Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katavi Amos Makalla amekabidhi rasmi ofisi kwa mkuu mpya wa mkoa huo, Juma Homera.
Akikabidhi, amesema amekitumikia Chama cha Mapinduzi na Umoja wa vijana kwa muda mrefu kwa hiyo vipaji na uzoefu alionao vitamfanya andelee kuwa Kada wa mstari wa mbele wa Chama
Makalla, amemshukuru Rais Dk. John Magufuli kwa kumuamini kwa nafasi ya Ukuu wa Mkoa kwa miaka minne.
Amesema mwaka 2015 Alipokosa Ubunge ilitosha yeye kubaki kuwa mwananchi na mwana CCM tu huko Mvomero lakini Rais wa awamu ya nne Dk. Jakayla Kikwete alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na baadaye Rais Dk. Magufuli akamteua kuwa mkuu wa mkoa wa Mbeya na halafu Katavi.
Amewashukuru wananchi na viongozi wa ngazi zote dini na serikali kwa kumpa ushirikiano katika Kipindi cha miezi 10 alipokuwa mkuu wa mkoa wa Katavi na Amewaomba wananchi na viongozi wampe ushirikiano wa kutosha mkuu wa mkoa Mpya Juma Homela
Post a Comment