siku maalumu kwa sababu ni siku ya kuadhimisha kumbukizi ya kufa kwa mashujaa wetu hawa, Mainjinia pamoja na wataalamu mbalimbali walioshiriki katika ujenzi huu, na kufariki, na hili adhimisho limefanyika hapa Tanzania kwa sababu tunaushirikiano wa muda mrefu tangu ujenzi wa reli mwaka 1975”, Balozi wa China, Wang Ke alisema.

Wang Ke alisema kuwa maadhimisho hiyo ni msingi mzuri wa kujenga uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania, Zambia na China kwani maadhimisho hayo yanatukumbusha matumizi ya reli ya TAZARA katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika, ikiwemo Zambia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Paramagamba Kabudi akihutubia katika siku ya kumbukumbu ya Mashujaa waliojenga reli ya TAZARA, wakati wa zoezi la kuweka mashada ya maua iliyofanyika leo (Ijumaa April 5, 2019), katika makuburi ya mashujaa hao yaliyoko Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam, waliosimama kulia ni Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akiwa pamoja na  viongozi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Paramagamba Kabudi akihutubia katika siku ya kumbukumbu ya Mashujaa waliojenga reli ya TAZARA, wakati wa zoezi la kuweka mashada ya maua iliyofanyika leo (Ijumaa April 5, 2019), katika makuburi ya mashujaa hao yaliyoko Gongo la Mboto Jijini Dar es Salaam, waliosimama kulia ni Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akiwa pamoja na  viongozi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi (watatu kulia), akipata maelezo kuhusu Mashujaa waliojenga reli ya TAZARA, katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mashujaa hao yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam leo (Ijumaa April 5, 2019), kushoto ni Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke akiwa pamoja na  viongozi wengine wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China na Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi (wapili kulia) na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke (katikati) wakiweka mashada ya maua katika moja ya makaburi ya Mashujaa waliojenga reli ya TAZARA katika maadhimisho ya siku ya mashujaa hao iliyofanyika leo (Ijumaa April 5, 2019) Jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi (kulia) na Balozi wa China Nchini Tanzania, Wang Ke, wakiweka mashada ya maua katika mnara wa makaburi ya Mashujaa waliojenga Reli ya TAZARA, katika maadhimisho ya siku ya mashujaa hao iliyofanyika leo (Ijumaa April 5, 2019) Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi akiweka maua kwatika  moja ya makaburi ya Mashujaa waliojenga reli ya TAZARA, katika maadhimisho ya siku ya mashujaa hao iliyofanyika leo (Ijumaa April 5, 2019) Jijini Dar es Salaam.




author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana